Tafuta

Papa katika misa amesema ni vigumu kufikia makubaliano ya amani iwapo hakuna unyenyekevu, upole na uvumilivu Papa katika misa amesema ni vigumu kufikia makubaliano ya amani iwapo hakuna unyenyekevu, upole na uvumilivu  (Vatican Media)

Papa:Unyenyekevu,upole na uvumilivu ni msingi wa kujenga amani

Ni lazima kuwa na matendo ya dhati na kuimarisha umoja wa dunia ya leo mahali ambapo hata taasisi za kimataifa zinahisi kutokuwa na uwezo wa kukabiliana na suala la ujenzi wa amani. Kwa mtazamo wa Papa Francisko na kwa mujibu wa Mtakatifu Paulo, unyenyekevu, upole na uvumilivu ni njia mwafaka katika kujenga na kukuza amani

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ili kuweza kupata njia ya amani katika dunia inapitia unyenyekevu, upole na uvumilivu  katika jamii zetu, lakini hata katika familia zetu. Ndiyo wazo kuu la Baba Mtakatifu Francisko alilolitoa wakati wa Misa ya asubuhi tarehe 26 Oktoba 2018, Akitafakari kuhusu somo la kwanza la siku, kutoka  barua ya Mtakatifu Paulo mtume kwa Waefeso. Papa Francisko anakumbuka Paulo katika upweke wake kwenye gereza, na anawalezea wakristo ukweli na udhati wa utenzi wa kuwa na umoja unao waalika katika hadhi ya wito.

Ni vigumu kufikia makubaliano ya amani

Upweke uliomsindikiza mtume Paulo hadi kifo chake, kilichomjia huko Tre Fontene, ulitokana na wakristo kuhangaikia sana mapambano yao ya ndani. Hata hivyo Yesu mwenyewe kabla ya kufa , wakati wa Karamu ya mwisho, alimwomba Baba yake neema ya umoja sisi sote.  Lakini pamoja na hayo, Papa anabainisha, “ tumezoea tayari kuvuta hewa ya migogoro”. Kila siku kupitia luninga, na magazeti wanazungumza migogoro mmoja baada ya mwingina na vita, lakini bila amani hakuna umoja”. Kwa kusisitiza zaidi Papa anasema, ansema, wanafanya mikataba ya kusitihsa kila aina ya mogogoro, lakini baadaye migogoro hiyo haitiliwi maanani. Kwa namna hiyo, shughuli za silaha, maandalizi ya vita na uharibifu unaendelea mbele.

Hata taasisi za kidunia leo hii tunaona kuwa na matashi mema ya kuanda mipango ya kusaidia umoja wa kibinadamu, wa amani, lakini wanahisi kukosa kutokuwa na uwezo wa  kufikia makubaliano ya dhati,  kwa maana utasikia zipo kura za hapo, au kuna faida pale … na hivyo inakuwa vigumu kufikia makubaliano ya kweli ya amani. Na wakati huohuo, watoto hawana chakula, hawaendi shuleni na hawaelimiki na hakuna mahospitali kwa sababu vita vimeharibu kila kitu. Ipo kasumba yetu ya uharibifu na vita na tabia ya  ukosefu wa muungano. Ipo tabia ambayo inapandikiza adui ndani ya mioyo yetu, muharibifu  huyo na mkoseshaji wa umoja  ni  shetani.  Katika sehemu hiyo Paulo anatufundisha safari katika kuelekea umoja  na ambayo anasema, umoja umefunikwa  kwa maana kuna vizuizi ambavyo tunaweza kusema na vizingiti vya amani. kwa maana hiyo Papa anasisitza, “amani inapelekea umoja”.

Kufungua moyo, kwa maana ya kuwa na unyenyekevu, upole na moyo mkuu

Kutokana na maelezo hayo ndipo , kuna mwaliko wa namna ya kuwa wenye kustahili na ambao ndiyo  wito tulio pokea kwa unyenyekevu, upole na moyo mkuu. Ili kutengeneza amani na umoja kati yetu, tunahitaji kuwa wanyeneyekvu, wapole na moyo mkuu hasa sisi ambao  tumezoea kukalia watu vitako na kupigizana kelele, Baba Mtakatifu ameshauri. Hachilia mbali lakini fungua moyo wake.  Je inawezekana kutengeneza amani kwa mambo hayo madogo matatu? Ndiyo, kwani hiyo, ndiyo safari. Unaweza kuufikia umoja? Ndiyo  maana huo ndiyo umoja, ikiwa na maana ya kujikita katika suala la  unyenyekevu, upole na uvumilivu ndiyo safari yenyewe ya kuweza kufikia amani.

Mtakatifu Paulo amejikita kufanya matendo ya dhati  na anaendelea kushauri sana juu ya matendo hayo kuwa, "kwa kuchuliana katika upendo na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katia kifungo cha amani". Papa Francisko anaongeza: "kuchukuliana mmoja na  mwingine siyo kitu rahisi na daima hujitokeza hukumu, lahumu ambazo baadaye hupelekea kutengena na kuleta umbali…

Makubaliano ya amani tangu mwanzo ni rahisi

Hayo yote hutokea  hata  inapojitokeza katika umbali kati ya watu wanaoishi ndani ya familia moja. Na shetani anafurahia hilo, maana ndiyo mwanzo wa vita. Kwa maana ushauri ni ule wa kuchukuliana kwa sababu sisi sote tunazo sababu za kusumbuliwa, kukoa vumilivu , na kwa sababu wote tu wadhambi, na tunazo kasoro zetu. Mataktifu Paulo, anasihi kuhifadhi umoja wa roho kwa njia vifungo vya amani na kwa hakika ni chini ya mfano wa maneno ya Yesu wakati wa karamu ya mwisho akisema Mwili mmoja na Roho moja. Na wakati huo huo Paulo anaendelea mbele na kutifanya tuone upeo wa amni na Mungu; kama Yesu alivyotufanya tuone upeo wa amani katika sala kwamba: “ Baba ili wote wawe wamoja , kama ilivyo mimi na wewe katika umoja.  Katika Injili ya Siku, ya mwinjili Luka, Papa anakumbwa kuwa Yesu anatoa ushauri wa kutatufa makubaliani na mshitaki wetu wakti tuko njiani. Huo ni ushauri mzuri, amebainisha Papa kwa maana siyo nguvu kutafuta makubaliano katika mwanzo wa migogoro.

Ushauri wa Yesu ni kupatana na mshitaki ukiwa njiani 

Ushauri wa Yesu ni kwamba, unapofuatana na mshitaki wako kwenda kwa mwamuzi hapo njiani fanya bidii ya kupatanishwa naye kwanza na hivyo ni ndiyo makubaliano ya kwanza ya kufanya amani na ambayo nayhitaji unyenyekevu, ndiyo upole na uvumiluvu. Inawezekana kujena amani katika dunia nzima kwa manemo hayo madogo kwa mtindo huo ambao ulikwa wa Yesu mnyenyekvu, mpoke na anayesamehe yote. Dunia leo hii inahitaji amani, na sisi ambao tunahitahi amani katika familia zetu na katika jamii zetu. Tuanzie nyumbani mantendo hayo marahizi ya uvumilivu, upole na unyenyekevu. Twende mbele katikanjia hiyo na kutengeneza daima umoja na kuimarisha umoja ambao ni Bwana.

 

26 October 2018, 14:52
Soma yote >