Tafuta

Nia ya Ibada hii ya Misa Takatifu ilikuwa ni kuliombea Kanisa la Tanzania, ulinzi, amani, ustawi na maendeleo, hasa wakati huu, Tanzania inapojiandaa kwa uchaguzi. Nia ya Ibada hii ya Misa Takatifu ilikuwa ni kuliombea Kanisa la Tanzania, ulinzi, amani, ustawi na maendeleo, hasa wakati huu, Tanzania inapojiandaa kwa uchaguzi. 

Jumuiya ya Watanzania Wakatoliki Italia: Sadaka Safi: Unyenyekevu!

Nia ya Ibada hii ya Misa Takatifu ilikuwa ni kuliombea Kanisa la Tanzania, ulinzi, amani, ustawi na maendeleo, hasa wakati huu, Tanzania inapojiandaa kwa uchaguzi ili kuendelea kujizatiti katika ujenzi wa umoja na mshikamano wa Kitaifa. Ilikuwa ni nafasi ya kumkumbuka na kumwombea Marehemu Sr. Maria Antonia Daniel Halot, aliyefariki dunia tarehe 4 Januari 2024 kwa ugonjwa wa Shinikizo la Damu. pamoja na marehemu wengine wa wanajumuiya katika ujumla wao.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Maisha ya kiroho ni safari yenye mwanzo wake, inatua hatua kwa hatua katika vituo vyake mbalimbali na lengo lake ni kuishi vema hapa duniani na kufikia utimilifu wa maisha kwa Mwenyezi Mungu mwenyewe. Mababa wa maisha ya kiroho wameyafananisha na nyakati za siku: asubuhi, mchana na jioni. Thomas Halik (Mwandishi wa Kitabu “Pomeriggio del cristianes imo”) amechambua historia ya Ukristo: akisema asubuhi inaendana na kipindi cha mwanzo cha uinjilishaji, mchana na kipindi cha changamoto na jioni kipindi cha ukomavu. Na huu ndio ukweli katika maisha ya kiroho na hasa safari ya wito, mchanganuo huo una ukweli wake. Hii ni sehemu ya tafakari ya Kipindi cha Kwaresima iliyotolewa na Padre William Bahitwa kwa Jumuiya ya Watanzania Wakatoliki Italia, JWWI, Dominika tarehe 25 Februari 2024 kwenye Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Paulo, kilichoko mjini Roma.

Padre William Bahitwa akitoa mahubiri kwa watanzania wanaoishi Italia
Padre William Bahitwa akitoa mahubiri kwa watanzania wanaoishi Italia

Nia ya Ibada hii ya Misa Takatifu ilikuwa ni kuliombea Kanisa la Tanzania, ulinzi, amani, ustawi na maendeleo, hasa wakati huu, Tanzania inapojiandaa kwa uchaguzi ili kuendelea kujizatiti katika ujenzi wa umoja na mshikamano wa Kitaifa. Ilikuwa ni nafasi ya kumkumbuka na kumwombea Marehemu Sr. Maria Antonia Daniel Halot, aliyefariki dunia tarehe 4 Januari 2024 kwa ugonjwa wa Shinikizo la Damu. Pamoja na Marehemu wa wazazi wa wana umoja waliotangulia mbele ya haki wakiwa na tumaini la ufufuko wa wafu. Maombi yameimbwa na Sr. Maria Benjamina Msendo, wa Shirika la Masista wa Bibi Yetu wa Kilimanjaro, lenye Makao yake makuu Jimbo Katoliki la Moshi, Tanzania.

Baadhi ya mapadre waliohudhuria mkutano wa watanzania Italia
Baadhi ya mapadre waliohudhuria mkutano wa watanzania Italia

Tafakari hii ilipambwa kwa maungamo binafsi na hatimaye, Ibada ya Misa Takatifu. Katika mahubiri yake, Padre William Bahitwa aligusia kuhusu: Abraham aliyekomaa, huku akionesha jioni ya mtu mwenye busara, mwenye mang’amuzi na mtu aliyetulia. Abrahamu katika jioni yake anatoa kipaumbele cha kwanza kwa amani, uchaguzi kwa Lutu, anaunda jeshi kwenda kumwokoa Lutu na zaidi ya yote, anakuwa tayari kumtoa sadaka ya kuteketezwa mwanaye wa pekee na ampendaye Isaka. Wataalamu wa Maandiko Matakatifu wanasema, hadi kufikia uamuzi huu, kulikuwa na mjadala mkali kati ya Abraham una Mwenyezi Mungu. Hata leo hii, bado kuna watu wanaoamini na kuendeleza sadaka ya Kikaanani ya kutoa “watu kafara” ili wapate mafanikio.

Asubuhi, Mchana na Jioni ya Maisha na Wito wa waamini
Asubuhi, Mchana na Jioni ya Maisha na Wito wa waamini

Lakini Mungu alimtoa Mwanaye wa pekee, Kristo Yesu ili ateswe, na hatimaye kufa Msalabani ili kuwakimboa binadamu wote kutoka katika lindi la dhambi na mauti. Kumbe sadaka safi inayompendeza Mungu ni moyo wa unyenyekevu. Isaka anamwakilisha Kristo Yesu katika Agano Jipya. Liturujia ya Neno la Mungu, Dominika ya Pili ya Kwaresima inapania pamoja na mambo mengine, kuimarisha imani na waamini watambue uwepo endelevu na angavu wa Mungu katika maisha yao. Jambo la msingi ni kumsikiliza kwa makini Kristo Yesu. Kumbe, mateso, kifo na ufufuko wa Kristo vimedhihirishwa katika tukio la kung’ara Kristo Yesu, mbele ya Mitume wake watatu.

Watanzania Italia

 

26 February 2024, 14:39