Kardinali Zuppi akutana na vijana wa Ukraine waliokaribishwa kiangazi
Vatican News
Kardinali Matteo Zuppi Rais wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI) na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Bologna, alikutana na baadhi ya watoto wa Ukraine waliokaribishwa kwa likizo ya kiangaza kwa mshikamano huko Jimbo la Chieti-Vasto. Hawa ni baadhi ya watoto 670 waliofika kutoka katika mazingira yaliyoathiriwa na migogoro na ambao wamekaa au wanakaa kwa muda nchini Italia, kando ya bahari au milimani, kama sehemu ya mpango wa It's more beautiful together, yaani ni vizuri zaidi kuwa pamoja, unaoratibiwa na Caritas Italia, pamoja na Ofisi ya kitaifa ya huduma ya kichungaji ya familia ya Baraza la Maaskofu wa Italia, kwa ushirikiano na Caritas Spes, Caritas Ukraine, Sekretarieti ya Kanisa Katoliki la Ugiriki nchini Ukraine, Ubalozi wa Ukraine, Balozi za Ukraine nchini Italia na Vatican. Kwa njia hiyo Kardinali Matteo Maria Zuppi alikutana nao tarehe 9 Agosti 2024 katika Parokia ya Mtakatifu Martino Askofu Chieti Scalo.
Likizo za mshikamano
Mwaka huu pia, kiukweli, katika mikoa mbalimbali na kwa idadi kubwa zaidi kuliko matoleo ya awali, uzoefu wa mapokezi unarudiwa ambayo mwaka 2022 na 2023 iliruhusu watu 218 na 542 kuishi siku chache mbali na hofu na giza la vita. Mwaka 2024 majimbo yaliyohusika ni yale ya Aversa, Como, Cosenza-Bisignano, Iglesias, Jesi, Lamezia Terme, Senigallia, Teggiano-Policastro, Ugento-Santa Maria di Leuca ambayo, pamoja na ACLI ya Lombardia, wamejitolea kuandaa likizo ya mshikamano, na wakati wa burudani katika hewa ya wazi, furaha, michezo, ugunduzi wa uzuri wa eneo hilo. Yote kwa jina la kawaida, ambayo inakosa sana wale ambao, kwa zaidi ya miaka miwili, wamelazimika kukimbilia kwenye bunkers chini ya ardhi na kuishi kwa hofu ya milipuko ya mabomu.
Wakati ujao wa amani
Madhumuni ya mpango huo ni kusaidia watoto na vijana kushughulikia kiwewe cha vita, katika sehemu salama ambapo wanaweza kujadili na kukua huku wakifikiria mustakabali wa amani. “Kupitia shughuli za burudani, tunajaribu kuwapa fursa za kuzaliwa upya, kujumuika na kujenga mahusiano chanya na makini. Kwa upande mwingine, kwa jumuiya za Kiitalia, hii ni fursa muhimu kwa ukuaji na kushiriki.” Na Mkutano wa Kardinali Zuppi na watoto wa Kiukrainena familia zinazowapokea, alisema Padre Marco Pagniello, Mkurugenzi wa Caritas Italia, ambayo inahamasisha mkutano huo na alithibitisha kujitolea kwa jumuiya ya kikanisa katika kusaidia wale wanaopitia wakati wa matatizo na alitoa mwaliko wa kujenga amani na kupanda mbegu za matumaini kupitia chaguo madhubuti, kila hisia inaitwa kufanya sehemu yake.”