Tafuta

Kardinali Pizzaballa, Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu Kardinali Pizzaballa, Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu  (ANSA)

Kard.Pizzaballa:Sitisheni silaha za moto haraka Nchi Takatifu!

Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu ametoa wito kwa ajili ya amani katika Ukanda wa Gaza uliozidiwa na janga la vita:“Watu hawana chochote kilichobaki:kuna ukosefu wa chakula,maji,madawa.Makubaliano yanawezekana bali yanahitaji utashi tu.Kanisa mahalia lilijitolea kusali na kusaidia watu wote.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kardinali Pierbattista Pizzaballa Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo vya habari Vatican ametoa wito wa kusitisha mapingano huko Gaza ambao unazidi kuwa wa dharura. Kwa njia hiyo ametoa wito tena kwa kilio chake kipya cha uchungu ambacho kinasimulia juu ya Ukanda uliosambaratishwa na vifo na machafuko makali. “Mbali na vurugu za kutisha za mabomu pia kuna shida ya maisha ya kawaida. Kuna ukosefu wa chakula, dawa na maji. Kwa mfano, Wakristo wetu wanaweza kupika mara moja au mbili na kile wanachopika lazima kiwe cha kutosha kwa angalau juma zima.”

Picha za kutisha kwa waliopoteza maisha

Picha za kutisha za wanaume, wanawake na watoto hao ambao siku chache zilizopita walipoteza maisha katika jaribio la kunyakua mabaki ya misaada ya kibinadamu bado ziko wazi machoni pa kadinali huyo. "Nilichanganyikiwa pia kusikitishwa na machafuko ambayo Ukanda mzima umeangukia: hakuna aina ya udhibiti wa eneo hilo na kutatiza kila kitu pia kuna kuwasili kila wakati zaidi na tatizo kuliko misaada ya kibinadamu.” Kardinali Pizzaballa haoni kufaa kwamba vifurushi vya chakula na mahitaji ya kimsingi sasa viangushwe katika makundi yenye miamvuli: "Tunahitaji suluhisho la utaratibu na uratibu zaidi, kwa sababu uchaguzi wa aina hii unahatarisha kuongezeka kwa machafuko. Na labda pia umati na wafu.”

Ufumbuzi thabiti

Imani ya Kardinali Patriaki wa Yerusalemu iliyoshirikishwa na Mapatriaki wakuu wote wa Makanisa ya Jiji Takatifu, ambapo mnamo tarehe 1 Machi 2024 walitia saini ombi lingine la amani ni kwamba makubaliano ya amani huko Gaza sio ya kufikirika na ndoto isiyoweza kufikiwa. “Unahitaji tu kuitaka na vipengele vya kutekeleza vipo. Kwa pande zote mbili, nia ya kufikia maelewano ni muhimu. Ninaamini kuwa wakati umefika wa kujaribu kuanza njia tofauti.” Hata hivyo, hata kama hali nyingi za kutokuwa na uhakika zingesalia, kwa Kardinali jambo moja haliwezi kutiliwa shaka: “Baada ya mgogoro huu, mojawapo ya matatizo makubwa zaidi ya miaka 70 iliyopita, si Waisraeli wala Wapalestina watakuwa tayari zaidi kupata masuluhisho ya muda. Matukio haya yatalazimisha kila mtu kutafuta suluhisho thabiti. Watu wawili, majimbo mawili? "Sijui. Kitaalam inaonekana kuwa ngumu kwangu hata kama itakuwa njia pekee inayowezekana. Ni wazi kwamba chochote tunachochagua kufanya kitalazimika kuhakikisha utulivu na uhuru kwa watu wote wawili." Kutoka historia ya Patriaki wa Yerusalemu linaibuka jukumu la Kanisa mahalia ambalo  amesema  lina uaminifu,  na  sio tu kushughulikia mahitaji yake bali pia linaweza kusaidia watu wa jirani. Na wanaelewa jinsi, ambavyo kwa usiri, wanajaribu kuwapo katika njia za mawasiliano na jukumu la mwezeshaji kati ya wahusika wote wanaohusika.

06 March 2024, 11:05