Tafuta

Askofu Mkuu Peter Chung Soon-Taick Askofu Mkuu Peter Chung Soon-Taick 

Askofu wa Seuol:katika Pasaka maisha yetu yanasukana na Milele!

Katika fursa ya Siku kuu ya Ufufuko wa Bwana Askofu Mkuu Peter Chung Soon-taick OCD, wa Jimbo Kuu la Seoul na Msimamizi wa Kitume wa Pyongyang nchini Korea Kusini alitoa ujumbe wake kuwa:“Imani katika ufufuko wa Yesu inatoa mwanga wa matumaini kwamba hata mgawanyiko uliojikita katika peninsula ya Korea unaweza hatimaye kutatuliwa katika siku zijazo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika fursa ya Siku kuu ya Ufufuko wa Bwana,  Askofu Mkuu Peter Chung Soon-taick, OCD, wa Jimbo Kuu la Seoul na Msimamizi wa Kitume wa Pyongyang nchini Korea Kusini alitoa ujumbe wake kwamba: “Imani katika ufufuko wa Yesu inatoa mwanga wa matumaini kwamba hata mgawanyiko uliojikita katika peninsula ya Korea unaweza hatimaye kutatuliwa katika siku zijazo za kuwepo kwa umoja na inaweza kubadilika kuzaliwa upya kwa kuishi pamoja kwa usawa na ustawi wa pamoja. Kwa mujibu wa Shirika la habari za kimisionari FIDES, linabainisha kuwa “Ufufuko wa Yesu Kristo ni ushuhuda wa kina kwa ukweli kwamba kuwepo kwetu duniani kunavuka mipaka ya muda ya ulimwengu huu lakini kunaunganishwa na uzima wa milele. Maana yake inapita kiwango cha maisha yetu ya kimwili na yaliyokusudiwa, lakini inaunganisha maisha yetu na uzima wa milele,” alisema hayo Askofu Mkuu Peter Chung Soon-taick OCD, wa Jimbo Kuu la Seoul na Msimamizi wa Kitume wa Pyongyang  nchini Korea Kusini katika ujumbe wake wa Pasaka 2024.

Umri unazidi kurefuka kutoka 60 hadi zaidi ya 90

Tafakari ilianza kutoka katika uchanganuzi wa kisosholojia, akikumbuka kuwa miongo michache tu iliyopita, huko Korea ilikuwa desturi kusherehekea siku ya kuzaliwa ya kufikisha miaka 60 kwa fahari kubwa, katika sherehe iliyoitwa: “Hwangap.” Pamoja na kurefushwa kwa muda wa wastani wa maisha, hata hivyo, sasa tunaelekea kuepuka hata kusherehekea siku ya kuzaliwa ya sabini, inayoitwa ‘Gohui’- ambayo ina maana “kitu cha nadra sana kutoka siku za zamani” - kwa kuwa tunaona kwamba bado tuna safari ndefu ya  maisha. Kiukweli, maisha marefu ya pamoja kwa sasa yameongezeka sana.

Imani katika ufufuko ni zaidi ya miaka elfu

Takwimu zinaonesha kuwa wastani wa maisha ya wanawake wa Korea ni karibu miaka 86, wakati kwa wanaume ni karibu miaka 81. Zaidi ya hayo, umri wa kuishi kwa afya nchini Korea ni kati ya juu zaidi kati ya nchi za OECD, na takwimu zinafikia miaka 73-74. Hii inawakilisha ongezeko la zaidi ya miaka 10-20 ikilinganishwa na vizazi vilivyotangulia.”Hata hivyo -ikiwa maisha yetu ya kidunia yataisha baada ya miaka 80-90, ina maana gani katika jamvi kubwa la historia ya miaka elfu? Inaongeza maana gani katika historia ya dunia hii na ya ulimwengu? ikiwa maisha yetu ya mtu binafsi yatabaki kutengwa na umilele?". Na aliongeza kusema: “Imani katika ufufuko wa Yesu si kama kasumba inayotusaidia kuepuka ulimwengu huu wenye matatizo, kama Karl Marx alivyosema, lakini badala yake inadokeza utambuzi wa kina kwamba maisha yetu katika ulimwengu huu wa muda yamefungamana na Milele”.

Mazungumzo ya kweli yanaweza kuvuka migogoro

Uhakika huu, unahusisha dhamira ya dhati ya kukumbatia maisha kwa ukamilifu wake, hata katikati ya majaribu ya dhiki, kama vile kushindwa, magonjwa, utengano, mmomonyoko wa upendo. Ufufuko wa Yesu unatupatia tumaini kwamba 'vifo' hivi si mahali pa mwisho bali ni mwanzo mpya, uliojaa nguvu za kimungu.Alifafanua Askofu Mkuu . Aidha Askofu Mkuu pia akizungumzuia  hali ya Peninsula ya Korea alisisitiza kuwa: “Imani katika ufufuko wa Yesu inatoa mwanga wa matumaini kwamba hata mgawanyiko uliojikita katika peninsula ya Korea unaweza hatimaye kutatuliwa katika siku zijazo za kuwepo kwa umoja na inaweza kubadilika kuzaliwa upya kwa kuishi pamoja kwa usawa na ustawi wa pamoja. Nguvu ya mabadiliko na tumaini lililomo katika ufufuko, linawafunika wale wote wanaopambana na shida, haswa ndugu zetu wa Kaskazini.” Hivyo basi, njia ya kusonga mbele ni ile ya mazungumzo: “Mazungumzo ya kweli yana uwezo wa kuvuka migogoro na migawanyiko, kukuza uelewa na maelewano kwa wengine. Viongozi wa kisiasa wana wajibu mkubwa wa kuongoza mwelekeo wa mataifa yao kuelekea maendeleo na ustawi wa pamoja na  kuwa miongoni mwa watu wao.”

Uchaguzi wa viongozi wanaojali usawa na demokrasia

Kwa maana hii, akirejea hali ya ndani ya Korea Kusini, ambayo inaelekea kwenye uchaguzi wa wabunge mnamo Aprili 10 alisema: “Wanasiasa katika nchi yetu wanapaswa kutoa kipaumbele kwa ustawi wa watu badala ya ajenda za vyama.  Kwa hiyo inakuwa muhimu kwa sisi, wananchi wa jamii ya kidemokrasia, kutumia utambuzi wa busara katika mchakato ujao wa uchaguzi, kuchagua viongozi ambao wamejitolea kwa usawa kutumikia maslahi ya watu. Katikati ya changamoto za kibinafsi na kijamii, ufufuko wa Yesu Kristo unatumika kama mwanga wa tumaini, ukiimarisha imani yetu katika uwezekano wa ukombozi na kufanywa upya.”

02 April 2024, 17:27