Tafuta

Mti wa Mapambo ya Siku kuu ya Noeli katika jiji la Shanghai nchini China. Mti wa Mapambo ya Siku kuu ya Noeli katika jiji la Shanghai nchini China.  (ANSA)

Kutoka Beijing hadi Mongolia ya Ndani,Noeli ya imani na upendo wa Wakatoliki,China

Tarehe 25 Desemba 2023 wakati wa misa takatifu,Askofu wa Shanghai aliwaalika kila mtu kukamilisha hija yake binafsi ya kumwabudu Mtoto Yesu na kufurahia zawadi ya wokovu ambayo ametuletea ili furaha ya kila Mkristo iweze kuwa baraka kwa wengine katika maisha ya kila siku katika familia na mahali pa kazi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Noeli ya imani na upendo ilishuhudiwa na jumuiya za Kikatoliki katika majimbo yote ya Jamhuri ya Watu wa China. Katika mikesha  mbalimbali na misa takatifu, watu pia waliombea amani na kukusanya misaada kwa ajili ya watu waliokumbwa na tetemeko la ardhi katika majimbo ya Gansu na Qinghai. Askofu Giuseppe Shen Bin, Mjini Shanghai, katika mahubiri yaliyotolewa wakati wa mkesha wa Noeli, alikazia tafakari yake juu ya amani duniani na amani ya moyo wa kila mtu kama zawadi ya kumwomba Bwana Yesu siku ya kuzaliwa kwake.

Kila mtu akamilishe hija binafsi kwa kumwabudu mtoto Yesu

Katika shirika la Kipapa la Habari za Kimisionari Fides, linabainisha kuwa tarehe 25 Desemba, 2023 wakati wa misa takatifu, Askofu wa Shanghai aliwaalika kila mtu kukamilisha hija yake binafsi ya kumwabudu Mtoto Yesu na kufurahia zawadi ya wokovu ambayo ametuletea, ili furaha ya kila Mkristo iweze kuwa baraka kwa wengine katika maisha ya kila siku, katika familia na mahali pa kazi. Huko Beijing, iliyokumbwa na baridi kali, parokia 4 za kihistoria katikati mwa mji mkuu zimeanzisha huduma za muunganisho wa mtandao ili kuruhusu kila mtu - ikiwa ni pamoja na wagonjwa na wazee kufuata sherehe za kiliturujia kutokea nyumbani.

Ubatizo  watu wazima 23 na kipaimara watu 7

Katika majimbo ya Jiangxi, Hebei, Hubei, jumuiya kubwa za wafanyakazi wa Kikatoliki wahamiaji na pia wanafunzi wa kigeni walishiriki katika sherehe za jumuiya za wenyeji, kwa roho ya ushirika. Katika parokia ya Ximen (jimbo la Wenzhou) watu wazima 23 walibatizwa na 7 walipewa kipaimara. Mahali ambapo mapadre ni wachache, kama vile Daxunbao, jimbo la Sanyuan (jimbo la Shaanxi)- baadhi ya parokia zimeletewa maadhimisho ya mkesha wa Noeli ili kuwaruhusu walei kuleta ushirika kwa wazee na wagonjwa waliosalia na kulikuwa na baridi na hawakuweza kwenda kanisani. Hata majira ya baridi kali ya Inner Mongolia hayakuwazuia Wakatoliki kusherehekea Neoli  kwa furaha, wakiwaombea waathirika wa tetemeko la ardhi na amani ya ulimwengu.

Maadhimisho ya Noeli nchini China
29 December 2023, 12:22