Tafuta

Jumuiya Wakatoliki wa Congo mjini Roma waliudhuria Sala ya Malaika wa Bwana 10 Machi 2024. Jumuiya Wakatoliki wa Congo mjini Roma waliudhuria Sala ya Malaika wa Bwana 10 Machi 2024.  (Vatican Media)

Rwanda:Hapana makubaliano ya madini endelevu kati ya EU na Rwanda!

“Mtandao wa Amani wa Congo” na mitandao mingine 7 kwa jina: “Pamoja kwa ajili ya Amani ya Congo”wanakataa mkataba uliotiwa saini tarehe 19 Februari 2024 kati ya Umoja wa Ulaya na Rwanda kuhusu uendelevu na ufuatiliaji wa madini ya kimkakati na nchi ambayo haizalishi madini lakini inayapata kinyume cha sheria kutoka nchi jirani.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Inawezekanaje Umoja wa Ulaya (EU)kutia saini mkataba juu ya uendelevu na ufuatiliaji wa madini ya kimkakati na nchi ambayo haizalishi madini lakini inayapata kinyume cha sheria kutoka nchi jirani? Hivi ndivyo swali linaulizwa na “Mtandao wa Amani wa  Congo” na mitandao mingine 7 linalojulikana kwa: “Pamoja kwa ajili ya Amani ya Congo”(unaohamasishwa na wamisionari wanaofanya kazi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC), katika taarifa yao iliyotumwa kwa Shirika la Habari za Kimisionari Fides na  ambao wanaomba kufuta itifaki ya makubaliano iliyotiwa saini tarehe 19 Februari 2024  kati ya Umoja wa Ulaya (EU) na Rwanda. Hata hivyo Mkataba huo ulikuwa tayari umekosolewa na Kardinali Fridolin Ambongo Besungu, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la  Kinshasa.

Inawezekanaje nchi isiyo na madini kuuza kiasi kikubwa?

Kulingana na Umoja wa Ulaya (EU), Rwanda “ni mdau mkuu wa kimataifa katika sekta ya madini ya tantalum. Pia inazalisha bati, tungsten, dhahabu na niobium na ina akiba ya lithiamu na udongo adimu.” Katika taarifa iliyotumwa kwenye Shirika la habari Fides inataka kueleza nia thabiti ya kuheshimu uhalali, kulingana na viwango vya ufuatiliaji ambavyo Ulaya yenyewe imeanzisha mnamo 2021. Kwa njia hiyo inasema: “Ni aibu, hata hivyo  kwamba Umoja wa Ulaya (EU) unawekeza kwa maana hii katika nchi ambayo haina kiasi kikubwa cha madini haya, nchi ambayo imekuwa muuzaji mkubwa wa nje kutokana na vita ambayo ilianzisha mara kwa mara katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuanzia mwaka 1996, kila mara kupitia harakati lililoingiliana, ambalo katika miaka ya hivi karibuni limechukua jina la M23.”

Gharama za vita, wizi wa mali za watu masikini kisa ni kushi eneo la kunyonywa

“Kutoka mashariki mwa Congo, kwa msaada wa viongozi wafisadi katika ngazi mbalimbali, kwa miaka mingi madini ya thamani ya dhahabu, coltan, udongo adimu yamekuwa yakitiririka kuelekea Rwanda na nchi nyingine jirani za mashariki... Ugumu kwenye mipaka, hila za aina mbalimbali lakini sasa zinapita kwa uwazi, kutokana na maeneo ambayo M23-Rwanda inamiliki kuvuka mpaka. Hii inakuja kwa gharama ya vifo, vurugu za kila aina, za wizi wa mali za watu ambao kosa lao pekee ni kuishi katika eneo linalotamaniwa na zaidi ya watu milioni moja waliohamishwa - katika Mashariki pekee - ambao wanaishi vibaya na kufa katika kwenye maandaki ya muda katikati ya msimu wa mvua.” Hati hiyo  imesisitiza.

Ulaya ifute makubaliano hayo ili kuchangia ujio wa amani

Kwa njia hiyo “Ikiwa lengo la makubaliano ya tarehe 19 Februari 2024 kama ilivyotangazwa na Bunge la Ulaya katika kukabiliana na ukosoaji mwingi uliojitokeza, ni kuongeza ufuatiliaji na uwazi na kuimarisha mapambano dhidi ya usafirishaji haramu wa madini, labda haikuwa sahihi zaidi kuiwekea vikwazo Rwanda badala ya kuweka makubaliano nayo kuhusu matunda ya wizi unaoendelea? Ni swali  “Pamoja kwa Amani nchini Congo. “Tukirejea sauti nyingi ambazo zimetolewa dhidi ya makubaliano hayo, na mamlaka, na raia wa Congo, na nchi za Ulaya kama vile Ubelgiji na MEP, sisi pia kama Kamati ya “Pamoja kwa  ajili ya Amani ya Congo” tunatoa ombi kali kwa Umoja wa Ulaya kufuta mkataba huu, ili kuchangia katika ujio wa amani katika eneo hilo. Tunaamini kuwa ni mtazamo wa haki tu na usio na upendeleo unaoweza kukuza kuishi pamoja kwa amani katika eneo la Maziwa Makuu ya Afrika.”

 

11 March 2024, 15:26