Tafuta

Talitha Kum iliyoanzishwa mnamo 2009 ndani ya  Umoja wa Kimataifa wa Mama Wakuu wa Mashirika ya Kitawa(UISG),inahusika kuwasaidia waathirika wa Biashara haramu ya binadamu Talitha Kum iliyoanzishwa mnamo 2009 ndani ya Umoja wa Kimataifa wa Mama Wakuu wa Mashirika ya Kitawa(UISG),inahusika kuwasaidia waathirika wa Biashara haramu ya binadamu 

Zambia,TUKUZA:Siku ya maombi na tafakari kuhusu biashara haramu ya binadamu

Katika Siku ya Kimataifa ya Maombi na Tafakari ya Kupambana na Biashara Haramu wa Binadamu,tarehe 8 Februari 2024 ambayo ipia ilikuwa ni siku kuu ya Mtakatifu Bakhita,watawa wa Mpango wa Talitha Kum-Zambia(TAKUZA) wamerudia ahadi yao kwa ajili ya waathirika.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kila tarehe 8 Februari ya kila Mwaka, Mama Kanisa anamkumbuka Mtakatifu Josephine Bakhita, sanjari na Siku ya Kimataifa ya Maombi na Tafakari ya Kupambana na Biashara Haramu wa Binadamu. Katika fursa ya siku hiyo, hata watawa wa Mpango wa Talitha Kum nchini Zambia (TAKUZA) wamejikita kutoa ahadi ya uendelevu wa utetezi wa watu hao na kuwa karibu na waathirika wote. Katika kudhimisha siku kuu hiyo ambayo Makatifu  osephine Bakhita, ni msimamizi wa wathiriwa wa Utumwa Mamboleo na bishara haramu ya binadamu, iliyoongozwa  mwaka 2024 na mada:“ Safari katika hadhi: kusikiliza, kuota na kutenda”, Watawa wa Zambia walitoa ahadi zao za kupambana na janga hili baya sana la utumwa mamboleo.

Mtandao wa TUKUZA

Kwa mujibu wa Shirika la Habari za Kimisionari Fides, limebainisha kuwa, TAKUZA ilianzishwa mnamo mwaka 2021 na watawa watatu, Sista Kayula Lesa wa Shirika la Masista wa Upendo, Sista Mutinta Simaanza wa Masista wa Roho Mtakatifu na Sista Veronica Ramotse wa Shirika la Watumishi Wadogo wa Maria Safi. Watawa hao watatu walikuwa miongoni mwa washiriki 35 wa kozi iliyofanyika mnamo mwaka 2020 iliyohamasishwa na Mtandao wa Kimataifa wa  Talitha Kum kwa ajili ya kuunda mitandao ya kitaifa na kikanda duniani kote ili kukabiliana na janga hilo la  biashara haramu ya binadamu.

Mtandao wa kimataifa wa Talitha Kum

Talitha Kum iliyoanzishwa mnamo 2009 ndani ya Umoja wa Kimataifa wa Mama Wakuu wa Mashirika ya Watawa  (UISG), unahamasisha ushirikiano kati ya mitandao iliyoandaliwa katika ngazi ya kitaifa, kikanda na bara, ili kupambana kikamilifu  na biashara haramu ya binadamu na unyonyaji, kusaidia kwa dhati  waathiriwa, waathirika na watu walio katika mazingira  hatarishi. Kwa njia hiyo chombo hiki TAKUZA kilianza kufanya kazi rasmi  mnamo Mei 2022. Kwa sasa kina wafanyakazi watatu wa kudumu nchini kote na vikundi vya uhamasishaji katika majimbo 11 ya Kikatoliki nchini Zambia. Mpango  huo kwa sasa unatekelezwa na Masista wa Shirika la Upendo.

Kitovu cha biashara haramu

Kuhusiana na mtanado huo ni kwamba Zambia inabainika kuwa  kitovu cha biashara haramu ya binadamu kusini mwa Afrika, hasa kwa upande wa wahamiaji kutoka sehemu mbali mbali kama vile  Ethiopia, Somalia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Rwanda na sehemu nyinginezo, wanaotafuta nafasi za kazi katika nchi tajiri kama vile Namibia na Afrika Kusini. Kanda hiyo ina makubaliano ya usafirishaji huru wa watu na bidhaa chini ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), ambayo inafanya iwe rahisi kwa wafanyabiashara wa binadamu kusafirisha watu kuvuka mipaka.

Vitisho vya wafanya biashara haramu

Yapo Mashirika mbambali chini ya vivuli vya kibiashara wakati wakifanya biashara haramu  ya binadamu yanayofanya kazi nchini Zambia  ambayo yanawanyonya wanawake na watoto kutoka nchi jirani ili kuwageuza kuwa vibarua vyao kwa  kulazimishwa au kuwatuma wanawake katika ukahaba. Wanawake wa Rwanda ndio hasa walengwa. Wanashawishiwa hadi Zambia kwa ahadi kwamba watapata hadhi ya ukimbizi na kupata manufaa ya kiuchumi. Hatimaye, katika kudanyanywa huko wanakuwa watumwa wa ngono na wanashikiliwa kinyume na mapenzi yao. Wasafirishaji haramu wa binadamu, wanatishia kuwakabidhi wahamiaji haramu kwa maafisa wa uhamiaji iwapo watakataa kufanya kile wanachoambiwa. Hivi ni vitisho vikubwa ambavyo Watawa wa Mpango wa Talitha Kum- TUKUZA wanajaribu kuwanasua katika mtego huo, ili kuwarudishia hadhi yao na ikibidi kuwarudisha nyumbani kwao.

Mtandao wa Talitha Kum ni kumkomboa mwathirika wa biashara haramu ya binadamu
Mtandao wa Talitha Kum ni kumkomboa mwathirika wa biashara haramu ya binadamu
09 February 2024, 14:31