Tafuta

Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Arabia huko Baharain. Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Arabia huko Baharain. 

Baharain:mwanga na tumaini katika hija takatifu ya kupitia Mlango Mtakatifu

Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Arabia (OLA) huko Bahrain ni mwanga wa mwanga wa kiroho na matumaini kwa Wakatoliki.Na sio mahali pa ibada tu bali pia ni ishara ya amani na umoja. Tangu 24 Oktoba 2023 Kanisa Katoliki katika Peninsula lilianza maadhimisho ya sikukuu ya kiliturujia ya kuuawa kwa Mtakatifu Areta na wenzake kwa ufunguzi wa Jubilei katika parokia zote itakayomalizika 23 Oktoba 2024.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kupitia barua iliyoshirikishwa kwenye Shirika la Habari za Kimisionari la Fides, Vicariate ya Kitume ya Kaskazini mwa Arabia inatoa mrejesho wa hija hadi kwenye Mlango Mtakatifu wa Kanisa Kuu la Awali, mojawapo utamaduni mtakatifu na unaoheshimika zaidi wa Kanisa Kuu, ambalo ni Kanisa kuu la Kikatoliki katika Peninsula ya Arabia. Ni mlango wa kiishara uliofunguliwa katika maadhimisho ya mwaka wa Jubilei ya Mtakatifu Areta na  Wenzake, mashahidi.

Mwaka wa jubileio utafungwa 23 Oktoba 2024

Tarehe 24 Oktoba 2023 Kanisa Katoliki katika Peninsula lilianza maadhimisho ya sikukuu ya kiliturujia ya kuuawa kwa Mtakatifu Areta na wenzake kwa ufunguzi wa Jubilei katika parokia zote itakayomalizika mnamo tarehe 23 Oktoba 2024. Kitendo cha kuvuka Mlango Mtakatifu kinaonekana kama njia ya kufikiria kutoka katika dhambi hadi neema, kutoka gizani hadi nuru. Mahujaji kutoka sehemu zote za dunia hufika kuvuka Mlango Mtakatifu wakiomba msamaha  ambapo inatumika pia kuombea roho za waamini walio Toharani.

Hija ya kiroho inaimarisha vifungu vya udugu

Ni uzoefu wa kipekee na wenye nguvu kwa wote wanaoufanya. Safari ya kiroho na kimwili inayowahitaji washiriki kutafakari maisha yao, kutafuta msamaha wa dhambi zao na kufanya upya imani yao kwa Mungu. Hija ya kiroho inaimarisha vifungo vya udugu, kumkumbusha kila mmoja juu ya utume wa pamoja wa kumpenda na kumtumikia Mungu katika uzoefu wa upya na mabadiliko ya kiroho. Ni wakati wa neema na baraka, ni wakati wa kufungua mioyo na akili ya mtu kwa nguvu ya kubadilisha ya neema ya Mungu na kuvuka Mlango Mtakatifu kuelekea wakati mpya na angavu zaidi. Mahujaji wanapovuka Mlango Mtakatifu wanaoneshwa vifungu vinane ambavyo ni pamoja na Picha ya Mtakatifu Aretas, Kanisa la Mama Yetu wa Arabia, Bwawa la Ubatizo, Altare kuu, Taji la Fumbo (picha 16), Kiti cha Askofu, Kikanisa cha Upatanisho na Kikanisa cha Sakramenti Takatifu.

05 March 2024, 09:51