Seoul:Askofu Mkuu Chung aongoza misa ya Sikukuu ya Mama Yetu wa Guadalupe
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika maadhimisho ya ajabu ya umoja wa kiutamaduni na kidini, Kanisa Kuu la Myeongdong huko Seoul limeadhimishwa Misa ya uzinduzi wa kuadhimisha kwa mara ya kwanza Siku kuu ya Mama Yetu wa Guadalupe ambayo Mama Kanisa anafanya kila ifikapo tarehe 12 Desemba ya kila mwaka. Tukio hilo lililoongozwa na Askofu Mkuu Peter Soon-taick Chung, lilileta pamoja watu mbali mbali, akiwemohata Balozi wa Mexico nchini Korea, Carlos Peñafiel Soto, washiriki wa Wamisionari wa Guadalupe (M.G.), na takriban waamini Watu wa Mungu 300.
Askofu Mkuu atimiza ahadi
Mwanzo wa Misa Askofu Mkuu Chung alielezea juu ya ahadi ya mapema mwaka huu 2023, wakati wa ziara ya Balozi wa Mexico kwa Askofu Mkuu huyo. Balozi ni Mkatoliki mwenye bidii, ambaye alionesha nia yake ya kusherehekea Sikukuu ya Mama Yetu wa Guadalupe katika Kanisa Kuu la Myeongdong. Na kwa kujibu, ombi hilo Askofu Mkuu Chung alikuwa ameahidi kuongoza Misa hiyo binafsi. Na kuhusu Wamisionari wa Guadalupe, walikuwa muhimu katika kuandaa Misa hiyo. Utume huu wa kihistoria uliashiria uwepo wa kwanza wa Wamexico kwenye peninsula ya Korea na wamisionari wawili wa kwanza waliwasili Busan mnamo tarehe 27 Novemba 1962. Kuwasili kwao kulifungua njia ya mapadre zaidi kutoka Mexico katika miaka iliyofuata.
Tunapopambana Mama Yetu wa Guadalupe yupo nasi
Askofu Mkuu Peter Soon-taick Chung wakati wa mahubiri yake, alitoa maneno mazito akisisitiza umuhimu wa kina wa ujumbe wa Mama yetu wa Guadalupe kwa changamoto za kisasa zinazoikabili jamii. “Tunapopambana na matatizo kama vile kujiua, kutoa mimba, imani dhaifu, migogoro ya kijamii na mgogoro katika Peninsula ya Korea, ujumbe wa Mama Yetu wa Guadalupe unatuhusu sana,” alisisitiza. Matokeo ya Mama Yetu, kama yalivyosimuliwa na Askofu Mkuu Chung, yalitoa neema ya uponyaji na faraja kwa wengi, yakiimarisha jina lake kama mlinzi wa watoto ambao hawajazaliwa na Nyota ya Uinjilishaji Mpya. Pamoja na changamoto za kisasa, Askofu Mkuu Chung alisisitiza umuhimu wa kuomba maombezi ya Mama yetu wa Guadalupe.
Carlos Peñafiel Soto, Balozi wa Mexico nchini Korea
Baada ya Misa, naye Balozi Carlos Peñafiel Soto, alitoa shukrani, akimshukuru Askofu Mkuu Chung kwa kuheshimu ahadi ya awali na kutambua juhudi za Wamisionari wa Guadalupe. Katika taarifa yake ya dhati, Balozi Soto aliwasilisha furaha yake ya kusherehekea sikukuu hiyo huko Myeongdong na Kanisa la Korea, akitambua umuhimu wa maadhimisho hayo katika kuimarisha uhusiano wa kiutamaduni na kiroho kati ya Mexico na Korea Kusini.
"Sikukuu ya Mama Yetu wa Guadalupe katika Kanisa Kuu la Myeongdong inajikita kama ishara ya kuhuzunisha ya umoja, kubadilishana kiutamaduni na imani ya pamoja. Misa Takatifu ni mfano wa nguvu ya uhusiano wa kiutamaduni na uwezo wa sherehe za kidini kuvuka mipaka."