Tafuta

2024.02.07  kikundi ccha mtanadao wa Talitha kum. 2024.02.07 kikundi ccha mtanadao wa Talitha kum. 

Kuondoa biashara haramu ya binadamu kuanzia nguvu za vijana

Katika kuadhimisha Siku ya 10 ya Kimataifa ya Sala na Tafakari dhidi Biashara haramu ya Binadamu,ambayo hufanyika kila Februari 8,Juma la uhamasishaji na maombi linafanyika Roma,linalohamasishwa na mtandao wa kimataifa wa Talitha Kum na kuhusisha wavulana na wasichana kutoka Ulimwenguni.

Vatican News

Biashara haramu wa binadamu inahusisha mamilioni ya watu duniani kote na kwa bahati mbaya ni jambo linalozidi kukua na kubadilika. Haya ndiyo yanaibuka kutokana na ripoti za hivi karibuni za Umoja wa Mataifa. Ili kukabiliana na ukweli huu mbaya, Papa Francisko amekuwa mstari wa mbele katika mapambano ya janga hili baya tangu 2015. Kwa njia hiyo ilianzisha Siku ya Kimataifa ya sala na tafakari dhidi ya biashara haramu ya binadamu katika tarehe ya kumbukumbu ya Mtakatifu Josephine Bakita, tarehe 8 Februari ya kila mwaka na limefika toelo lake la kumi. Katika maandalizi ya maadhimisho haya, Juma la uhamasishaji na maombi na tafakari ambalo limehamasishwa jijini  Roma linahusisha zaidi ya vijana hamsini,ambapo ni pamoja na wanafunzi, watu wa kujitolea, watafiti, wabunifu, wawasilianaji, wanaharakati na wafanyakazi wa kupambana na biashara haramu  ya binadamu, ambao walikuja kutoka ulimwenguni kote. Mpango huo unaratibiwa na Talitha Kum, mtandao wa kimataifa wa kupambana na biashara haramu na unahamaisha pia na Umoja wa Kimataifa wa Mama Wakuu wa Mashirika ya Kitawa, kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la KuhamasishaMaendeleo Fungamani ya Binadamu, Baraza la Kipapa la Mawasiliano na Taasisi ya Kipapa la Maisha.

Usiwaache pekee ambao ni wahanga wa biashara haramu ya binadamu

Kwa mujibu wa Sr. Mayra Cuellar wa Mtandao wa Kimataifa wa Talita Kum alisema kuwa: “Kwa bahati mbaya, biashara  haramu wa binadamu ni jambo ambalo linaweza kuathiri nyanja nyingi za maisha yetu, kutoka katika nguo zetu, vifaa vya elektroniki tunavyotumia, hadi chakula tunachokula, kwa sababu hatujui unyonyaji unaoweza kufanyika nyuma ya mambo haya. Hatuna takwimu sahihi kuhusu watu wangapi duniani ni waathiriwa, lakini kulingana na makadirio ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa, tunapaswa kuwa na takriban watu milioni ishirini na tano wanaohusika.” Zaidi ya 70% ni wanawake na watoto, wengi wao hujihusisha na ukahaba na kuombaomba. Ni jambo linalokua kwa sababu linaathiri walio hatarini zaidi, ambao mara nyingi huanguka katika mitego hii mamboleo.” Talitha Kum imekuwa ikiwasaidia wale ambao wametumbukia katika biashara haramu ya binadamu kwa miaka mingi, ikiwapa usaidizi wa kiroho na kimwili. Kwa njia hiyo Sr. Mayra aliongeza  kuwa: "Kamwe hatuwaachi peke yao dhamira yetu ya kwanza ni kuzuia, na kisha pia katika utunzaji na kusindikiza waathirika, katika upatikanaji wa haki. Kwa kawaida tunafanya kazi katika mtandao na taasisi na vyombo mbalimbali vinavyotusaidia katika misheni hii.” 

Vijana ulimwenguni na mapambano dhidi ya biashara haramu

Kuna vijana wengi ulimwenguni ambao wamejitolea kupambana na jambo hili la kusikitisha, kama vile Genc Gjoci, ambaye alikuja Roma kutoka nchini Albania, ili kupata uzoefu wa Juma hili la tafakari na sala pamoja na wenzake: "Ninaamini kuwa kwa mvulana ni kweli changamoto kubwa ya kushiriki katika mada kama vile biashara haramu ya binadamu, alifafanua Genc – Jamii  mara nyingi hutaka tuvutiwe na mambo mengine, na badala yake ni vizuri kujikuta tukiwa na wenzetu wanaofikiri kama mimi, kwa sababu wakati mwingine tunajihisi kuwa peke yetu katika mapambano yetu, na kwa hiyo wakati huu wa mitandao hutupatia nguvu basi wahusishe watu wengine pia, kwa sababu ina maana kwamba tuko kwenye njia iliyo sawa!” Kiukweli, Juma hili kwa vijana pia wanashiriki shughuli tofauti wanazofanya katika nchi zao za asili. “Kuzungumza na kila mmoja  na tunapata mawazo mengi mapya na mawazo mengi. Ni lazima tutoe mifano chanya ya kuigwa kwa vijana, kwa sababu mwishowe, wema daima huvutia na daima ni jambo zuri kuwasaidia wengine”, alieleza Genc -

Mipango ya Juma

Kwa usahihi ili kuongeza ufahamu wa janga la usafirishaji haramu wa binadamu, vijana walipanga kundi la watu alasiri tarehe 6  Februari 2024 katika Uwanja wa Mtakatifu  Maria huko Trastevere, ambalo lilifuatiwa na mkesha wa kiekumene katika lugha tano zinazoongozwa na vipengele 5: maji, moto, hewa, chuma na ardhi. na Wakati huo huo tarehe 7 Februari 2024 vijana hao walishiriki Mkutano na Baba Mtakatifu Francisko.

Mkutano wa kimataifa kwa mabara yote kwa njia ya mtandao

Tarehe 8 Februari 2024  ilikuwa ni kufanya mkutano kwa njia  mtandaoni  kwa  sala na tafakari dhidi ya usafirishaji haramu wa binadamu ambao  uliowaona mabara yote kuanzia saa 3.30 asubuhi kutoka Oceania, na kisha kufuata Asia, Mashariki ya Kati, Afrika, Ulaya, Amerika ya Kusini na, hatimaye, kufunga saa 10.30 jioni  na bara la Amerika Kaskazini. Zaidi ya nchi 50 zinashiri kwa mwaka wa pili mfululizo, kupitia mtandao huku vijana wakijihusisha kupambana na biashara haramu ya binadamu. Tukio hili lilitiririshwa moja kwa moja katika lugha 5 kwenye tovuti: www.prayagainsttrafficking.net.

 

08 February 2024, 11:40