Tafuta

Vatican News
Misa ya papa Francisko katika Kanisa la Mtakatifu Marta Misa ya papa Francisko katika Kanisa la Mtakatifu Marta  (Vatican Media)

Papa: tukumbuke daima mahali tulipo chaguliwa!

Liturujia ya siku inatazama wito wa Mtakatifu Matayo, mtoza ushuru aliye chaguliwa na Mungu na kuwa mtume. Maneno matatu, “ishara ya huruma, kuchagua na kuanzisha”, yameongoza Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri yake ya siku kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatica, katika Sikukuu ya Mtakatifu Matayo Mtume

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Matayo mtoza ushuru alikuwa ni mfisadi kwa sababu ya fedha zilikuwa zikisaliti uzalendo wake. Kuwa msaliti wa watu ni jambo baya. Mwingine anaweza kufikiria kuwa hivi Yesu alikuwa na maana gani wakati wa kuchagua watu, kwa maana kati yao alio chagua  hata  Matayo kutoka katika nafasi iliyoku inadharauliwa. Lakini pia katika mfano huo hata hisotria ya msamaria na wadhambi wengi aliwachagua na wakawa mitume.

Ndiyo mwanzo wa mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko,  katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, tarehe 21 Septemba 2018, Mama Kanisa akiadhimisha sikukuu ya Mtakatifu Matayo mtoza ushuru. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu akiendelea na tafakari hiyo anasema, baadaye katika maisha ya Kanisa, wakristo wengi na watakatifu wengi wamechaguliwa kutoka katika hali ya chini kabisa.

Na hiyo ndiyo dhamiri ambayo wakristo, tunatakiwa kuwa nayo anathibitisha Baba Mtakatifu na kufafanua kuwa lazima kujiuliza swali, je! nimechaguliwa kutoka wapi, ni wapi nimechaguliwa ili kuwa mkristo. Ndiyo ufahamu ambao unapaswa kuwa wa kudumu maisha yote na kubaki pale pale,  kadhalika kuwa na kumbukumbu ya dhambi zetu, kumbukumbu ambayo Bwana  daima amekuwa mwingi wa huruma kwa ajili ya dhambi zangu, akanichagua ili niwe mkristo na ili niwe mtume wake.

Matayo hakusahau asili yake

Papa Francisko akikumbuka matokeo ya Matayo katika kujibu  wito wa Bwana anasema: hakuwa na mavazi ya kifahari, na hata hakuanza kusema wengine, kama vile mimi ni mfalme wa mitume, na mimi ninatawala, hapana, yeye alifanya kazi katika maisha yake yote kwa ajili ya Injili.

Iwapo mtume anasahau asili yake na kuanza kuifanya kama kazi nyingineyo, anakwenda mbali na Bwana na kugeuka kuwa kama mfanyakazi yoyote yule wa ofisini; hafanyi vizuri, hivyo siyo mtume. Baba Mtakatifu anaongeza kusema: ndiyo anaweza kuwa na uwezo wa kumwonesha Yesu alivyo; atakuwa na uwezo wa kufanya mikakati ya kichungaji na mambo mengi;  lakini  mwisho wake anageuka kuwa kama mfanya biashara!,  yaani mfanya biashara wa Ufalme wa Mungu, maana amesahau kuwa  mahali alipochaguliwa. Kutokana na hilo ni muhimu kufanya kumbukumbu ya asili yetu. Na kumbukumbu hiyo lazima isindikizwe na maisha ya mtume na kila mkristo

Sisi tunakosa ukarimu lakini Bwana hakosi

Baba Mtakatifu akiendelea na mafundisho hayo anasema, badala ya kujiangalia sisi wenyewe, tumekuwa na mazoea ya kutazama wengine, dhambi zao na hata kudiriki kuwasengenya, lakini ni tabia ambayo inakufanya uishi vibaya. Ni bora kujihukumu mwenyewe na kukumbuka ni wapi Bwana alikuchagua ukae hadi kufika hapa ulipo. Bwana anapochagua, anachagua kwa ajili ya kitu fulani kilicho kikubwa. Kuwa mkristo ni jambo kubwa na zuri. Ni sisi ambao tunakwenda mbali,na kutaka kubaki nusu safari, na hiyo ni kutokana na kwamba  sisi tunakosa ukarimu na kuanza kufanya mjadala Bwana, lakini yeye anatusubiri.

Kashifa ya walimu wa sheria: Katika wito wa Matayo, anaacha upendo wake binafsi wa fedha ili kumfuasa Yesu na waliwaalika marafiki wa kikundi chache kushiriki chakula cha mchana na kuadhimisha na Mwalimu. Baba Mtakatifu anongeza kusema: kwa hiyo meza hiyo ilikaliwa na ubaya sana kati ya ubaya wa jamii ya wakati hule. Na Yesu pamoja nao. Na walimu wa sheria walikuwa wakikashifu: na  wakawaita mitume wake na kusema: hivi kwanini mwalimu wenu anafanya hivyo na watu wale? Anageuka kuwa najisi”: kula na watu najisi inaambukiza unajisi na huwezi kutakasika. Yesu anawatazama na kusema neno la tatu: “nendeni mkajifunze nini maana ya huruma ninayotaka na siyo sadaka”. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anaongeza kusema, “Huruma ya Mungu inatafuta wote, na ndiyo hiyo tu inakutaka hata wewe usema “Ndiyo nisaidie”.

Fumbo la huruma ni moyo wa Mungu:   Kwa wote wanao kashifu Yesu anawajibu kuwa, “wenye afya hawana haja ya daktari, bali wagonjwa”; “ huruma ndiyo ninataka na siyo sadaka”. Kwa kutambua huruma ya Bwana, ni fumbo Baba Mtakatifu anahitimisha na kusema,“fumbo kubwa zaidi na lililo zuri ni moyo wa Mungu”. Iwapo wewe unataka kufika kweli katika moyo wa Mungu anza kujikita katika njia ya huruma na hacha ukumbatiwe na huruma hiyo.

 

 

 

21 September 2018, 13:49
Soma yote >