Tafuta

Misa ya Askofu Mkuu Lompo wa Jimbo Kuu la Niamey Nchini Niger. Misa ya Askofu Mkuu Lompo wa Jimbo Kuu la Niamey Nchini Niger. 

Niger,Askofu mkuu wa Niamey anasali kwa ajili ya mwaka mpya wa amani na usalama

Kwa kuzingatia mwaka mpya unaokuja Askofu Mkuu Lompo anawatakia Watu wote wa Niger,bila kujali dini,kuwa waaminifu kwa Mungu,licha ya hali ngumu ya kijamii na kisiasa.Miezi michache baada ya mapinduzi,lengo la mwaka mpya wa kichungaji ni kutembea pamoja ili kubadilisha mazingira ya kijamii.

Françoise Niamien  na Angella Rwezaula -Vatican.

Katika tathmini yake ya mwaka 2023 ya maisha ya Kanisa nchini Niger, Askofu Mkuu Laurent Lompo, wa Jimbo Kuu Katoliki ka Niamey, amesifu “uchangamfu wake, licha ya matatizo yote”. Mwaka ambao unakaribia kuisha kiukweli umekuwa wenye matukio mengi, Amesisitiza hayo Askofu Mkuu  huku akizungumza na Vatican News. "Mwaka wa uchungaji unaokaribia kuisha ulifunguliwa huko Niamey  mnamo mwezi Oktoba iliyopita katika Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Msaada wa Milele kwa kuongozwa na mada: “Katika familia ya Kanisa la Mungu, tunatembea pamoja kwa ajili ya mabadiliko ya mazingira yetu ya kuishi. Ni mada  inayohusishwa na ile ya Sinodi ya Kisinodi, itakayodumu hadi 2024. “Kwa msukumo wa maadili ya Injili, kutembea pamoja kunatufaa sana katika mabadiliko haya Njia hii," alieleza kuwa: “itatufanya tuwe ushuhuda hai wa upendo wa Kristo katika nchi yetu yenye Waislamu wengi. Mchakato wa kuleta mabadiliko ambao pia unapitia mafunzo na kujitolea kwa walei pamoja na mapadre na watawa”.

Mapinduzi ya kijeshi mara tano nchini Niger

Askofu mkuu Lompo, aidha alimshukuru Mungu kwa kumruhusu kuadhimisha Jubilei yake ya fedha kama Padre mnamo mwezi Oktoba iliyopita, katika sherehe iliyoambatana na kuwekwa kwake wakfu katika Kanisa Kuu la Niamey. Kuhusu maisha ya kijamii na kisiasa ya nchi hiyo, Askofu Mkuu Lompo alikumbuka "mapinduzi yaliyompindua Rais Mohamed Bazoum tarehe 26 Julai 2023, ikiwa ni mara ya tano tangu uhuru wa nchi hiyo kuwapo mnamo mwaka 1960. Katika kujibu, wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) waliweka sheria ya vikwazo vikali vya kiuchumi na kifedha mapema Agosti, vikitaka kurejeshwa kwa utaratibu wa kikatiba." Hata hivyo Askofu mkuu wa Niamey anaamini kwamba "hali ya nchi licha ya kuwa ngumu sana kutokana na  mtazamo wa kiuchumi na kijamii, ni funzo kwa watu wa Niger, ambao katika ahadi zao zote wanaomba kumtumaini Mungu. Kupitia ahadi ya kumtumaini Kristo," aliongeza kusema, “tutaweza kukabiliana na changamoto zote zitakazotupeleka kwenye ushindi dhidi ya ugaidi unaoendelea kuitumbukiza nchi yetu katika maombolezo”.

Amani na usalama

Katika kipindi cha Noeli, Askofu Lompo aliomba kwamba katika  "Siku Kuu ya kuzaliwa kwa mtoto Yesu jamii  ijitaidi kubaki daima kuwa jumuiya hai za uaminifu kwa Mungu kwa matumaini ya ulimwengu bora, licha ya ukosefu wa usalama ulioene. Uaminifu kwa Mungu katika ahadi zetu zote utatuongoza kwenye njia za ushindi, alisisitiza tena," akiwaalika "Wakristo na Waislamu kufanya kazi pamoja kwa umoja, ili umoja huu katika uaminifu uweze kuleta ushindi kwa Niger.”

Upepo wa demokrasia

Niger imekumbwa na ugaidi wa kijihadi tangu mwaka 2013. Katika mwaka wa 2023, mashambulizi yamesababisha vifo vya takriban watu 1,200, wakiwemo wanajeshi na raia. "Mnamo 2024 tunaomba kwamba taasisi mpya iliyoundwa na mamlaka ya sasa ya nchi inaweza kupumua upepo wa demokrasia, ili watu wa Niger waweze kuishi kwa amani, mshikamano wa kijamii na usalama. Haya ndiyo matarajio yetu.”

Matashi mema na amani nchini Niger yameoneshwa na Askofu Mkuu Lompo wa Niamey,Niger
29 December 2023, 12:09