Tafuta

Wafiadini wa wakati ule hadi leo wanandelea kushuhudia na kumwaga damu kwa ajili ya wokovu wa wengine. Wafiadini wa wakati ule hadi leo wanandelea kushuhudia na kumwaga damu kwa ajili ya wokovu wa wengine. 

Huendi Mbinguni peke yako.Maisha yaliyotolewa ya mashahidi wa imani kwa ajili ya wokovu

Kufuatia na Fides kuchapisha taarifa kuhusu wamisionari 20 waliouwa kwa mwaka 2023 unaomalizika,Mwandishi Gianni Valente anaeleza kuwa:“Vita vya ulimwengu mpya vinavyoendelea vinadai damu ya maskini,vinadai sadaka ya kibinadamu ya watu wengi wasio na hatia.Ni maisha ya wahudumu 20 wakichungaji waliouawa ambao walikutana na hatima ya ulimwengu.

Gianni Valente
Katika mwaka unaokwisha ni wamisionari ishirini wa Kikatoliki, wahudumu wa kike na kiume wakichungaji waliuawa. Na pia mwishoni mwa mwaka huu 2023, kama kila mwaka, Shirika la Habari za Kimisionari Fides limewakumbuka, huku likipendekeza tena historia yao na hali ya kifo chao cha umwagaji damu katika marejeo mafupi. Ni kitendo cha kawaida, kinachorudiwa kila wakati kwa mshangao lakini pia kwa shukrani na sio nje ya jukumu rasmi,  wala  nje ya mazoea. Kwa sababu historia zilizotajwa tena mwaka huu katika ripoti iliyohaririwa na Stefano Lodigiani kamwe haiwezi kutosha kwa sazabu haizoeleki. Mwaka huu pia, kama inavyotokea mara nyingi, wengi wao walipata kifo cha kikatili katika maisha yao ya kawaida, kilichofungamana na maisha ya wengine, katikati ya shughuli za kila siku. Katika vifo vingi vyao vya umwagaji damu, hatuwezi hata kutambua nia ya chuki za kidini. Mara nyingi wameuawa kwa ukatili usiochochewa, nyakati fulani kwa kupofushwa na pupa. Mwaka huu 2023 takwimu inaonesha orodha ya wamisionari waliouawa, labda zaidi kuliko katika hali nyingine za kihistoria. Kwani wengi wao waliuawa katika maeneo na hali zilizo na migogoro, na hivyo waliuawa na wanajeshi wa majeshi ya kawaida, wanamgambo wa magenge yenye silaha yasiyodhibitiwa na vikundi vya magaidi, na watu waliokuwa na bunduki katika maeneo yaliyotawanyika ya vita. Katika hali kama hii ya kuenea duniani kote kwa kansa ya ‘Vita Kuu ya Dunia tena vilivyomegeka vipande vipande’ ambayo huvujisha damu maisha ya watu wote, ambavyo Papa Francisko amekuwa akirudia katika majisterio yake.

Katika orodha ya wahudumu wa kichungaji waliouawa mwaka 2023, miongoni mwa wengine, kuna Padre Isaac Achi, aliyeuawa kwa moto wakati wa kushambuliwa na kundi lenye silaha kwenye parokia yake nchini Nigeria; kuna padri Moses Simukonde Sens, aliyeuawa kwa risasi iliyofyatuliwa na maajenti waliokuwa wakisimamia kituo cha ukaguzi cha kijeshi katika mji mkuu wa Burkina Faso; kuna Janine Arenas mwenye umri wa miaka 18 na Junrey Barbante mwenye umri wa miaka 24, wanafunzi wa Kifilipino walioshiriki katika shughuli za Kuhani wa chuo kikuu cha Chuo Kikuu cha Jimbo la Mindanao, waliouawa kwa bomu lililolipuliwa kwenye ukumbi wa mazoezi ya chuo kikuu, ambapo misa ilikuwa ikiadhimishwa; kuna Samar Kamal Anton, aliyeuawa pamoja na mama yake Nahida na mpiga risasi mkali wa jeshi la Israeli katika parokia ya Kikatoliki ya Familia Takatifu, huko Gaza. Kama kawaida, ushuhuda wa Kristo hutokea katikati ya mikasa na misiba ya wakati uliotolewa wa kihistoria. Inang'aa kwenye mandhari ya ulimwengu jinsi cheche zinavyoweza kuangaza kwenye uwanja wa mabua, “Tamquam scintillae in arundineto” ( Kitabu cha Hekima 3, 7 ).

Vita vya ulimwengu mpya vinavyoendelea vinadai damu ya maskini, vinadai sadaka ya kibinadamu ya watu wengi wasio na hatia. Na maisha duni yaliyovunjika ya wahudumu ishirini wakichungaji waliouawa mnamo 2023 ambao hukutana na hatima ya ulimwengu. Zinahusiana na uwezekano wa wokovu au laana inayoonekana kwenye upeo wa macho ya kila mtu. Damu yao inachanganyikana na maumivu ya kimya na yaliyokandamizwa ya waathriwa wengi wa sadaka katika vichinjio vipya vya historia. Mbele ya kukabiliwa na umati wa roho maskini zilizoangamizwa katika migogoro inayoikumba dunia, wamisionari ishirini na wachungaji waliouawa mwaka wa 2023 wanaonekana kuwa ukweli usio na maana. Na hali hii pia inafunua kitu kuhusu jinsi wokovu unaotangazwa katika Injili unavyotokea ulimwenguni. Katika fumbo la mapendo linalowaunganisha na Mateso na Ufufuko wa Kristo, mashahidi wa imani waliokufa mikononi mwa wengine pia wanashiriki katika maumivu ya Kristo mwenyewe kwa ajili ya wote wasio na hatia wanaoteseka isivyo haki, bila sababu.

Karama ya maisha yao inaakisi kujishusha kwake Kristo mwenyewe ili kujitwika huzuni, majeraha na matarajio ya wokovu wa kila kiumbe. Na inadhihirisha upendo wa Mungu kwa wote, ikikumbatia hata wale wasiojua jina la Kristo na hata maadui. Kwa sababu kila mwanadamu, aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu, bado anabaki kuwa "kaka au dada katika ubinadamu", kama Padre Christian de Chergé, Mtangulizi wa watawa wafia imani wa Tibhirine, alivyorudia. Kila ndugu au dada ni mtu ambaye Kristo alikufa na kufufuka kwa ajili yake. Kanisa la Roma, kwa mtazamo wa Jubile ijayo ya 2025, linajiandaa kuwakumbuka kwa shukrani pia, mashahidi wa imani waliotoa maisha yao kwa kumfuata Yesu. Kuomba na kusihi kwamba, katika fumbo la wokovu, utoaji wa maisha yao yenye baraka huzaa matunda ya uzima wa milele pia kwa umati wa watu leo waliokufa katika Mauaji mapya ya Wasio na Hatia.

Habari zinasema kwamba wakati wa mazishi ya Askofu Mkuu ambaye alitangazwa Mtakatifu, Oscar Romero, katika uwanja mbele ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Salvador, iliyojaa watu, mabomu yalianza kulipuka na risasi za kupotea zilipigwa. Maelfu walikimbilia katika Kanisa Kuu, na kulijaza hadi kukosa hewa, huku watawa wakisali sala za kifo cha furaha. Mwishowe, milima ya viatu, mifuko, glasi zilizopotea na wale waliokimbia kwa hofu, na miili arobaini isiyo na uhai, yenye damu na iliyovimba ilibaki kwenye Uwanja. Akikumbuka siku hiyo, Samuel Ruiz García (1924-2011), Askofu asiyesahaulika wa Mtakatifu Cristóbal de las Casas, huko Chiapas, alisema miaka ishirini baadaye, huko Mtakatifu Salvador kwamba: "Huendi mbinguni peke yako. Katika kwenda Mbinguni, Romero atakuwa amekwenda pamoja naye, kama kundi la wafiadini.”
 

30 December 2023, 11:57