Tafuta

Kanisa Kuu la Kuzaliwa kwa Bwana, Bethlehemu. Kanisa Kuu la Kuzaliwa kwa Bwana, Bethlehemu. 

Nchi Takatifu,Mapatriaki na wakuu wa Makanisa:Ni Noeli,vurugu zikome

Kuzaliwa kwa Kristo ni ujumbe wa kimungu wa tumaini na amani hata katikati ya mateso.Wameandika viongozi wa jumuiya za Kikristo za Yerusalemu ambamo wanashutumu vurugu zinazoendelea na mateso makubwa yanayosababishwa na vita pamoja na kutoa mwaliko wa matumaini na kujitolea kwa ajili ya amani ya haki na ya kudumu.

Vatican News

“Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume; uweza wa kifalme utakuwa begani mwake, naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.” Kwa tangazo hilo la msingi kwa ubinadamu,lililochukuliwa kutoka kwa kitabu cha nabii Isaya, ni Ujumbe wa Mapatriaki na Wakuu wa Makanisa Nchi Takatifu kwa ajili ya Siku Kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana 2023  unavyofunguliwa.  Ujumbe huo unaendelea kubainisha kuwa:“Tunaleta salamu zetu za Noeli kwa waamini duniani kote katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, Mfalme wa Amani, aliyezaliwa hapa Bethlehemu zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita. Marejeo ya matukio ya sasa hayawezi kuepukika. Katika kurefusha matakwa haya tunafahamu vyema kufanya hivyo wakati wa maafa makubwa katika nchi aliyozaliwa Bwana wetu.”

Katika kipindi cha miezi miwili na nusu iliyopita, jeuri la vita limesababisha mateso yasiyowazika kwa mamilioni ya watu katika Nchi yetu Tuipendayo. Vitisho vyake vinavyoendelea vimeleta taabu na maumivu yasiyoweza kufarijiwa kwa familia nyingi katika eneo letu, na kuibua vilio vya huruma vya uchungu kutoka kila sehemu ya dunia. Kwa wale ambao wanajikuta katikati ya hali mbaya kama hii, tumaini linaonekana kuwa mbali na haliwezi kufikiwa. Na bado, ni katika ulimwengu kama huo ambapo Bwana wetu Mwenyewe alizaliwa ili kutupa tumaini.” Mapatriaki na wakuu wa Makanisa ya Nchi Takatifu wanakumbuka kwamba wakati wa Noeli ya kwanza hali haikuwa tofauti sana na ile ya leo hii. Hivyo Bikira Maria na Mtakatifu Yosefu walipata shida kupata mahali pa kuzaliwa kwa mtoto wao, na ilikuwa ni mauaji ya watoto. Kulikuwa na uvamizi wa kijeshi. Na kulikuwa na Familia Takatifu iliyolazimishwa kuhama kama wakimbizi. Kwa nje, hakukuwa na sababu ya kusherehekea zaidi ya kuzaliwa kwa Bwana Yesu.

Hata hivyo, katikati ya dhambi na uchungu mwingi, Malaika aliwatokea wachungaji akitangaza ujumbe wa matumaini na furaha kwa ulimwengu wote kuwa: 'Msiogope, kwa maana, tazama, nawatangazia furaha kuu itakayokuwa kwa mataifa yote, kwa maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana. Yesu, Emmanueli, ni Mungu pamoja nasi.” Katika Neno la kufanyika mwili wa Kristo, Mwenyezi alitujia kama Emmanueli, 'Mungu pamoja nasi', ili kutuokoa, kutukomboa na kutubadilisha. Kwa njia hii maneno ya nabii Isaya yalitimia asemapo: “Bwana amenitia mafuta, ili kuwatangazia walioonewa habari njema, kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na waliofungwa kufunguliwa kwao, na waliofungwa kufunguliwa kwao, na kuutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.” Huu ni ujumbe wa kimungu wa matumaini na amani ambao Kuzaliwa kwa Kristo hututia moyo ndani yetu, hata katikati ya mateso. Kristo mwenyewe, kiukweli, alizaliwa na kuishi katikati ya mateso makubwa. Hakika aliteswa kwa ajili yetu hata kufa kwake msalabani, ili nuru ya tumaini iangaze katika ulimwengu, kulishinda giza. Tukomeshe vurugu na tushirikiane kwa amani.”

Katika ujumbe wa viongozi hawa wa kidini wa Makanisa ya Yerusalemu hakuna upungufu wa kukemea vitendo vyote vya kijeuri vinavyofanyika, wakitaka kukomeshwa kwao. Vivyo hivyo, wanaandika tena tunawaalika watu wa dunia hii na duniani kote kutafuta neema ya Mungu ili kujifunza kutembea na kila mmoja katika njia za haki, huruma na amani. Mwisho tunawaalika waaminifu. na wale wote wenye nia njema wafanye kazi bila kuchoka kwa ajili ya misaada ya wanaoteseka na kwa ajili ya amani ya haki na ya kudumu katika ardhi hii ambayo ni takatifu sawa na imani tatu za tauhidi. Kwa njia hii, tumaini la Noeli litazaliwa tena, kuanzia Bethlehemu na Yerusalemu hadi miisho ya dunia, wanahitimisha  na hivyo kutambua maneno ya kufariji ya Zekaria, kulingana na ambayo mapambazuko kutoka juu yatatuangazia, kuwaangazia wale walioketi katika giza na uvuli wa mauti, na kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya uzima.

Ujumbe wa Mapatriaki wa Nchi Takatifu
23 December 2023, 18:22