Tafuta

Viongozi wa dini mbali mbali kutoka ulimwenguni waliudhuria COP28 kuanzia 30 Novemba hadi 12 Desemba,miongoni ni wawakilishi wa UISG. Viongozi wa dini mbali mbali kutoka ulimwenguni waliudhuria COP28 kuanzia 30 Novemba hadi 12 Desemba,miongoni ni wawakilishi wa UISG. 

Baada ya COP28,Watawa wa UISG watoa maoni:kuendeleza sauti ya mtandao wetu

Waliorejea kutoka COP28 ni Umoja wa Kimataifa wa Mama Wakuu wa Mashirika (UISG),Shirika mwamvuli wa watawa waliojitolea kukabiliana na changamoto za maendeleo ya kimataifa. Sr. Maamalifar Poreku,mratibu wa kampeni ya UISG ya Kupanda matumaini kwa sayari ametoa maoni yake kuwa wataendelea na kazi yao kufanya sauti za Jumuiya ya Mtandao wao kusikika.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kuunganisha hatua ya tabianchi na mbinu ya jumla ya kushughulikia upotevu wa bayoanuwai, uchafuzi wa mazingira na changamoto zingine za mazingira; kuunganisha huduma kwa mazingira na huduma kwa watu, kukataa maono ya kibanadamu ambayo yanasaidia tabia za matumizi ya uharibifu; kuunganisha matakwa ya walio hatarini zaidi ndani ya mifumo ya kitaasisi na uongozi, kuhakikisha kwamba sauti za wale walio katika mstari wa mbele kutokana na mabadiliko ya tabianchi ambayo yako katikati ya mjadala wa kimataifa. Haya ni mambo ya msingi ambayo Umoja wa Kimataifa wa  Mama wakuu(UISG) ambalo shirika linawaleta pamoja wanachama 1,903 wanaowakilisha zaidi ya watawa 600,000 duniani kote, liliongoza kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Wanachama COP28, kuhusu mabadiliko ya tabianchi, ambao ulihitimishwa tarehe 12 Desemba 2023 huko Dubai.

Vipaumbele vya maono ya UISG

Kwa mujibu wa Sr. Maamalifar Poreku, mratibu wa kampeni ya UISG iitwayo "Kupanda matumaini kwa sayari" alisema: “Hitimisho la COP28 linatuletea maswali tata, likionesha, kwa upande mmoja, upinzani mkali ambao nguvu za nishati ya mafuta zinapinga hatua zinazohitajika kukomesha uharibifu wa sayari yetu. Kwa upande mwingine, hata hivyo, majuma haya pia yameakisi nguvu, uwezo na azimio la mitandao iliyojitolea ulimwenguni kote kulinda na kuunda upya nyumba yetu ya pamoja.” Watawa hao wamejitolea  ulimwenguni kushughulikia changamoto za mazingira kwa vitendo na utetezi, wakiwa mstari wa mbele katika harakati linalotaka kuunda mazungumzo ya kimataifa kuhusu masuala ya maendeleo kuhusu mahitaji ya jumuiya za wenyeji. Mnamo Novemba 2022, kwa msaada kutoka kwa Mfuko wa Kimataifa wa Mshikamano, UISG walizindua Kampeni "Watawa kwa ajili ya  Mazingira: Kuunganisha Sauti kutoka Pembeni." Ni kampeni inayoelezea maono ya Watawa kwa ajili ya uongofu wa kiikolojia unaojikita katika imani. Taarifa hiyo ilieleza vipaumbele vilivyoongoza utetezi wa UISG kwa  mwaka 2023, ikiwa ni pamoja na mazungumzo yaliyoongozwa na Sr huyo kuhusu mazingira, kufanya meza za miduara ambazo UISG ilianzisha midahalo na mabalozi wa Nchi wanaowakilisha Nchi zao mjini Vatican na ushirikiano na washirika wapya na kufikia kilele cha uwakilishi wa kwanza wa UISG katika Mkutano wa COP.

Hitimisho la COP28 linatuletea maswali tata

“Kushiriki katika kilele cha mkutano wa COP kwa mara ya kwanza kulituwezesha kuelewa vyema jinsi midahalo ya kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi inavyofanya kazi, kusikiliza uzoefu wa makundi ya kidini ambayo tayari yanashiriki katika utetezi katika Umoja wa Mataifa, na kuchunguza mikakati iliyoratibiwa ya kupitisha na washirika wetu katika siku za usoni - alielezea Sr Maamalifar Poreku, mratibu wa kampeni ya UISG ya Kupanda matumaini kwa sayari. Kwa njia hiyo “hitimisho la COP28 linatuletea maswali tata: mkutano huo uliakisi upinzani thabiti na uliopangwa vyema ambapo nishati ya  mafuta na tasnia zingine za kimataifa zinapinga hatua zinazohitajika kukomesha uharibifu wa sayari yetu. Kwa upande mwingine, hata hivyo, majuma haya wameakisi nguvu, uwezo na azimio la mitandao iliyojitolea ulimwenguni kulinda na kuunda upya nyumba yetu ya pamoja".

Viongozi watafute suluhisho la mizozo

Mratibu huyo akifafanua zaidi alisema kuwa “Kwa mwaka 2024, kipaumbele cha UISG kitakuwa kutumia rasilimali zetu kwa njia madhubuti iwezekanavyo, kwa kuzingatia uharaka wa changamoto tunazokabiliana nazo. Lengo letu litakuwa katika ushiriki wa kimkakati katika maeneo ya utetezi wa kimataifa, kuimarisha mitandao ya mazingira katika ngazi ya kitaifa, na uingiliaji kati unaolengwa katika maeneo yenye maslahi maalum kama vile kilimo endelevu na viwanda vya madini.” Na zaidi mtawa huyo alisema: “Ili kushughulikia sababu kuu za mzozo huu wa wakati, lazima tuwahimize viongozi wetu kutafuta suluhisho kali kwa changamoto kali. Kama UISG, tumejitolea kutembea bega kwa bega na jumuiya zinazoishi pembezoni mwa dunia, ili kusonga pamoja kuelekea mustakabali salama, wa haki na amani kwa watu wote na sayari yetu takatifu" alimalizia kusimulia Sr. Maamalifar.

UISG ni mtandao Mkubwa wa kitawa wenye wawailishi laki sia Ulimwenguni

Ikumbukwe kuwa Umoja wa Kimataifa wa Wakuu Mkuu (UISG) ni shirika linalowakilisha zaidi ya watawa 600,000 duniani kote. Mtaguso mkuu wa pili wa Vatikani ulioanzishwa mwaka 1965, lengo lake ni kukuza ushirikiano wa kina kati ya makutano ya wanawake wakatoliki. Mbali na dhamira yake kuu ya mafunzo, usaidizi na uunganisho, UISG hufanya kama shirika mwamvuli kwa watawa waliojitolea kushughulikia baadhi ya changamoto kubwa zaidi za maendeleo ya wakati wetu.

UISG NA COP28 HUKO DUBAI
14 December 2023, 11:02