Cerca

Vatican News
Baba Mtakatifu akazia utu na heshima ya wanawake katika ulimwengu mamboleo! Baba Mtakatifu akazia utu na heshima ya wanawake katika ulimwengu mamboleo!  (Vatican Media)

Tuwaombee wanawake wanaodhalilishwa utu na heshima yao!

Tuwaombee wanawake wanao baguliwa, wanaotumiwa kama soko na tuwaombee wasichana ambao wanalazimika kuuza hadhi yao ili wapate nafasi ya kazi.Ndiyo kiini cha tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri yake tarehe 15 Juni 2018 kwenye Kanisa la Mtakatifu Martha mjini Vatican.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tuwaombee wanawake wanao baguliwa, wanaotumiwa, na tuwaombee wasichana ambao wanalazimika kuuza hadhi yao ili wapate nafasi ya kazi. Ndiyo kiini cha tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri yake tarehe 15 Juni 2018 kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican. Baba Mtakatifu amejikita kutafakari Injili ya Siku ya Mtakatifu Matayo Mt. 5:27-32, katika maneno ya Kristo asemaye: “Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake”na Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa,azini.

Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anasema maonyo makali ya Yesu yanajikita kutazama kwa karibu yale manyanyaso ya wanawake leo hii, kwani wanawake wanatumiwa kama bidhaa, na ni jinsi gani unakosena ule utambuzi kwa binadamu ya kwamba, mtu ni sura na mfano wa Mungu. Yesu alitumia lugha hii kali ili aweze kuweka mbele ya wafuasi lengo moja katika maisha yaani jambo ambalo ni maisha safi ya sadaka, na maneno hayo yanabadili historia, kwani hadi wakati ule, mwanamke alikuwa abaonekana wa daraja la pili au kwa jina rahisi alikuwa kama mtumwa , hakuwa na uhuru kamili anasisitiza Baba Mtakatifu!

Mafundisho ya Yesu juu ya wanawake yanabadili historia yake manaa sasa, unaweza kuona mwanamke kabla ya Yesu na mwanamke baada ya Yesu. Maana Yesu anampa hadhi mwanamke na kumweka katika ngazi sawa na mwanaume kwa sababu anatumia neno la kwanza la Uumbaji, wote wawili walikuwa sura na mfano wa Mungu, ni wote wawili hapakuwapo nafasi ya kwanza kwa mwanaume na baadaye kidogo mwanamke! Hapana, wote wawili pamoja! Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu amesisitiza mwanaume bila mwanamke karibu, awe kama mama, kama dada, mwali, mwenza katika kazi, kama rafiki, mwanaume peke yake siyo sura kamilifu ya Mungu.

Akiendelea na tafakari amesema: leo hii wanawake wanatumiwa kama kitu cha tamaa, akitoa mfano, amesisitiza kwa namna ya pekee, tamaa ya mwanamke ilivyo somwa katika Injili ya siku, kwa mfano amesema, katika programu za televisheni, magazeti, habari, wanaonesha wanawake kama kitu cha tamaa na cha kutumia au kama vile soko. Katika matangazo ya kibiashara, kwenye televisheni tendo la kuuza nyanya, ndilo mwanamke anageuka kuwa kitu, kunyenyekeshwa, hajavaa nguo, vilevile Baba Mtakatifu ametoa mifano ya karibu na kusema: bila kwenda mbali hata inajitokeza katika maofisi ya karibu, hata katika makampuni mengi, wanawake wanakuwa kama kitu kiitwacho falsafa ya kutumia na kutupwa, utafikiri ni bidhaa za kuchagua na siyo watu!

Hiyo ni dhambi dhidi ya kazi ya Uumbaji, Baba Mtakatifu anasisitiza, kwa upande wa wanaume, hawawezi kuwa sura na mfano wa Mungu iwapo wanatamtupa mwanamke. Na kwa sasa kuna tatizo kubwa dhidi ya wanawake na jambo hili ni baya sana amesisitiza kwa uchungu! Lakini hata bila kusema je ni wasichana wangapi ambao, ili waweze kupata nafasi ya kazi wanalazimika kujiuza kama bidhaa ya kutumiwa na kutupwa? Mara ngapi? Ndiyo, si katika kusikia taarifa kutoka nchi fulani hata hapa Roma bila kwenda mbali ameongeza!

Baba Mtakatifu Francisko ameendelea kusisitiza juu ya kujitazama kwa karibu ili kuona manyanyaso akitoa mfano mmoja kwamba, ni jambo gani litaonekana iwapo utafanya hija ya kutembea usiku katika baadhi ya miji, mahali ambapo wanawake wengi, wawe wahamiaji na wasio wahamiaji wananyanyaswa kama soko. Wanawake hawa, wanasogelewa na wanawaume wakiambiwa habari za jioni…, je ni kiasi gani? Wakati huo huo anayetaka kuosha dhamiri anawaita makahaba.

Lakini hata wewe unayewasogelea umefanya ukahaba huo huo, kwani Yesu amesema: Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini. Na istoshe mwanamke anaishia kunyanyaswa na kuwa mtumwa mara nyingi. Ni vema kutazama wanawake hao na kufikiria kwamba mbele ya uhuru wetu wao ni watumwa wa mawazo hayo ya ubaguzi. Hayo yote pia yanatokea mjini Roma kama ilivyo kwa kila aina ya mji kuona wanawake wasio kuwa na jina au kusema wanawake wasio kuwa na mtazamo, kwasababu ya aibu, wanajifunika nyuso zao, ni wanawake wasio kuwa na tabasamu, kwa maana wengi wao hawajui furaha ya kunyonyesha, hata kuhisi umama. Lakini vile vile hata maisha yao ya kila siku kwenda katika sehemu zile za kusubiri wateja ni hisia mbaya sana Baba Mtakatifu anasisitiza yaani kumtupa mwanake kama kitu na kuonekana kama daraja la pili.

Halikadhalika amesema ni lazima kutafakari vema. Kwa maana, kusema hilo au mawazo mengine , ni kudharau sura ya Mungu ambaye ameumbwa mwanamke na mwanaume pamoja kwa mfano na sura yake. Sehemu ya Injili hiyo itusaidie kutafakari juu ya soko la wanawake, hasa inayojikita katika manyanyaso yanayo onekana, hata masoko ambayo hayaonekani, kwa maana yanafanyika lakini hayaonekani. Mwanamke anazidi kukanyagwa kwa maana ni mwanamke. Lakini Yesu anarudisha hadhi ya mwanamke kwa maana alikuwa na mama, alikuwa na marafiki wengi walio kuwa wanamfuata ili kumsaidia katika huduma yake. Yeye alikutana na wanawake wengi waliokuwa wamedharauliwa, wamewekwa pembezoni na kutupwa, aliwasaidia kwa upendo mkuu na kuwarudishia hadhi yao.

 

15 June 2018, 07:15
Soma yote >