Tafuta

2024.02.13 Wafranciskani OFM Nairobi Kenya katika Mkutano kuhusu Ulinzi wa Watoto. 2024.02.13 Wafranciskani OFM Nairobi Kenya katika Mkutano kuhusu Ulinzi wa Watoto. 

Wafransiskani Barani Afrika na masuala ya Ulinzi wa Watoto na walio hatarini

Kikao cha kwanza cha mafunzo kwa mapadre wafransiskani barani Afrika (OFM)kuhusu Ulinzi wa watoto na Watu wazima walio katika mazingira magumu,kilichofanyika jijini Nairobi,Kenya kuanzia tarehe 1 hadi 15 Februari 2024,kimemalizika.Ni matumaini kuendeleza umuhimu wa kusikiliza waathirika.

Olivier Bonnel na Angella Rwezaula – Vatican.

Ni kwa mara ya kwanza kwa Wafransiskani barani Afrika kukutana kuanzia  tarehe 1 hadi 15  Februari 2024 kwa viongozi 55 wa Shirika la Ndugu Wadogo  Wafranciskani (OFM) kutoka bara la Afrika ambao walikusanyika jijini Nairobi, Kenya  katika kikao cha mafunzo ya uhamasishaji juu ya ulinzi wa watoto na watu walio katika mazingira magumu. Mnamo mwaka wa 2021, Shirika la Ndugu Wadogo Wafranciskani (OFM)liliamua kuunda ndani yake ofisi ya Ulinzi  ya Ulinzi Watoto na watu walio katika mazingira magumu na wakati wa hitimisho la Mkutano Mkuu wa Shirika uliwahimiza Ndugu Wadogo Wafranciskani  kulishughulikia suala hilo.

Wakati wa kikao cha mafunzo kwa OFM Nairobi Kenya
Wakati wa kikao cha mafunzo kwa OFM Nairobi Kenya

Kwa njia hiyo shughuli hii ilileta pamoja Watawa hao kutoka majimbo yote ya Wafransiskani na Ofisi za Ulinzi wa masuala hayo kutoka barani Afrika. Katika kikao hicho Wataalamu kutoka duniani kote walizungumza ili kujadili mambo mengi ya mapambano dhidi ya unyanyasaji kuanzia na: kuwasikiliza waathiriwa, mafunzo, athari za unyanyasaji kwa wapendwa wa waathirika na zaidi ya yote kufikiria juu ya zana za kujikita nazo ili kukabiliana vyema na janga hilo baya. Miongoni mwao hao, alikuwa ni Augusta Muthigani, Mkuu wa Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto, barani Afrika.

Kurudi kwa Mtakatifu Francis

Kinachoonekana kuendeleza mbele ni kushiriki kiroho ambamo kikao kilipangwa. Wakati wa utangulizi wake wa kikao, Ndugu Mdogo Albert Schmucki, Mkuu wa Kitengo cha  Ulinzi wa Watoto  na Watu walio katika mazingira magugu cha  Shirika la Wafransiskani, alitoa tafakari ya wosia wa Mtakatifu Fransis wa Assisi, ambapo Maskini huyo anachochea uongofu wake. Historia hiyo inahusu kukutana na kusaidia wakoma, na ndiyo ilikuwa hatua yake ya kwanza ya uongofu.

Wakati wa Mkutano wa OFM huko Nirobi kenya kuhusu Ulinzi wa Watoto
Wakati wa Mkutano wa OFM huko Nirobi kenya kuhusu Ulinzi wa Watoto

Kwa mujibu wake alisema kwamba “Bila kuwatambulisha na watu wenye ukoma wa Enzi za Kati, kuna mambo yanayofanana na waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono leo hii. Wakoma walitengwa, wakatengwa na jiji na ilibidi wabaki wasioonekana.  Hapo ndipo Mtakatifu Francis alipopata uwongofu wake, na akapatana na huruma ya pande zote. Kujifunza kwa upya juu ya maisha ya Mtakatifu wa Assisi kulifanya iwezekane kujifunza mengi ili kujua jinsi ya kuunda nafasi kwa waathiriwa.” Na kwa kuongezea maoni yake Ndugu Albert hali ya sasa imebadilika baada ya kushiriki huku katika kueleza masuala haya wazi.  Waligundua jinsi ilivyokuwa muhimu kusikiliza kwa moyo.

Kusikiliza waathirika

Ushahidi wa waathriwa wawili pia ulikuwa wa maamuzi mwanzoni mwa kikao. Padre Joulain, mmisionari kutoka Afrika na mmoja wa waandaaji wa mkutano huo, ambaye amekuwa akiwasaidia manusura wa unyanyasaji wa kijinsia kwa miaka naye alisema kuwa “Ilibadilisha kabisa mwelekeo wa kikao” Na kwa upande wa Padre Blanc, hatua muhimu ni kuwasikiliza wahanga hao. “Tuliona kwamba usikilizaji huu, ukiangalia ukweli huu usoni haukusababisha woga tena, bali ukawa sehemu ya kazi ya Kanisa la wamisionari leo katika Afrika.”

Upinzani wa kiutamaduni

Majuma mawili  yaliwezesha kutambua mwelekeo wa kiutamaduni ambao unaweza kuwa kizuizi kwa mtazamo wa mgogoro wa unyanyasaji. “Katika bara la Afrika, familia bado ni kitengo chenye nguvu sana kwa jamii, ndiyo maana suala la ulinzi wa watoto wakati fulani linaonekana kuwa tishio kubwa,” alileza Ndugu Albert Schmucki. “Ndugu wenyewe walisisitiza kwamba ili tusitishie familia, bado tunapendelea utamaduni wa kunyamaza. Kipengele kingine ni kile cha uongozi wa kisiasa, kijamii au kiuchumi barani Afrika, lakini pia katika Kanisa ambako wakati mwingine kuna ukosefu wa kutafakari juu ya jinsi mamlaka yanavyotumika,” alibainisha.” Ndugu Schmucki.

Mkutano kuhusu ulinzi wa Watoto
Mkutano kuhusu ulinzi wa Watoto

Padre Stéphane Joulain, alisema: “Ni muhimu kuunganisha tamaduni tofauti za Afrika ili kuweka ulinzi wa kweli, haitoshi kutatua kesi chache za pekee. Kuna upinzani kwa sababu ni suala linaloweza kuogopesha, alisisitiza “lakini kikao hiki kilionesha kwamba tunatoka kwenye mfumo wa ubongo hadi kwenye swali hadi mtazamo wa ukweli huu unaotoka zaidi kutoka moyoni” alijipongeza.

Ndugu Pierre-Auguste Kacou,OFM wa(Ivory Coast)

Ndugu Pierre-Auguste Kacou, mwenye asili ya Ivory Coast, akiwa Nairobi, alieleza suala hilo kuwa mojawapo ya vikwazo katika mtazamo wa uhalifu wa watoto pia ni mazingira ambapo kuna vipaumbele vingine, vinavyohusishwa na masuala ya kijamii au usalama, ustawi wa idadi ya watu. Kwa hivyo suala la unyanyasaji halionekani kama tatizo la dharura.” Mfransiskani wa Ivory Coast pia aliweka sifa ya kiutamaduni ya utatuzi wa migogoro, ambayo mara nyingi inahusisha mazungumzo. "Lakini kwa kufikiria zaidi na zaidi, kwa kusoma tena Injili na kujikita katika uzoefu wa Makanisa mengine, tunatambua kwamba suala la unyanyasaji limekuwa muhimu.” Changamoto ni kubwa: pamoja na miundo ya mapokezi kwa waathirika, ni muhimu pia kuwafundisha wafanyakazi kupokea ushuhuda wao na kuanzisha mchakato wa msaada. Kwa wengi wa washiriki katika kipindi cha mafunzo, Kanisa Barani Afrika bado halina msingi thabiti wa kufanyia kazi, kama vile matokeo ya uchunguzi. Hata hivyo, Wafransisko katika bara la Afrika hawajaanza kutoka mwanzo.

Matumaini kwa Afrika

Kikao hiki kwa hivyo kilifanya iwezekane kushiriki uzoefu adilifu tayari, katika kukaribisha maneno ya wathiriwa. “Nchi fulani tayari zina uzoefu mzuri kwa kuanzia, kwa sababu miundo inaanzishwa huko” alisitiza Ndugu Pierre-Auguste. Hivi ndivyo hali ilivyo kwa mfano ndani ya Baraza la Maaskofu wa Kenya ambapo Tume ya Elimu imeunda mpango wa kusaidia waathiriwa. Huko Brazzaville, kitengo cha usikilizaji na usaidizi kiliundwa; Togo pia ilisifiwa kama nchi adilifu katika eneo hili. Kikao hiki nchini Kenya kinaruhusu mbegu kukua kwa siku zijazo. Ni matashi mema ya Wafransiskani ya kutatua matatizo yote ya Afrika", alihitimisha Padre Stéphane Joulain, na kwamba tangu wakati huo, kuwa  rasilimali yake imeundwa ili kujenga programu za ulinzi. Katika ulimwengu huu mpya, ndugu hao wote wanaweza kuwa mawakala wa mabadiliko.” Hata hivyo Washiriki hao pia walitembelewa na Askofu Mkuu Hubertus Matheus Maria van Megen, Balozi wa Vatican Nchini Kenya ili kuwakaribisha na kuwasalimia na kuwatia moyo Ndugu Wadogo Wafranciskani.

Kikao cha mafunzo kwa Ndugu wadogo wafranciskani OFM
16 February 2024, 11:40