Tafuta

2024.01.11 Mapadre nchini Myanmar wanaendelea na huduma yao kwa wakimbizi na watu wenye shida huko msituni. 2024.01.11 Mapadre nchini Myanmar wanaendelea na huduma yao kwa wakimbizi na watu wenye shida huko msituni. 

Myanmar:Mapadre washerekea na kuadhimisha misa kwenye misitu

Wako karibu na watu,ambapo pia wamesherehekea misa msituni na kupeleka misaada kwa wakimbizi.Hii ni kutokana na vita vinavyoendelea vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka miwili ambavyo vimepelekea watu kukimbia makazi yao,lakini pia watu wa kidini kuwa katika mkumbo huo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Miaka miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, ambayo imeongezeka polepole, imebadilisha sura na mtazamo wa kichungaji wa mapadre, watu waliowekwa wakfu, makatekista, wachungaji wa majimbo mengi ya Myanmar, hasa katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mapigano kati ya jeshi na waasi wa Jeshi wa Ulinzi wa Wananchi, ambao waliungana na wanamgambo wa kikabila waliopo katika maeneo ya mpaka wa Myanmar. Hali ya kijamii ilikuwa na sifa ya kuwepo kwa mtiririko mkubwa wa wakimbizi wa ndani: watu waliolazimika kuacha nyumba zao kutafuta hifadhi katika misitu, mbali na vurugu, ambapo walianza maisha kwa shida; au familia zinazopata hifadhi katika kambi za wakimbizi zilizoboreshwa kuanzishwa kadiri wawezavyo, wakati mwingine hata na parokia za Kikatoliki.

Katika hilo kulizuka hitaji la mabadiliko katika dhana ya kichungaji: ili “kuwa na harufu ya kondoo” kama maneno ya Papa Francisko ya kukaa karibu na watu na kuwashirikisha watu shida na mateso ya maisha kila siku, mapadre, watawa, makatekista pia huacha makanisa kwa muda na kuhamia (kwa muda mrefu au, wakati mwingine, kwa kudumu) hadi mahali pa hatari, kwenye vibanda, au mahema ambako watu waliohamishwa wanaishi. Mfano wa kujitokeza ni jimbo la Loikaw, ambalo eneo lake linashughulikia Jimbo la Kayah (mashariki mwa Myanmar), ambako mzozo wa wenyewe kwa wenyewe unashuhudiwa kwa ukali na mfululizo. Hapa hata Askofu Celso Ba Shwe alifukuzwa kutoka Kanisa kuu, kwanza, alipigwa, kisha akachukuliwa na jeshi la Birmania ambalo lilifanywa kuwa kambi lake msingi.  Kama ilivyothibitishwa na Shirika la Habari za Kimisionari Fides, Askofu aliishi Noeli kama ‘mkimbizi’, huku  akisafiri katika maeneo na parokia mbali mbali za jimbo, kuadhimisha sakramenti, kutembelea kambi za wakimbizi, kubariki na kufariji familia zilizojaribiwa na vita na umaskini.

Wakimbizi wanaishi msituni nchini Myanmar
Wakimbizi wanaishi msituni nchini Myanmar

Kwa mujibu wake Askofu Ba Shwe alisema: “Bwana amenipatia wakati wa kulazimika kusafiri. Licha ya uchungu wa kuondoka katika Kanisa kuu, bidhaa na hati zote za Kanisa letu la mahalia,  hatutajua tutapata nini wakati haya yote yatakuwa wamekwisha  lakini  ninaikaribisha neema hii kwa moyo wazi. Bwana huniruhusu kukutana na watu wengi, kuwa karibu na watu kama siku zote, kusikiliza na kufariji.” Kwa  hiyo Askofu Ba Shwe aidha aliongeza kusema: “Mimi pia ninaishi katika hali ya hatari kabisa, katika zawadi ninayopokea kila siku kutoka kwa ndugu, kutoka kwa makuhani na kutoka kwa watu ninaokutana nao. Ni uzoefu wa imani ya kina katika Utoaji wa Mungu, ambaye ananitunza mimi na sisi sote, na ambayo sitamsahau kamwe.”  “Ni wakati maalum wa ukaribu na upendo kwa Mungu na wengine’, aliongeza, huku akielezea jinsi alivyosherehekea Noeli katika kikanisa ambacho kipo katikati ya msitu. Askofu hayuko peke yake: mapadre wa jimbo mara nyingi wanafuata njia ngumu na huvuka maeneo ya hatari sana, wakisafiri katika maeneo ambayo mapigano yanaendelea. Lakini wanafahamu kwamba, “watu wanahitaji uwepo wetu na kutiwa moyo wakati wa woga na mashaka,” alieleza Padre Paul, mmoja wa mapadre wa Loikaw, kwa kufafanua hali hiyo kuwa: “Kuna zaidi ya kambi 20 za wakimbizi wa ndani ya eneo la parokia moja”.

Huduma inatolewa na mapadre katika familia
Huduma inatolewa na mapadre katika familia

Kati ya parokia 35 za jimbo hilo, zaidi ya nusu zimeachwa kwa sababu mapadre na watawa wamekimbia na waamini kwenda kwenye kambi msituni. Misa zinaadhimishwa za Dominika  zikiwa karibu tupu au katika makanisa rahisi ya mbao yaliyojengwa na waamini. Watu wanaogopa na wana kiwewe.’’ Mapadre, watawa, makatekista, wachungaji na wafanyakazi wa Caritas ‘wanatembea kwenye ukingo wa wembe kwa sababu, katika kutoa faraja ya kiroho na kuleta misaada ya kibinadamu kwa watu waliohamishwa, wanaweza kushtakiwa kwa uwongo na jeshi kwa kuunga mkono upinzani, na hivyo kukamatwa na kuwekwa ndani jela’, alieleza Padre huyo. Tangu mwanzo wa mzozo, Kanisa la Loikaw limehusika katika kazi ya kibinadamu, hata katika hali mbaya: kwa kweli, ikiwa mstari wa mbele wa mapigano unabadilika, watu waliokimbia makazi mara nyingi wanapaswa kuhama.

Katika mazingira haya, miundombinu ya makazi, usambazaji wa maji, chakula na majaribio ya kuandaa shule ni changamoto ya mara kwa mara. Kanisa la ndani, pia kutokana na misaada kutoka nje ya nchi, limeandaa kliniki zinazotembea, mipango ya misaada ya dharura na programu za elimu kwa watoto, vijana na vijana ambao, kwa karibu miaka miwili, hawajahudhuria shule mara kwa mara, daima kwa lengo la "kusimama karibu watu.’’ “Tunatumai na kuomba kwamba watu wa nchi hii waweze kurejea kuishi kwa amani, utu na uhuru wa kweli. Tunasali kila siku kwa ajili ya kurejesha amani na haki nchini, kwa ajili ya upatanisho na wongofu wa watu wetu”, anasema Askofu Celso Ba Shwe.

Wakati huo huo, ripoti za habari katika siku za hivi karibuni zinathibitisha vurugu dhidi ya raia: katika shambulio la anga lililozinduliwa na jeshi mnamo Januari 7 katika eneo la magharibi mwa nchi, raia 17 waliuawa, pamoja na watoto, na zaidi ya watu 30 walibaki. Shambulio hilo lilitokea wakati wa hafla ya kidini katika mji wa Kanan, kati ya Khampat na Boukkan, katika wilaya ya Tamu, eneo la dayosisi ya Kikatoliki ya Kalay. Uvamizi huo uliharibu zaidi ya nyumba kumi, pamoja na shule na kanisa. Mashambulizi kama haya yanaendelea kuongeza idadi ya wakimbizi wa ndani, raia wote, haswa wazee, wanawake na watoto ambao kwa ujumla wamevuka milioni 2.5 nchini (PA).

Huduma kwa wakimbizi nchini Myanmar hata kwenye misitu
11 January 2024, 14:27