Togo,Askofu Alowonou,msalaba wetu ni silaha dhidi ya magaidi!
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Leo hii tunamshukuru Bwana kwa miito mingi ya kipadre, kimisionari na kitawa tuliyo nayo. Katika hali hii ya Neema, hata hivyo, tuna tatizo la kuhakikisha mafunzo ya mapadre wa baadaye na wa kitawa. Elimu sio tu kutokana na mtazamo wa kitaalimungu na kimafundisho bali pia kutoka kwa jamii. Haya yameelezwa na Askofu Benoît Comlan Messan Alowonou, wa Jimbo katoliki la Kpalimé na rais wa Baraza la Maaskofu nchini Togo, akihojiana na Shirika la Kipapa la Habari za Kimisionari Fides kuhusiana na utume wa chi hiyo ambayo ni moja ya nchi zanazolengwa mara kwa mara na makundi ya magaidi.
Hata hivyo Maaskofu hawa hivi karibuni mwishoni mwa Oktoba 2023 walikuwa katika ziara yao ya kitume mjini Vatican, ambao kama kawaida ya ziara hii ya kitume maaskofu hao walipata fursa ya kutembelea baadhi ya Mabaraza ya Kipapa ili kujua shughuli zao na hatimaye kukutana na Baba Mtakatifu.Kwa njia hiyo, Shirika la habari Fides linabainisha kwamba Kanisa la Togo lilizaliwa kutokana na juhudi za wamisionari kutoka nchi mbili kati ya Ujerumani na Ufaransa ya Jamhuri ya Tatu, kufuatia matukio ya kihistoria ya Ulaya na makoloni yake ya Afrika mwanzoni mwa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Na kwa msingi hiyo, ndipo lilianza swali ka kwanza katika mahojiano Askofu wa Kpalimé.
Togo, koloni la Ujerumani hadi Vita vya Kwanza vya Dunia, iliwekwa chini ya mamlaka ya Ufaransa na Umoja wa Mataifa wa wakati huo. Je, ukweli huu wa kihistoria umekuwa na athari kwa maisha ya Kanisa mahalia?
Kanisa la Togo lina historia ya kipekee, kwa sababu lilianzishwa na wamisionari wa Kijerumani wa Verbiti, lakini kutokana na Vita vya Kwanza vya Kidunia hao wa mwisho walilazimika kuondoka nchini. Baadaye, wamisionari wa Ufaransa waliokuwa wa Jumuiya ya Utume wa Afrika (SMA) walifika. Katika kipindi cha kati ya kuondoka kwa wamisionari wa Ujerumani na kuwasili kwa Wafaransa, jumuiya ya Kikatoliki iliachwa bila mapadre. Hata hivyo, Waverbiti walikuwa na makatekista waliofunzwa. Nao ndio walioshika nuru ya imani kabla ya kuwasili kwa wamisionari wa SMA.
Kwa hiyo ni urithi muhimu. Je, hali ya Kanisa nchini Togo ikoje kwa sasa?
Leo hii tunamshukuru Bwana kwa miito mingi ya kipadre, kimisionari na kitawa tuliyo nayo. Katika hali hii ya Neema, hata hivyo, tuna tatizo la kuhakikisha mafunzo ya mapadre wa baadaye na wa kitawa. Elimu sio tu kutoka kwa mtazamo wa kitaalimungu na kimafundisho bali pia kutoka katika jamii. Hata katika Afrika tunasikia swali la uhusiano kati ya Kanisa na jumuiya ya kiraia ambayo inazidi kubadilika. Kuhusiana na hilo, majuma ya hivi karibuni yameshuhudia kuchapishwa kwa Biblia katika lugha ya Ewé. Lugha ya Ewé imepokea kutambuliwa kama lugha rasmi ya Kanisa na Barza la Kipapa la Uinjilishaji na hivyo tumetafsiri Biblia nzima katika lugha hiyo. Kufikia sasa tulikuwa tunatumia maandishi ya Biblia yaliyotafsiriwa katika lugha ya Ewé na ndugu zetu wa Kanisa la Kipresbyterian.
Hata nchini Togo shinikizo linalotolewa na makundi ya kigaidi kutoka Burkina Faso linaonekana. Je, una wasiwasi kuhusu tishio hili?
Lazima niseme kwamba tuna wasiwasi kwa sababu magaidi wamekuwa mlangoni mwa Togo kwa miaka kadhaa sasa. Lakini kwa vyovyote vile tunahifadhi imani na tumaini na zaidi ya yote msalaba ambao ndio “silaha yetu ya upendo”. Ninapenda pia kuwashukuru Caritas ambao walikuja kusaidia kaka na dada zetu wa ukanda wa Sahel kaskazini ambao wanakabiliwa na ukosefu wa utulivu unaosababishwa na magaidi hawa kwa mpango wa hivi karibuni kutuliza eneo la mpaka na Burkina Faso na Benin.