Tafuta

Vatican News
Misa ya Papa katika kanisa la Mtakatifu Marta:Malaika ni msaada maalum wa kutusindikiza katika hija yetu Misa ya Papa katika kanisa la Mtakatifu Marta:Malaika ni msaada maalum wa kutusindikiza katika hija yetu  (Vatican Media)

Papa:Bwana ametoa ahadi ya malaika ili alinde watu wake!

Papa Francisko katika mahubiri ya Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, tarehe 2 Oktoba 2018, ambapo Mama Kanisa Katoliki, anaadhimisha Sikukuu ya Malaika walinzi. Amethibitisha juu ya uwepo wa malaika walinzi, ambao lakini lazima tuwasikilize ushauri wao, na utokanao na Roho Mtakatifu

Angela Rwezaula – Vatican

“Tazameni mimi namtuma malaika awatangulie safarini ili awalinde na kuwafikisha katika nchi niliyowataraishia (Kut 23,20). Ndiyo maneno ya somo la Kitabu cha Kutoka ambacho kimemwongoza Papa Francisko katika mahubiri ya Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, tarehe 2 Oktoba 2018, ambapo Mama Kanisa Katoliki, anaadhimisha Sikukuu ya Malaika walinzi. Papa Francisko, amethibitisha kuwa, ni wao kweli ambao kwa msaada maalum, Bwana anameahidia watu na hata sisi kutembea nao katika njia ya maisha.

Malaika ni dira ambayo inatusaidia kutembea

Ni katika hija ya kusindikizwa ambayo Baba Mtakatifu Francisko amekujikita kuendelea kusisitiza kwamba, lazima tusaidiwe na wasikindizaji na walinzi, ambao wanatoa dira ya kibinadamu au dira ambayo inafanana na ubinadamu na kusaidia kutazama mahali ambapo tunatakiwa kwenda. Na kwa mujibu wa Papa Francisko anasema, katika maisha inawezekana kukumbana na hatari za aina tatu.

Akifafanua hizo hatari amesema, kuna hatari ya kutotembea, akitoa mfano dhahiri kamili kwamba bi watu wangapi wanasimama, bila kutoka nje yaani katika kujishughulisha, bila kufanya chochote kile… hiyo ni hatari. Kama Injili inavyoelezea mtu yule aliyeogopa kuzalisha talanta yake. Alikwenda akaichimbia shimoni. Na kuhisi yuko na amani na utulivu.  Kwa maana alifikiri hapo hawezi kuharibu kitu, na hawezi kujiweka katika hatari.

Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa, wapo watu wengi sana hawajuhi kutembea, kwa maana wanahofia kujiweka hatarini na kusimama mahali walipo.  Lakini katika maisha yanafundisha kuwa, yule ambaye anasisima katika maisha, mwisho wake anaishia kuharibika. Ni kama maji yalitotuhama mahali pamoja na matokeo yake ni kuzaliana mbu, kwa maana mayai na viluwiluwi vingi huzaliana na kupasuka humo.  Kutokana na hiyo Malaika anatoa msaada wa kutusukuma na ili kuweza kwenda mbele.

Hatari ya kukosea na kuzungukia barabara isiyo na njia ya kutokea

Hatari nyingine mbili katika njia ya maisha yetu, Papa anendelea ni ile ya kukosea njia na ambayo mwanzo huwa ni rahisi hata kukosea; lakini hata hatari ya kuacha njia na kupotelea katika uwanja kumbwa, kwa upande mwingine ni kama ile njia isiyo kuwa na mwisho (Labrinthy, ambayo ukiingia katika njia hiyo hufikia mwisho wake. Na ndiyo maana: “Tazama Malaika anakuja ili kusaidia usipotee njia ya kutembea ndani mwake, lakini hiyo, inahitaji sala zetu na kuomba msaada wake, Papa Francisko amethibitisha.

Bwana anasema,“msikilizeni na kutiii atakachosema,wala msimwasi kwani hatawasamehe uasi wenu maana nimemtuma kwa jina langu”. Hii ina maana ya kusikiliza ushauri wake ambao daima ni Roho Mtakatifu, lakini pia ni Malaika ambaye anatupelekea mbele, pamoja na hayo, Papa ameuliza swali wote: “ je ninyi mnazungumza na Malaika wenu? Je mnatambua jina la Malaika wenu? Je mnasikiliza malaika wenu? Je mnajiweka mikononi mwake ili awapeleke katika njia au kuwasukuma mpate kuondoka?

Malaika anatuonesha njia ili kufikia Baba

Akizidi  kusisitiza amesema, nafasi ya Malaika walinzi katika maisha yetu, bado ni muhimu sana kwa sababu,  si tu wanatusaidia kutembea hija yetu ya maisha vizuri, bali hata kutulekeza ni njia gani ya kuweza kufika.  Katika Injili ya Matayo imeandikwa “Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika zao mbinguni sikuzote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni. (Mt 18:1-5,10). Katika huduma ya Malaika walinzi ipo  hata namna ya kutafakari Mungu Baba, ambaye tuomwombe Bwan atupatie neema ya kuwa na utambuzi huo na ndiyo Baba Mtakatifu anahitimisha kwamba: “ Malaika wetu si kwamba yupo nasi tu, bali yeye anatazama Baba Mungu. Malaika anaouhusiano na Yeye. Yeye ni daraja la kila siku, tunapoamka na tunaporudi usiku kitandani kulala, anatusindikiza na kutuhusisha na Baba Yetu wa Mbinguni.

Malaika ni mlango wa kila siku wa kuelekea juu ili kukutana na Bwana , kwa maana Malaika anatusaidia kwenda katika njia maana yeye anatazama Bwana na anajua ni njia gani ya kumfikia Baba. Tusisahau wasindizaji hawa wa njiani. Baba Mtakatifu amehimiza.

02 October 2018, 14:25
Soma yote >