Cerca

Vatican News
Papa anasema kuna utofauti wa  Habari njema ya Injili na mapya ya kidunia Papa anasema kuna utofauti wa Habari njema ya Injili na mapya ya kidunia   (ANSA)

Papa:Habari mpya ya Injili inabadili na kuondoa mchanganyo!

Kuna utofauti kati mapya ya habari za dunia na habari mpya iliyoletwa na Yesu. Ni kwa mujibu wa maelezo ya Papa Francisko wakati wa misa ya Asubuhi katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican ambapo amesisitiza juu ya Injili inayobadili mtu katika ukamilifu wake na hairuhusu kamwe unafiki. Ametoa onyo:njia ya mkristo ni kifodini na si kuchakachua Injili

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ndugu habari imeenea ya kuwa, kwenu kuna zinaa na zinaa ya namna isiyokuwako hata kati ya wapagani. Lakini ninyi ni wakristo na mnaishi hivi? Ni maneno ya magumu na makaripio ambayo yanaonekana katika Somo la Mtume Paulo kwa wakorinto, Mtume Paulo akiwageukia Wakristo hao wanaoendesha maisha yao kwa namna ya mchanganyo. Mtume Paulo amekasirikia sana kwani walikuwa wanajidai kuwa ni wakristo walio wazi, ambao wanaungama imani kwa Yesu Kristo wakati huohuo wanakwenda kinyume na maadili. Paulo anakumbusha kuwa chachu hufanya unga kuongezeka, na  kwa maana hiyo inahitajika chachu kwa ajili ya unga mpya. Hayo ni maneno ya mahubiri ya Baba Mtakatifu  Francisko asubuhi ya siku ya Jumatatu tarehe 10 Septemba 2018 katika Kanisa la Mtakatifu Marta Mjini Vatican.

Injili inabadili kabisa mtu: Yesu alikuwa anawahimiza mitume wake: divai mpya katika mabarasi mapya. Habari njema ya Injili, ambayo ni habari mpya ya Kristo, haibadili  roho zetu tu, kwani inabadili sisi wote kwa ujumla, ni katika  moyo,  roho na mwili, kila kitu,  yaani divai iliyotiwa chachu katika mabarasi mapya na kila kitu. Hiyo ndiyo habari njema ya Injili kamili ambayo inawahusu wote kwa sababu inatubadili ndani na nje, kwa  maana ya kiroho, kimwili na maisha yetu ya kila siku.

Habari njema ya Injili na mapya ya dunia: Papa Francisko amejaribu kutazama wakristo wa Korinto walivyokuwa wanaishai na ambao hawakutambua habari mpya ya Injili ambayo siyo itikadi au namna ya kuishi kijamii, kama walivyokuwa wakiishi ukawaida wa kipagani. Habari ya Injili ni Ufufuko wa Kristo, ni Roho ambayo alitutumia ili kutusindikiza katika maisha. Wakristo ni wanaume na wanawake wa habari mpya na siyo wa siyowakristo wa mapya. Kuna watu wengi wanatafuta kuishi ukristo wao kwa mapya ya habari: Leo hii unaweza kufanya hivi… hapana leo hii unaweza kuishi hivi… Watu hawa wanaoishi mapya ambayo yanapendekezwa na dunia  ni malimwengu, kwa maana  hawakubali kuishi habari mpya. Kuna  utofauti kati ya kukabiliana na habari mpya ya Yesu Kristo na mapya ambayo dunia inapendekeza kuishi.

Kuwa wadhaifu  ndiyo lakini siyo wanafiki: Watu ambao Paulo anawahukumu, ni watu ambao wana uvuguvugu, ni watu waovu (…) ni watu ambao wadanganyifu, ni watu kijujuu, ni watu wanafiki anaongeza Baba Mtakatifu kwa maana hiyo  Wito wa Yesu ni  wito wa kujikita katika habari mpya. Mtu mwingine anaweza kusema: lakini padre, sisi ni wadhaifu, na sisi ni wadhambi…” aha… hili ni jambo jingine Papa anathibirisha kwani anaongeza kusemaa: Iwapo unakubali kuwa mdhambi na mdhaifu, Yesu anakusamehe, kwa kuwa ni sehemu ya habari mpya ya Injili ambayo unaungama kuwa Yesu Kristo alikufa kwa ajili ya kusamehe dhambi. Lakini iwapo unasema kuwa wewe ni mkristo wakati huohu unaishi mapya ya mchanganyo wa malimwengu, hapana, kwa maana huo ni unafiki. Na huo ndiyo utofauti uliopo.Yesu alikuwa amesema katika Injili: “ kuweni makini maana watafika na kuwaeleza Yesu yuko hapo na pale…. Mapya ni hayo…: hapana, kwa kuwa wokovu ni huu Yesu Kristo ni mmoja tu. Na ujumbe wake Kristo ni wazi!

Njia ya yule anayefuata Kristo ni ile ya ufiadini: Yesu hakatishi tamaa kwa yule anayetaka kumfuata: Baba Mtakatifu anauliza swali je  ni njia gani kwa yule anayetaka kuishi mapya na hataki kuishi habari njema? wakati huohuo Baba Mtakatifu anakumbuka jinsi gani Injili ya Siku imehitimisha kwa kuona jinsi gani wandishi na walimu wa sheria walivyo “chukua uamuzi wa kutaka kumua na kumuondoa”. Kwa maana hiyo anabainisha Papa na kusema, njia ya wale ambao wanaamua kufuata habari mpya ya Yesu Kristo ni njia sawaswa na ya Yesu. Ni njia ya kuelekea kifodini. Kifodini wakati mwingine siyo kile cha kuona ukatili, bali kile cha kila siku. Sisi tuko njiani na tunatazamwa na wafitini wakubwa ambao leo hii wanatoa mashtaka  na kututafuta hitilafu. Lakini inabidi kutofanya mazungumzo na mchakato wa mapya hayo, pia ahitajiki kuchakachua habari njema ya  Injili.

 

10 September 2018, 14:01
Soma yote >