Tafuta

Tafakari Liturujia ya Neno la Mungu Dominika ya III ya Kipindi cha Majilio Mwaka B wa Kanisa: Furaha ni utajiri wa watu wote wanaomwamini Mungu Tafakari Liturujia ya Neno la Mungu Dominika ya III ya Kipindi cha Majilio Mwaka B wa Kanisa: Furaha ni utajiri wa watu wote wanaomwamini Mungu  (Vatican Media)

Tafakari Dominika ya III Majilio Mwaka B wa Kanisa: Furaha ya Injili

Baba Mtakatifu Francisko katika Wosia wake wa Kitume Furaha ya Injili, “Evangelii gaudium” anasema, furaha ya Injili huijaza mioyo na maisha ya wote wanaokutana na Kristo Yesu. Wale wanaoikubali zawadi yake ya ukombozi wanawekwa huru kuondokana na dhambi, uchungu, utupu wa ndani na upweke. Pamoja na Kristo Yesu, daima furaha inazaliwa upya.” Evangelii gaudium, 1.Wazo kuu la Dominika ya tatu ya Kipindi cha Majilio ni furaha ambayo ni utajiri kwa waamini!

Na Padre Joseph Herman Luwela, - Vatican.

UTANGALIZI: Leo tunawasha mshumaa wa furaha katika Dominika ya tatu ya majilio, tulipoanza kipindi hiki cha majilio tulianza na toba, tumekua tukiomba huruma ya Mungu, sasa dirisha la furaha linafunguliwa leo dominka ya tatu ya majilio ‘amabayo mama kanisa hiita kwa lugha ya kilatini” "Gaudete" Neno la kwanza la wimbo wa mwanzo leo ni "Furahi!" Huu ni utamaduni amabao ulitumika kabla ya mtaguso wa pili wa vatikano. Na kwa hivyo dominika hii hujulikana kama "Dominika ya Gaudete". Yaani Dominika ya furahini kwanini tunafurahi kwasababu tayari tumevuka nusu ya kipindi cha majilio, na mwokozi yu karibu kuja kama ilivyo katika jamii zetu mgeni mahusi anapokaribia kufika wanyeji huwa na shangwe na furaha ya kumpokea mgeni huyo na watu huamini kuwa mgeni huleta neema, ndipo tunaponogeshwa na maneno ya wahenga” mgeni njoo mwenyeji apone.” Baba Mtakatifu Francisko katika Wosia wake wa Kitume Furaha ya Injili, “Evangelii gaudium” anasema, furaha ya Injili huijaza mioyo na maisha ya wote wanaokutana na Kristo Yesu. Wale wanaoikubali zawadi yake ya ukombozi wanawekwa huru kuondokana na dhambi, uchungu, utupu wa ndani na upweke. Pamoja na Kristo Yesu, daima furaha inazaliwa upya.” Evangelii gaudium, 1.

Waamini wanaitwa na kutumwa kutangaza furaha ya Injili
Waamini wanaitwa na kutumwa kutangaza furaha ya Injili

UFAFANUZI: Kabla ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, Kipindi cha Majilio kilikuwa ni msimu wa toba, wakati huu kulikuwa na siku nne za kufunga katika kipindi hiki na kuhani mwadhimishaji wa misa alivaa mavazi na rangi ya zambarau au urujuani kama alama ya toba. Hali ya hewa ilikuwa ya kutisha na ya toba.  Kwa hiyo, katikati ya yote, sisi sote tulihitaji kukumbushwa kile amabcho tumekuwa tukijiandaa kumpokea Kristo aliye furaha yetu timilifu. Katikati ya toba dirisha la furaha linafunguliwa na mwangaza unatujilia katikati ya giza. Siku hii, pia, mavazi ya violet katika makanisa mengi hutoa njia ya rangi ya chini ya toba, nyekundu ya “pinkish”, urujuani ya   inayoashiria kuwa kuna furaha sasa Kadiri ya Kamusi ya Kiswahili neno “furahi” limetokana na “furaha” ambayo ni “hali ya ukunjufu wa moyo, kuchangamka, kuridhika, kustarehe kwa ajili ya jambo Fulani.” Katika Biblia neno “furahi” limejitokeza mara 205 hivi na neno “furaha” limejitokeza kama mara 214. Hii inatokana na umuhimu wa neno hili kwa vile Mungu hakutuumba ili tuhuzunike bali tufurahi katika Yeye anayetupenda. Katika somo la kwanza, Nabii Isaya anatabiri ujio wa Masiha ambaye Roho wa Bwana atakuwa juu yake. Huyo ataondoa huzuni ya utumwani Babeli na kuleta furaha kwa sababu Bwana amemtia mafuta kuwahubiri wanyenyekevu Habari Njema, kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru na waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.

Roho wa Bwana amenipaka magfuta kutangaza na kushuhudia Injili
Roho wa Bwana amenipaka magfuta kutangaza na kushuhudia Injili

Unabii huu unatimia katika Yesu Kristo alipousoma Yeye mwenyewe nyumbani kwake Nazareti na kuwaambia machoni “leo Maandiko haya yametimia masikioni mwenu” (Lk 4:21). Kwamba Roho wa Bwana yu juu ya Kristo naye amemtia mafuta atuhubiri mimi, wewe, sisi masikini, Habari Njema, basi hatuna lingine zaidi ya kuimba na Nabii Isaya “nitafurahi sana katika Bwana maana amenivika mavazi ya wokovu…” Kwa kusema hivyo, Yesu anajitambulisha wazi kuwa ni mfalme mpakwa mafuta ambaye ni Masihi na Mwokozi wa watu wa Mungu. Na kwa nini amekuja? Kwa nini alitumwa? " amejibu kwa kusema Amenituma ili alete habari njema kwa maskini, ili kuponya mioyo iliyovunjika; kutangaza uhuru kwa wafungwa, uhuru kwa wale walio gerezani; kutangaza mwaka wa neema ya Bwana yaani wakati ulikubakika ndio sasa kwani muda wa Mungu ni di sahihi ebu tutumie fursa hiitena." Maisha yetu ya leo, ambapo umasikini, mateso, chuki, mapigano, uonevu, ukandamizwaji wa haki, ukosefu wa chakula na huduma msingi za kijmamii na kiutu kama afya, maji, elimu, nakadhalika, kutopokeleka kukataliwa, ukimbizi, ukosefu wa ajira, kusukumizwa pembezoni mwa jamii, ulemavu.  Pamoja maendeleo ya teknolojia katika ulimwengu wa leo lakini bado kuna changamoto nyingi sana ya mamilioni ya watu wanaishi katika mazingira magumu na hatarishi. Katika Maisha haya kijamii, kihisia, kiakili, kiroho); aina nyingine za utumwa bado kuna matamanio, tamaa, ulevi, katika matumizi yaliyopitiliza mahitaji hasa kwa wale wenye ukwasi mkubwa hivyo wanakua na upofu na uziwi wa wale ambao hawawezi kuona maisha halisi, na u maana katika yote ya mengi wanayofuatilia; kukosa maarifa na ubunifu. Ikiwa Bwana amekuja kutukomboa kutoka kwa haya yote, basi hakika tuna sababu ya kufurahi. "Nafurahi kwa ajili ya furaha katika Bwana... kwa maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunga katika vazi la uadilifu."

Tangazeni na kushuhudia furaha ya Injili katika maisha
Tangazeni na kushuhudia furaha ya Injili katika maisha

Kuja kwa Yesu ni ahadi kwa sisi sote na ni ukamilifu huu na uadilifu ambao ni wokovu na sio tu kupata pasipoti ya dakika ya mwisho kwenye kitanda chetu cha kifo na kucheza kinubi milele katika mawingu. Wokovu ni uzoefu halisi ambao sisi sote tunaitwa kushiriki katika maisha yetu hapa na sasa. Kama bado hatujapata uzoefu huo, basi tunaweza kusema kwamba Krismasi haijawahi kuja katika maisha yetu. Hatujakutana na Yesu bado, Yesu ambaye anatufanya kuwa wakamilifu, ambaye anatukomboa kutoka kwa aina zetu za utumwa. Mtume Paulo katika Somo la pili anasema furaha ni kwa ajili ya watu wote ana furaha hiyo huja kupitia Yesu Emmanuel. "Kuwa na furaha wakati wote."  Hata hivyo, kwa Mkristo wa kweli, furaha ni uzoefu wa msingi wa maisha ya kila siku, hata kama, sasa au baadae, kuna matatizo chungu nzima ya kukabiliana nayo. Ufunguo wa furaha yetu ya kudumu ni ukweli na upendo usio na masharti ambapo Mungu anatuongoza na utayari wa kuzungumza na kutenda kwa ujasiri kwa jina lake kwaajili yetu na jirani. Injili ya leo (Yn 1:6-8, 19-28) inazungumza pia juu ya kufurahi. Inamzungumzia Yohane Mbatizaji mwenye mengi ya kujadili. Huyu hakuwa mtu wa utani utani kama sisi wengine. Aliishi peke yake mbali na watu, alikula panzi tu na asali na akavaa nguo za ngozi, alipokuja kwa watu alihubiri vitisho na adhabu. Hata hivyo aliifurahia siku ya Bwana ilipofika, alipoulizwa kama Yeye ni Masiha alijibu bila kusita kwamba yeye siye, akamtangaza na kumtambulisha Bwana akisema “katikati yenu amesimama yeye msiyemjua ninyi. Ndiye yule ajaye nyuma yangu, ambaye mimi sistahili kulegeza gidamu ya kiatu chake.” Tuungane na Yohane Mbatizaji katika kufurahi, tunazo changamoto nyingi lakini wakati fulani inafaa kumwachia tu Mungu na kufurahi. Tufurahi leo kwa sababu dunia ishashindikana hivi tuache mawazo na masahibu yetu, tumwachie Mungu magonjwa, misiba, vikwazo na mengine tuliyonayo nasi tumfurahie Bwana atakayezaliwa kwetu.

Kristo Yesu ni chemchemi ya furaha ya kweli katika maisha
Kristo Yesu ni chemchemi ya furaha ya kweli katika maisha

Kwa kila mmoja wetu, kwa ubatizo wetu na ushirika wetu katika familia ya Kristo, hajatumwa, kwa wazi, kuwa Mwanga wa asili bali kutoa ushuhuda kwa Nuru. Mahubiri ya Mlimani yanatuzungumzia kama "nuru ya ulimwengu" lakini sisi ni nuru kwa njia ile ile kama mwezi unavyoakisi kutoka katika nuru ya jua na kutuangazia wakati wa usiku. Tunapojiandaa kusherehekea Noeli na kuja kwa Mungu katika maisha yetu kupitia kwa Yesu tunahitaji pia kujikumbusha kwamba tumeitwa kuwa njia ya kumleta Yesu katika maisha ya watu wengine. Kuna watu wengi sana huko nje ambao wanaishi katika giza. Kuna wengi ambao ni maskini kwa njia nyingi, ingawa kifedha wapo vizuri. Wengi ambao hawana uhuru wa kweli, uhuru wa kuchagua ukweli na upendo katika yote wanayofanya na kusema. Wengi ambao ni viziwi na walaji karibu nao. Wengi sana, katikati ya furaha zote za juujuu, ambao wanahisi upweke, wasiohitajika, kukataliwa, kutengwa. Mioyo mingi iliyovunjika katikati ya sherehe zote. Kuna watu ambao huchukia tu Sherehe ya Noeli kwa sababu inaongeza tu maumivu yao ya ndani na huzuni kubwa. Mtakatifu Paulo, Mwalimu na Mtume wa Mataifa leo anahamasisha jambo hilo la kufurahi daima (1Tes 5:16-24). Furaha ni dalili ya uwepo wa ufalme wa Mungu katika moyo wa mtu. Kadiri ya Mtakatifu huyu tunapata furaha katika kuomba bila kukoma na kushukuru kwa kila jambo, kutokumzimisha Roho, kutotweza Unabii, kushika lililo jema na kujitenga na ubaya. Tunaposali tunakutana na Mungu naye anatujalia mahitaji yetu, tunaposhukuru tunaonesha kujali na matokeo ya hayo mawili ni kujipatia moyo mwepesi wenye furaha takatifu... tupige magoti na kupokea maombezi ya Mtume huyu wa mataifa anapotubariki akisema… “Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa, nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo. Yeye ni mwaminifu ambaye awaita, naye atafanya, amina! Jitahidi leo umtembelee jirani na umwambie “Rafiki, acha kuhuzunika, anza leo kufurahi, unastahili, kwa kuwa Mungu wa amani yu pamoja nawe!”

Liturujia D3 Majilio
16 December 2023, 14:04