Tafuta

Marehemu wote 15 waliokufa wakiwa wanasali huko Jimbo la Dori nchini Burkina Faso wapumzike kwa Amani,Amina. Marehemu wote 15 waliokufa wakiwa wanasali huko Jimbo la Dori nchini Burkina Faso wapumzike kwa Amani,Amina. 

Burkina Faso:Watu 15 wamekufa katika shambulio la kigaidi wakati wa Misa

Kwa mujibu wa taarifa kutoka jimbo la Dori nchini Burkina Faso,watu hao wameshambuliwa asubuhi ya Dominika tarehe 25 Februari 2024 wakati wa kuadhimishwa misa Takatifu.Shambulio hilo kwa mujibu wa taarifa lilitekelezwa na watu wenye silaha ndani ya Kanisa Katoliki la Essakane.

Vatican News

Idadi ya vifo kutokana na shambulio la kigaidi Dominika asubuhi tarehe 25 Februari 2024 dhidi ya jumuiya ya Kikatoliki ya kijiji cha Essakane nchini Burkina Faso, wakati Misa ikiendelea ni waamini 15. Hayo yametangazwa na Askofu Laurent Bifuré Dabire wa Jimbo Katoliki la  Dori, katika taarifa yake. Kati ya waaathirika hao waamini 12 walikufa papo hapo na watatu walikufa baadaye kutokana na majeraha makubwa.  Pia kuna ripoti za majeruhi wengine wawili.

Kuombea waathirika na uwongofu wa magaidi

Kulingana na vyanzo vya habari, "shambulio hilo lilitekelezwa na watu wenye silaha ndani ya Kanisa katoliki la Essakane na kwa njia hiyo: “Katika hali hizi zenye uchungu, tunawaalika kusali kwa ajili ya pumziko la milele la wale waliokufa katika imani, kwa ajili ya uponyaji wa waliojeruhiwa na kwa ajili ya faraja ya mioyo yenye huzuni. Pia tunawaombea uwongofu wale wanaoendelea kupanda kifo na ukiwa katika nchi yetu. Juhudi zetu za toba na sala katika kipindi hiki cha Kwaresima zilete amani na usalama katika nchi yetu, Burkina Faso.”, Taarifa hiyo inahitimishwa kwa saini na Padre Jean-Pierre SAWADOGO, makamu wa Jimbo la Dori kwa niaba ya Askofu Laurent B. DABIRE, Askofu wa Jimbo Katoliki la Dori nchini Burkina Faso.

Watu 15 wakufa katika shambulio la kigaidi huko Burkina Faso wakati wanasali kanisani

Shambulio jingine la msikiti

Shambulio dhidi ya msikiti ulioko mashariki mwa Burkina Faso pia lilikuwa baya sana.  Kwani: “Watu wenye silaha walishambulia msikiti huko Natiaboani majira ya alfajiri saa 11.00 Dominika, 25 Februari na kuua watu kadhaa, pia ni ripoti iliyotolewa na chombo cha usalama iliyozinduliwa upya na AFP. Waathiriwa, aliongeza mkazi wa eneo hilo, kuwa: “wote walikuwa Waislamu, wengi wao wakiwa wanaume waliokuwa wamekusanyika msikitini kusali.” Chanzo kingine cha habari za ndani kilisema kuwa: “magaidi hao waliingia mjini alfajiri na kuuzingira msikiti huo na kuwafyatulia risasi waamini waliokuwa hapo kwa ajili ya swala ya kwanza ya siku hiyo ambao wengi wao waliuawa akiwemo kiongozi muhimu wa kidini.”

Imesasishwa 25 -02-2024, alasiri  saa 9.11. 

25 February 2024, 16:19