Tafuta

Misa Takatifu ya Papa Katika Kanisa la Mtakatifu Marta Misa Takatifu ya Papa Katika Kanisa la Mtakatifu Marta  (Vatican Media)

Papa:Tazama dhambi binafsi siyo wengine katika njia ya ukristo!

Tubu dhambi zako binafsi kama Mtakatifu Petro kwa maana wapo watu wengi wanaishi kwa kusengenya wengine, kulaumu wengine na kamwe hawajishutumu wao binafsi. Omba neema leo hii ya kujikuta mbele ya Yesu kwa mshangao wa uwepo wake ilikupata neema ya kuhisi dhambi binafsi na mwisho kukiri kama Petro

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Wokovu wa Yesu siyo kama vipodozi vinavyoisha, bali unageuza. Na Ili kuweza kuacha  nafasi, lazima kujitambua kuwa sisi wadhambi na kujishitaki, badala ya kuwashutumu wengine. Ndiyo kiini cha mahubiri ya Papa Francisko wakati wa Misa katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican tarehe 6 Septemba 2018. Baba Mtakatifu amesisitizia juu ya ulazima kwa kujitambua dhambi, na kwamba bila ya kujifunza kujishitaki binafsi  haiwezekani kutembea katika njia ya  maisha ya kikristo.

Tafakari ya Injili ya Luka

Mahubiri ya Baba Mtakatifu yamejikita kuanzia Injili ya siku ya Mtakatifu Luka (Lk 5,1-11), mahali ambapo Yesu anamwambia Petro amfuate na kuingia katika mtumbwi, mara baada ya kuhubiri,wakati huo  akamwalika atupe jarifa na kutokea maajabu ya samaki wengi. Kutokana na tukio hilo Baba Mtakatifu anabainisha, hili ni tukio ambalo lijikite ndani ya akili kwa kuona maajabu ya samaki na lile baada ya ufufuko, ambapo Yesu aliwaomba mitume wake kama walikuwa na chochote cha kula. Kesi hizi mbili Papa anathibitisha,  kuna upako wa Petro: kwanza kama mvuvi wa watu  na baadaye  kama mchungaji. Yesu baadaye alibadili jina lake Simon na kumwita Petro. Akiwa mwisraeli mwema, Petro alijua kubadili jina maana yake ni kubadili utume kwa maana hiyo Petro alijisikia kwa maana alikuwa kweli  anampenda Yesu na maajabu haya ya samaki yanawakilisha hatua msingi ya mbele katika maisha.

Hatua ya kwanza kujitambua dhambi

Baada ya kuona nyavu karibia  zivunjike kutokana na wingi wa samaki, yeye mara moja alipiga magoti mbele ya Yesu na kumwambia: Bwana ondoka mbali nami kwa kuwa mimi ni mdhambi”. Hiyo ni hatua ya kwamba msingi ya Petro katika njia ya kufuasa, kuwa mfuasi wa Yesu katika kujishtaki binafsi: “mimi mdhambi”. Hatua ya kwanza ya Petro ni hiyo, lakini hata hivyo ndiyo hata kwa kila mmoja wetu anayetaka kutembea katika maisha ya kiroho, katika maisha ya Yesu, kuhudumia Yesu, kumfuata, ni lazima iwe njia hiyo ya kujishitaki binafsi na bila kufanya hivyo haiwezekani kutembea katika maisha ya kikristo.

Wokovu wa Yesu siyo vipodozi  tu bali ni mabadiliko ya ndani

Akiendelea na mahubiri hayo, Baba Mtakatifu amebainisha kuwa, lakini ipo hatari, kwa maana wote tunatambua tulivyo wadhambi, lakini  siyo rahisi kujishtaki binafsi kwa dhati ya kuwa mdhambi. “ tumezoea kusema mimi mdhambi na wakati huo huo  kwa namna tunavyosema; mimi bi binadamu, au mimi mzalendo wa Italia. Kujishtaki binafsi badala yake ni kuhisi kweli udhaifu huo, kuhisi umaskini  mbele ya Bwana. Na hiyo inajikita kuhisi aibu anathibitisha Baba Mtakatifu. Jambo hili si halitendeki kwa maneno tu, bali kwa moyo, ni uzoefu wa dhati kama  alivyo sema Petro  kwa Yesu, kaa mbali nami kwa sababu mimi mdhambi. Yeye alijihisi mdhambi kiukweli na baadaye akahisi kuokolewa . Wokovu unaoletwa na Yesu unahitaji maungamo ya dhati kwa namna hiyo, siyo  kama vipodozi, ambavyo vinakubadili kidogo uso : lakini mabadiliko ya kweli ili yaweze kuwapo, lazima yapate nafasi kutubu kweli  ya dhambi binafsi , kama alivyo fanya uzoefu na mshangao wa Petro.

Hacheni kusengenya wengine

Kwa maana hiyo hatua ya kwanza ya wongofu ni kujishitaki binafsi na kuona aibu, wakati huohuo  kuhisi mshangao wa kujisikia umekombolewa. Lazima tuongoke na lazima kutubu, anasisitiza Baba Mtakatifu kwa kuwaalika watafakari juu ya vishawishi ambavyo vinatufanya tuwashutumu wengine. Akifafanua amesema, wapo  watu wengi wanaishi kwa kusengenya wengine, kulaumu wengine, na  kamwe hawajishutumu wao binafsi, je ninapokwenda kuungama, jinsi gani naungama  kama kasuku? Au  Bla bla bla..nimefanya hilo na hilo… je moyoni  kweli unaguswa na kile ambacho umetenda? Mara nyingi hapana Baba Mtakatifu  anathibisha. Wewe umekwenda pale kupaka vipondozi, ili kidogo utoke mzuri. Lakini msamaha huo haukuingia ndani ya moyo wako kabisa kwa sababu hukuacha nafasi  kwa kuwa hukuwa na uwezo wa kujishtaki mwenyewe

Neema ya kuhisi dhambi za kweli

Hata ya kwanza kwa hakika ni neema yaani kila mmoja ajifunze kujishitaki binafsi na siyo wengine. Akihitimisha Baba Mtakatifu amesema, ishala ambayo mtu ambaye hajui kwamba ni mkristo ni ule ya kutojua  kujishitaki mwenye, ni ile tabia ya kawaida ya kuwalaumu wengine, kuwasengenya wengine, na  kuweka  pua katika maisha ya wengine.  Hiyo ni ishala mbaya sana, hivyo ni kujiuliza je mimi ninafanya hivyo? Ni swali zuri ambalo litoke ndani ya moyo na kuomba neema leo hii ya kujikuta mbele yake kwa mshangao wa uwepo wake na neema ya kuhisi kuwa wadhambi, lakini kwa dhati kusema kama Petro,

06 September 2018, 14:24
Soma yote >