Tafuta

UISG na USG,Wakuu wa mashirika ya Kitawa kwa pamoja wameandaa warsha kuanzia 6/10 Novemba 2023 kuhusu ulinzi ndani ya mashirika. UISG na USG,Wakuu wa mashirika ya Kitawa kwa pamoja wameandaa warsha kuanzia 6/10 Novemba 2023 kuhusu ulinzi ndani ya mashirika. 

UISG na USG,waandaa Warsha kimataifa la kuunda utamaduni wa Ulinzi katika mashirika ya kitawa

Mpango huo unaoongozwa na mada “Kuunda Utamaduni wa Ulinzi”uliohamasishwa na Umoja wa Wakuu wa Mashirika ya kitawa ya Kimataifa UISG na USG utafanyika katika Nyumba ya"Fraterna Domus",Sacrofano nje kidogo ya Roma kuanzia tarehe 6 hadi 10 Novemba 2023,utaowaona washiriki zaidi ya 130 wa mataifa 39 tofauti.

Na Angella Rwezaula, Vatican

Katika Warsha iliyohamasishwa na Umoja wa Wakuu wa Mashirika ya kitawa kimataifa (USG-UISG), inaongozwa na kauli mbiu "Kuunda utamaduni wa ulinzi," ambapo itawaona washiriki 132, watakaombwa kujadili kwa pamoja, wakitoka katika mashirika 90 ya kitawa kama wawakilishi wa mataifa mbali mbali 39. Tukio hilo litafanyika katika Jumuiya ya "Fraterna Domus" ya Sacrofano, nje kidogo ya Roma, kuanzia tarehe 6 hadi 10 Novemba 2023 na litakuwa na lengo kuu la kuunda utamaduni wa ulinzi ndani ya  Mashirika ya Kitawa. Hii ni fursa isiyo na mfano kwa viongozi wa kidini na wahusika wa ulinzi kutoka duniani kote ili kujifunza, kubadilishana uzoefu na kushirikishana ili kuendeleza mazingira salama na jumuishi kwa waamini na watu wote watawa ambao ni watu wanaohudumia, hasa watoto na watu wazima walio katika mazingira hatarishi.

Mambo mengine ni pamoja na utamaduni wa kuzuia na kutoa taarifa

Katika Warsha hiyo kutakuwa na mambo matano muhimu ya kujadili: Kutoa mafunzo ya kina juu ya hatua za kuchukua ili kujenga utamaduni wa ulinzi kwa njia ya ulinzi na kuzuia; Kutoa taarifa za kina kuhusu unyanyasaji wa watoto wadogo na watu wazima walio katika mazingira magumu, wakiwemo waamini wa dini na vijana walio katika mafunzo; Kuwapatia walionusurika sauti kwa kuwaruhusu kushirikisha historia zao; Kuongeza maarifa juu ya mazoea ya kuzuia unyanyasaji, ikijumuisha mafunzo, uajiri na utekelezaji wa sera; Kuchunguza njia za kujibu matatizo, ikiwa ni pamoja na kushughulikia shutuma, jukumu la sheria ya kiraia na kanuni, kutunza watu walioathiriwa na unyanyasaji, na kuwasiliana vyema na wengine.

Warsha inawakilisha fursa ya kujifunza kutengeneza mazingira salama

Watakaowezesha warsha hiyo, watakuwa na watu mashuhuri wa kimataifa katika ulinzi na kuzuia unyanyasaji, wakiwemo Ndugu Brendan Geary, Sr.  Maria Rosaura González Casas, Padre Tim Brennan, Tina Campbell, na Sr. Tiziana Merletti. Kwa upande wa waandaaji, kuhusu warsha hiyo Ndugu Emili Turú, Katibu Mkuu wa USG, na mratibu mwenza wa tukio alisema kuwa “Hali za unyanyasaji ni tatizo kubwa ambalo lazima tushughulikie, na warsha hii inawakilisha fursa ya kujifunza jinsi ya kutengeneza mazingira salama kwa washiriki wa mashirika yetu na watu tunaowahudumia.” Kwa upande wake Sr. Mary John Kudiyiruppil, katibu Msaidizi wa UISG, alisema: "Tunafurahi kuona kwamba watu wengi kutoka ulimwenguni kote wameamua kuungana nasi katika tukio hili muhimu."

Kwa maelezao zaidi usisite...

Kwa hiyo kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na ofisi ya Mawasiliano ya UISG: comunicazione@uisg.org ;WhatsApp +39 349 935 87 44 na kutaka kujua mengine zaidi au mikutano ambayo tayari imekwisha fanyika unaweza kubonyeza linki hii:www.uisg.org

03 November 2023, 17:49