Tafuta

Wapalestia wakiwa wanahama kutafuta eneo salama Wapalestia wakiwa wanahama kutafuta eneo salama 

Tamko la maaskofu wa Australia Uyahudi,Ukristo na Uislamu unashiriki shauku ya amani

Baraza la Maaskofu nchini Australia wakiwa katika Mkutano wao Juma hili wametoa tamko lao la pamoja kuhusiana na Nchi Takatifu wakiwa wanaomba amani idumu.Hii siyo historia za habari tu au janga za televisheni badala yake ni historia za watu halisi.Wote ni watoto wa Mungu. wanawaombea pia msaada.

Na Angella Rwezaula, Vatican.

Kuombea amani idumu ndiyo kichwa cha tamko kutoka kwa Maaskofu Katoliki wa Australia, Ijumaa tarehe 10 Novemba 2023  wakati wakiwa kwenye Mkutano wao Juma hili wameungana wote  na jumuiya Kikatoliki ya Australia katika kueleza huzuni na uchungu wao juu ya mateso ya watu wa  Nchi Takatifu. Kwa mujibu wa taarifa yao wanabainisha kuwa hii siyo historia za habari tu au janga  za televisheni badala yake ni historia  za watu halisi. Wote ni watoto wa Mungu. Kwa hiyo wanawaombea kaka na dada zetu katika Nchi Takatifu na kuwaweka pamoja na mateso yao mioyoni mwao. Kukumbuka historia ndefu ambayo imesababisha ghasia za sasa katika Mashariki ya Kati ni hatua ya kwanza ya kutafuta njia zaidi ya ghasia hadi mwisho wa mzozo huo. Kwa njia hiyo amani inawezekana tu kutoka atika  haki. Maakofu wa Australia: Tunawalika watu wenye imani kuomba pamoja nasi kwa ajili ya amani ya kudumu na ushindi wa hadhi ya mwanadamu.

Maaskofu wa Australia wanaomba msaada na ukarimu wa mahitaji

Maaskofu wa Australia aidha amebanisha kuwa, Tunapomgeukia Mungu katika sala, tunahimiza pia matendo ya upendo na ukarimu ili kuwaandalia mahitaji ya kimwili watu waliotengwa na wanaokabili dhiki kubwa zaidi. Hitaji ni la haraka. Misaada inayosimamiwa ipasavyo inaweza kumaanisha tofauti kati ya maisha na kifo kwa raia wasio na hatia, na kwa hivyo tunatoa wito wa upatikanaji wa haraka kwa mashirika ya kibinadamu. Vile vila Baraza la Maaskofu Katoliki  nchini Australia katika tamko hilo wanabainisha kuwa Maandiko Matakatifu ya Uyahudi, Ukristo na Uislamu yanashiriki shauku ya amani na maelewano, na hii tunatafuta pamoja kama familia moja ya kibinadamu.

10 November 2023, 17:40