Tafuta

2024.02.29 Mkutano wa mwaka wa Baraza la maakofu nchini Angola na  São Tomé (CEAST). 2024.02.29 Mkutano wa mwaka wa Baraza la maakofu nchini Angola na São Tomé (CEAST). 

Angola:Maaskofu wa CEAST wanaonya juu kashfa ya umaskini

Maaskofu wa Baraza la Maaskofu la Angola na Sao Tomé(CEAST)wameelezea wasiwasi wao kuhusiana na kuongezeka kwa umaskini.Katika hotuba yake Rais wa Baraza hilo alisema kuwa“Wakati wetu wa sasa unadai upyaisho wetu wa ndani kutoka kwa kila mmoja.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baraza la Maaskofu la Angola, São Tomé na Príncipe CEAST walikutana katika Jimbo kuu la Malanje, takriban kilomita 400 mashariki mwa mji mkuu Luanda wa Angola. Askofu Mkuu José Manuel Imbamba, Rais wa baraza la Maaskofu hao, mwanzoni mwa mkutano wa mawasilisho kwa niaba ya  Maaskofu 21 alitoa hotuba yake ya ufunguzi. Katika hotuba yake, Askofu Mkuu wa Saurimo aliakisi baadhi ya hatua muhimu ambazo zimeashiria maisha ya Kanisa katika eneo hilo. Pia alitoa matamshi kuhusu mwaka wa mwisho wa tatu uliowekwa kwa  ajili ya watoto ambao majimbo ya Baraza la Maaskofu hao (CEAST) yamekuwa yakizingatia.

Misa ya Maaskofu wa Angola (CEAST)26 Februari 2024
Misa ya Maaskofu wa Angola (CEAST)26 Februari 2024

Askofu mkuu Imbamba alisema kuwa kumekuwepo na jitihada kubwa za kuwahamasisha mapadre, watawa wa kike na kiume na mawakala wengine wa kichungaji juu ya umuhimu na uharaka wa kuwatunza na kuwalinda watoto wadogo pamoja na kuhimiza utamaduni wa kukemea unyanyasaji dhidi ya watoto wadogo. “Pamoja na jitihada ambazo jamii imefanya kuboresha ubora wa maisha kwa watoto, bado kuna mengi yanahitajika kufanywa.”

Hali ya kijamii na changamoto

Katika mwaka wa tatu na wa mwisho wa madaraka yake kama Rais wa CEAST, Askofu Mkuu Imbamba alipendekeza kwamba Mkutano huo utafakari wasifu wa maisha ya kipadre na kitawa. “Wakati wetu wa sasa unadai upya wa ndani kutoka kwetu sote.” Kuhusu hali ya kijamii na changamoto za CEAST, Askofu Mkuu Imbamba alisema kwamba Angola, hasa, ina hatari ya kugeuza kashfa ya umaskini na taabu kuwa hali mpya ya kawaida. Askofu Mkuu aliegemeza hoja zake juu ya ripoti zilizowasilishwa na majimbo mbalimbali yanayounda CEAST na tafiti nyingi kuhusu hali halisi ya kijamii ya Angola.  “Kila kitu kibaya tunachoishi na kukipitia kinatokana na mzozo mkubwa wa maadili”, kwa njia hiyo aliomba kwa ajili ya matumaini na siku bora. Mkutano wa Mjadala wa CEAST ulimalizika tarehe 4 Machi 2024 katika mji wa Malanje.

05 March 2024, 10:02