Tafuta

2024.01.312024.01.31 Askofu Claudio Giuliodori, akiwa na watawa wa Shirika la Mtakatifu Gemma, Askofu Muu wa Dodoma Tanzania na wageni 2024.01.312024.01.31 Askofu Claudio Giuliodori, akiwa na watawa wa Shirika la Mtakatifu Gemma, Askofu Muu wa Dodoma Tanzania na wageni 

Chuo Kikuu Katoliki na Gemelli nchini Tanzania katika Hospitali ya Mt.Gemma

Kuanzia Januari 27 hadi 5 Februari 2024 ujumbe unatembelea hospitali ya Mtakatifu Gemma mjini Dodoma,ambako idara mpya ya magonjwa ya akina mama na uzazi inajengwa,shukrani kwa ushirikiano na Chuo Kikuu na msaada wa kifedha wa Baraza la Maaskofu wa Italia(CEI).

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Wajumbe kutoka Chuo Kikuu cha Kikatoliki na Taasisi ya Agostino Gemelli IRCCS Mfuko wa Chuo Kikuu waliondoka mnamo Januari 27 ili kusindikiza hatua ya nne ya moango wa kusaidia, kushirikiana na kuendeleza shughuli za afya ya kijamii na miundo ya nchi ya Afrika Mashariki, kama sehemu ya mipango ya mshikamano na kujitolea kimataifa kwa Mfuko  na Chuo Kikuu. Utume huu mpya unazaliwa, hasa, kwa lengo la kuimarisha na kusaidia shughuli za Hospitali ya Mtakatifu Gemma ya Dodoma kupitia awamu zote za mpango, shukrani kwa shughuli za ushauri na mafunzo, ukiambatana na uundaji mzima wa miundo mipya ya jengo la Idara ya Uzazi na uandaaji wa Chumba cha Upasuaji na Chumba cha Kujifungulia, shukrani kwa utaalamu wa wafanyakazi wa matibabu na afya wa Eneo la (wataalamu ya uzazi (Gynecology) na wakunga(Obstetrics) wa Mfuko wa Gemelli uliyoongozwa na Prof. Antonio Lanzone, Profesa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi katika Kitivo cha Tiba na Upasuaji cha Chuo Kikuu Katoliki.

Madakatari watawa wakisaidiana na wataalamu kutoka Italia katika Hospitali ya Mt Gemma
Madakatari watawa wakisaidiana na wataalamu kutoka Italia katika Hospitali ya Mt Gemma

Ujumbe huo, unaojumuisha madaktari wa magonjwa ya wanawake na wafanyakazi kutoka Usimamizi wa Kiufundi, TEHAMA na ubunifu wa teknolojia ya afya wa Mfuko wa Gemelli ulioongozwa na Mhandisi Giovanni Arcuri, inaongozwa na Askofu Claudio Giuliodori, Msaidizi Mkuu wa kikanisa wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki, ambaye amefuata tangu mwanzo, yaani tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000, mipango ya ujenzi na maendeleo ya Hospitali ya Mtakatifu Gemma na  uundaji wa mipango mitatu ya awali nchini Tanzania ambayo imepata msaada wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI): “Shukrani kwa kiungo na baadhi ya marafiki kutoka Trentino na ujuzi wa moja kwa moja wa Shirika la  ndani la Masista wa Mtakatifu  Gemma waliopo Jimbo Kuu la  Dodoma, baada ya ujenzi wa hospitali hiyo iliyozinduliwa mnamo mwaka 2004, na kutoa mafunzo kwa watawa na wauguzi 30, Watawa 3 na mpango ulioanza mnamo mwaka 2009, wa Jengo la huduma mpya ya gastroscopy uliundwa, huduma ambayo haikupatikana wakati huo ndani ya eneo la kilomita 500 la Dodoma (2016) na kusimamiwa kwa miaka mitatu ya kwanza kutokana na ushirikiano wa  madaktari 20 wataalamu wa gastroenterologists wenye utaalamu wa matibabu yam fumo ho wa gastroenterology wa kujitolea wa Kiitaliano ambao walichukua zamu kwenye eneo hilo kwa kipindi chote hicho.  Kwa sasa mpango huo unakua tena na unaongeza nafasi za hospitali maradufu, ukitoa muundo mzima mpya kwa magonjwa ya uzazi na magonjwa ya wanawake.”

Jengo jipya la Hospitali ya Mtakatifu Gemma Dodoma kwa mpango wa Hospt Gemelli Roma
Jengo jipya la Hospitali ya Mtakatifu Gemma Dodoma kwa mpango wa Hospt Gemelli Roma

“Kwa miaka mingi, Baraza la maaskofu Italia (CEI) limesaidia shughuli za Hospitali ya Mtakatifu Gemma kwa fedha za Mfuko wa 8x1000 ambazo wananchi huchangia kwa Kanisa Katoliki. Huu ni msaada kwa wanawake na watoto, katika awamu maalumu kabisa  kwa afya ya mama na mtoto, ambayo inaweka umakini wa mara kwa mara kwenye usindikizaji wa watu wanaokaribishwa. Msaada wa dhamana na utunzaji, kwa umahiri na uharaka, ni njia madhubuti ya kuwa karibu na kukuza utu wa mwanadamu,” alisisitiza Askofu  Giuseppe Baturi, Askofu Mkuu wa Cagliari na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI.)

Masisita wa Mtakatifu Gemma wakiwa na Askofu huko Dodoma
Masisita wa Mtakatifu Gemma wakiwa na Askofu huko Dodoma

Kwa njia hiyo mpango mpya, ulioandaliwa na Usimamizi wa Kiufundi wa Mfuko wa Gemelli wakati wa 2022, utajibu kwa jengo la kisasa zaidi  na vigezo vya udhibiti na utaweza kukidhi mahitaji mawili muhimu: hitaji la kupanua huduma ya uzazi kutokana na ongezeko kubwa la wanawake wanaojifungua ambao hukimbilia hospitali ya Dodoma na kwa hivyo, hitaji la kuanzisha huduma kwa watoto wengi wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti)ili kuepusha kuhamishwa katika hospitali pekee iliyopo, umbali wa kilomita 35.

Askofu akiwa na watoto huko Dodoma
Askofu akiwa na watoto huko Dodoma

Idadi ya watu mjini Dodoma, kiukweli, imeongezeka maradufu kati ya 2017 na 2018, kutokana na upanuzi wa majengo, hasa katika vitongoji vya pembezoni: hospitali ya Mtakatifu Gemma iko kimakusudi katika mojawapo ya vitongoji vilivyo na watu wengi, ikiwa ni kituo muhimu cha kumbukumbu kwa familia maskini Zaidi katika mji. Shukrani kwa ufadhili wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI)majengo ya afya yataimarishwa na kurutubishwa, kwanza kabisa kwa kuipatia hospitali idadi ya kutosha ya maeneo ya hospitali kwa ajili ya wanawake wanaojifungua, kwa kujenga jengo jipya la wodi mpya ya uzazi, na kwa huduma mahususi ya matunzo kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati(Njiti) ubunifu ambao unaweza kusaidia pia vituo vingine vya afya vya umma na binafsi katika mkoa wa Dodoma na maeneo jirani. Ushirikiano na wafanyakazi wa afya wa kujitolea wa Italia pia utaendelea kuwa muhimu: msaada wa wafanyakazi wa afya wa Hosptali kuu ya Gemelli utakuwa wa msingi kwa mafunzo ya “kazini” kwa ajili ya uzinduzi wa idara mpya ya uzazi na kwa ajili ya huduma ya watoto wachanga, pamoja na mpango wa Utumishi wa Umma kwa Wote ambao Chama cha Chuo Kikuu cha Ushirikiano wa Kimataifa (AUCI)kinazindua katika Hospitali ya Mtakatifu Gemma.

Mpango wa Gemelli na Hospitali ya Mt Gemma Dodoma
31 January 2024, 15:28