Tafuta

Watu wanazidi kusali kwa ajili ya nchi ya Haiti ambayo inazidi kwa ghasia na vurugu. Watu wanazidi kusali kwa ajili ya nchi ya Haiti ambayo inazidi kwa ghasia na vurugu.  (ANSA)

Haiti:Watawa Wacamilliani wamezuiwa kutoka hospitalini na watu wanakimbia

Idadi ya watu wakikimbizi,huduma ya afya ikiporomoka,watawa wa Camillian waliozuiliwa ndani ya hospitali ya mji mkuu wa Port au Prince nchini Haiti.Ndiyo maelezo ya Mmisionari ameelezea akizungumza na Shirika la habari za Kimisionari Fides.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kutokana na kile kinachoendelea katika Kisiwa kikubwa cha Hati, Padre Erwan, mmisionari wa Camillian wenye kutoa huduma kwa Wagonjwa aliandika barua akiwa huko  Port au Prince ambako janga linaendelea kuwazuia watu, vurugu ghasia na utekaji nyara. Katika barua hiyo aliyoituma kwa Shirika la Habari za Kimisionari FIDES anabainisha kuwa “Magenge yanakuwa na silaha zaidi na wakatili zaidi kila siku, tumezuiliwa ndani ya hospitali, kwa matumaini kwamba hawatatushambulia. Hatuwezi kwenda kununua chakula au dawa kwa watu tunaowakaribisha, watoto wenye ulemavu, wagonjwa, jamaa za wagonjwa waliolazwa hospitalini na wafanyakazi wa matibabu na wauguzi.

Katika maelezo hayo alisema “Walituruhusu, baada ya 'malipo ya pesa za ulinzi', kwenda nje na gari la wagonjwa mara moja tu kununua mitungi 30 ya oksijeni kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini na kwa ajili ya shughuli za upasuaji. Hali ni hatari zaidi kila siku!” alisisitiza Mcamillian ambaye na ambaye yupo pamoja na ndugu yake Padre Robert, ambaye ni mkurugenzi wa Foyer ambayo ipo huko La Plaine, katika manispaa ya Croix de Bouquet, kutoka kaskazini mwa mji mkuu Port au Prince.

“Ninafikiri  juu ya maafa ambayo watu wa Haiti wanapitia na ambayo kila siku yanaanguka ndani ya dimbwi la kutojali duniani - alirudia kusema hata Padre Antonio Menegon, MI. Hakuna mtu anayeizungumzia, mbaya zaidi, hakuna anayeingilia kati na hata kwa kidogo tunachoweza kufanya tunajaribu kuwepo ili kuwasaidia  wengi wa Haiti kuishi licha ya ukimya unaowazunguka. Kuokoa maisha ya watu wa Haiti kunamaanisha kuendeleza ufufuko wa Yesu katika maisha ya kila siku” alihitimisha Padre  ambaye anawajibika kwa shirika la  Wacamillian la Madian Orizzonti.

Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu elfu 50 wamekimbia mji mkuu katika majuma ya hivi karibuni, pamoja na zaidi ya wakimbizi elfu 100 tayari waliopo kusini mwa Haiti. Ghasia za magenge yenye silaha zimesukuma takriban watu 53,000 kuondoka katika mji mkuu katika majuma matatu yaliyopita, ripoti iliyochapishwa Jumanne na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji inaonyesha. Zaidi ya nusu wanaelekea kusini mwa nchi hiyo ambayo tayari ni nyumbani kwa watu elfu 116 ambao walikuwa wamekimbia hapo awali.

05 April 2024, 15:12