Nchi Takatifu,Gaza:mauaji ya Herode yamerudiwa tena
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mauaji ya watu wasio na hatia, yaliyotafutwa na Herode, yamerudiwa miaka elfu mbili baadaye. Hayo ni maneno mazito yaliyotamkwa na Padre Ibrahim Faltas, Msimamizi wa kuhifadhi Nchi Takatifu, katika siku ambayo Mama Kanisa aliadhimisha Mashahidi Watakatifu Wasio na Hatia, tarehe 28 Desemba. Padre Mfransiskani katika mahubiri yake huku akirejesha kifungu cha Injili kinachosimulia juu ya “nguvu kali ya chuki na uovu juu ya kundi la watoto wasio na hatia, waliouawa kwa kiu ya ya Herode kutaka kuokoa uwezo wake kabali kimevuka karne na kusimamishwa, kukua hadi leo yetu.”
Je hatia ya watoto ni kuzaliwa Gaza, Kiev au Damasco?
Katika habari zilizotolewa na Gazeti la Habari za kidini la SIR la Baraza la Maaskofu Italia, limebainisha kuwa, Padre Faltas alisisitiza: “Leo tunayapitia moja kwa moja, tumeona picha za maelfu na maelfu ya watoto waliokufa, wakiwa wamefunikwa kwa mashuka meupe na maelfu ya watoto wakitangatanga katikati ya vifusi, wakiwa na sura ya hofu, wamezungukwa na vumbi wakiwatafuta mama na baba zao, lakini sura hizo hazipo tena. Kuna zaidi ya watoto elfu kumi waliokufa na yatima sasa." Hawa "ndio watu wapya wasio na hatia wa karne hii na hatia yao labda ya kuzaliwa Gaza au Kiev au Damasco, lakini ni mashahidi wasio na hatia kutokana na unyama wa mantiki ya kibinadamu ambayo imevunja mustakabali wa kizazi kipya, na kuzikwa chini ya rundo hili kubwa la vifusi na kila wazo la Amani”.
Mashahidi Watoto wasio na hatia, wana majina halisi
Padre Faltas aidha alieleza:“Watoto wale wafiadini na wasio na hatia, leo hii ni wa vita vinavyoendelea, hapa katika nchi yetu, kama ilivyo katika vita vingine vilivyosahaulika duniani, wana majina halisi ya watoto, lakini pia ni wanandoa vijana, wazee, wagonjwa, wanaongoja majibu ya upendo na maombi yetu kutoka mbinguni. Tuko kwenye milenia ya tatu na sehemu nyingi za dunia, mauaji ya 'watu wasio na hatia' yanaendelea kwa kusikitisha, kuna idadi ya watoto ambao hawana chakula, wagonjwa ambao hawapati matibabu, kwa bahati mbaya mara nyingi hunyonywa ni waathiri wa vurugu. Wao ni 'mashahidi wapya wasio na hatia' wa leo hii, pigo baya katika ulimwengu wetu wa leo. Hatuwezi kukubali kwamba watu wako kwenye baridi, bila mkate, bila maji, bila umeme, bila nyumba, bila mahali salama pa kupata makazi. Lazima tuchukue hatua na kukomesha kashfa hii isiyovumilika, ambayo inawaona watoto kama wathiriwa.”