Tafuta

Jitihada za Wasalesiani katika elimu kwa watoto maskini. Jitihada za Wasalesiani katika elimu kwa watoto maskini. 

Ghana:Kulinda Utoto wa watoto waliodhaifu ni utume wa Walesiani wa Sunyani

Kuna hitaji la kuwasaidia watoto wa mitaani ili waweze kuondokana na utelekezwaji wao.Ili kufanya hivyo inaitaji kujitolea kama wafanyavyo Shirika la Wasalesiani la Mtakatifu Don Bosco nchini Ghana na kulinda utoto wa watoto walio wadhaifu.Lakini pia utume huo wa watoto mitaani upo nchini Uganda na Ethiopia.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Hali ya watoto wa mitaani katika mazingira duni sana ya Sunyani nchini Gana yanaleta dharura kubwa, pigo ambalo linatishia uhai na mustakabali wa maelfu ya watoto wadogo wanaotoka katika mazingira duni, kutoka kwa familia zilizokata tamaa, kutoka kwa wazazi wasio na makazi, wasio na uwezo, wasio na ajira au wagonjwa. Ili kusaidia kundi hili lililo hatarini, Wamisionari Wasalesian wa Don Bosco walizindua programu ya “Wewe ni mkate wa kila siku” inayolenga watoto wengi maskini, peke yao au waliotelekezwa. Huu ni mpango wa kimsingi wa kulinda utoto wa watoto dhaifu waliokaribishwa na Shirika la  Don Bosco katika utume wa kuwasindikiza katika miaka muhimu zaidi ya maisha yao, na kuwafanya wajisikie salama kila siku , walieleza  wamisionari hao. Kwa sasa kuna watoto 75 na vijana wenye umri kati ya miaka 5 na 24, wote wanatoka mijini na vituo vikubwa karibu na Sunyani.”

Ziara ya Mkuu wa Ofisi ya Mipango ya Wasalesiani

Kwa mujibu wa mkuu wa Ofisi ya Mipango, Marcella Mantovani, ambaye hivi karibuni alitembelea kituo cha Salesian alisema kuwa Akwaaba', ambayo kwa lugha ya kienyeji linamaanisha 'karibu', ndilo neno lililoambatana na ziara yake katika Nyumba ya Wavulana ya Bosco huko Sunyani. “Mara moja nilijikuta nimezungukwa na furaha na mapenzi ya watoto hawa wote na vijana wa rika zote. Kila mtu yuko tayari kushindana ili kuonesha ukarimu, kila mtu yuko tayari kutoa tabasamu, kupeana mkono, kukumbatiana, yote hayo chini ya macho ya upendo ya Padre Charles, mkurugenzi wa kituo hicho.”

Utume wa watoto hata Uganda na Ethiopia

Nyumba ya Wasalesiani inawatunza watoto na vijana waliolazimishwa, tangu umri mdogo, kuishi na kukua mitaani, waathiriwa wa kila aina ya unyanyasaji na unyanyasaji, kunyonywa katika biashara ndogo ndogo, uchuuzi mitaani, ukahaba na biashara ya madawa ya kulevya na wizi wa silaha. Lengo la Wamisionari ni kuwakomboa, kuwafanya wajisikie wamekaribishwa na kupendwa, kuwapa fursa ya kupata elimu ambayo umaskini unawanyima. Mpango huo pia unatumika katika nyumba za wamisionari Wasalesian huko Mekanissa, Ethiopia, na Namugongo, Uganda.

05 March 2024, 09:33