Tafuta

Hii ni nguo ya Kifransiskani. Hii ni nguo ya Kifransiskani. 

Je unajua vema Shirika la Wafransikani wasekulari (OFS)?

Shirika la Wafransiskani Wasekulari(OFS),kilatini(Ordo Franciscanus Saecularis)linajumuisha watu wacha Mungu,wanaume na wanawake.Hawa ni wanachama ambao hawaishi katika jumuiya,lakini wanaishi maisha yao ya kila siku katika ulimwengu na ambao,hukusanyika pamoja katika jumuiya mara kwa mara kusali na mikutano.

Na Angella Rwezaula, Vatican.

Kwa walio wengi, utasikia wamekuwa wakijiuliza tunasikia salamu isemayo  Amani na Salama, au Peace and Good, lakini hatujuhi jinsi gani ya kujibu au wengine wanasema wale wamevaa Tau aina ya msalaba tofauti na misalaba mingine tuliyozoea ndiyo wa amani na salama. Ndiyo Amani na Salama ni Salamu kweli ya Kifransiskani, inaashiria kweli na kielelzo cha kutaka Amani. Fikiria katika ulimwengu ulimomolewa na kinzani, vita, migogoro ya kisiasa, umaskini na mwengine, hakika kusikia neno Amani na salama hasa itokayo rohoni, inajieleza yenyewe, ile shauku ya amani ambayo Bwana wa Amani anataka kuiminina ndani ya mioyo ya kila mwanadamu.  Lakini basi na wengine utasikia, baada ya kusika salamu hiyo wakidai labda ni harakati ya Kanisa ambayo imezaliwa hivi karibuni. Ni mitazamo tofauti sana ambayo katika Nchi hasa za Uinjilishaji kwa wastani hawajuhi ni nini maana ya ke na hasa kwa mashirika yote kwa ujumla nikianzia na WAFRANSISKANI WASEKULARI (OFS) ambao leo hii kwa hakika ninataka kujadili katika makala hii.

Jumuiya katika Kanisa Katoliki

Ndugu msomaji wa kamala hii tutambue hata hivyo kwamba katika Kanisa Katoliki licha ya jumuiya nyingi zilizop kuna hata  jumuiya za maisha ya kawaida, zilizoidhinishwa na Mamlaka Kuu ya kikanisa, ambazo washiriki wake wanaelekea kwenye ukamilifu wa Kiinjili kwa kuweka nadhiri tatu za hadhara, za kudumu na za dhati, za umaskini, usafi wa moyo na utii, kwa mujibu wa kanuni maalum kwa kila mmoja wa Shirika.. Na wakati huo huo, kuna hata baadhi ya mashirika ambayo wanaongeza hata nadhiri ningine tofauti za zile za kiinjili, kulingana na mwanzilishi wa Shirika husika kutoka kukazia maana ya utume huo. Si lazima kwa washiriki wote kuweka nadhiri nzito, ali mradi baadhi yao, kwa mfano,  wa makuhani wa majimbo, tofauti na Makuhani wa Mashirika. Kwa hiyo suala la mashirika kwa ujumla nitalijadili katika makala nyingine, lakini leo hii nitataka kukuuliza  na kufanua kama Je,  unajua nini maana ya Shirika la Kifransiskani la Kisekulari kwa kifupi (OFS,) kwa Kiingereza:The Third Order Secular au (Ordo Franciscanus Saecularis, kwa kilatini?

Awali ya yote OFS yaani Shirika la Kifransiskani la Kisekulari (O.F.S.), ambalo hadi mnamo mwaka 1978 liliitwa Shirika la Tatu la Wafransiskani (T.O.F.) ni mojawapo ya vipengele vitatu  msingi vya Familia kuu ya Wafransiskani inayoundwa na Mashirika Matatu ambayo kwa hakika yaliundwa na Mtakatifu Fransis wa Assisi. Hayo ni: Shirika la Kwanza la (mafrateri yaani Ndugu Wadogo kwa kifupi OFM, 1209), Shirika la Pili ni (Waklara Maskini walioitwa hivyo kwa sababu walianzishwa pamoja na Mtakatifu Clara 1212) na  ndipo tunakuja katika Shirika la tatu kifupi  T.O.F hapo zamani(1221) ambalo kwa karne nyingi lilijulikana la kisekulari, yaani la kidunia na mitindo mingine mingi ya wanaume na wanawake wa kidini waliojishughulisha na shughuli za kitume au hata watawa wa ndani peke yao ambao waliundwa kutokana na safu hiyo kuu ya kisekulari au kutoka katika ulimwengu). Tunaye Mtakatifu Elizabeti wa Hungaria ambaye kumbukizi yake ni tarehe 17 Novemba na watakatifu wengi sana walei, kwa kutaja mmoja tu. Kwa njia hiyo ni kuanzia na Wakristo walei ambao, kwa wito maalum, wanajitolea kuishi Injili kwa namna ya Mtakatifu Fransis wa Asssi, katika hali ya kidunia ya mtu alivyo, akizingatia Kanuni maalum iliyoidhinishwa na Kanisa. 

OFS linamshukuhudia mambo yajayo:upendo kwa maskini,utii na usafi wa moyo

Ni wito hasa unaotofautisha, kutoka katika mtazamo wa motisha, kuwa sehemu ya Shirika la Wafransiskani Wasekulari(OFS)ukilinganishwa na vyama vingine vya wachamungu ambavyo ni vingi sana Ulimwenguni. Wafransiskani wa Kisekulari, wakiweka nadhiri zao baada ya muda wa mafunzo na masomo ya kiroho na kiutamaduni, wanajitolea kuishi wito huo katika kila hali ambayo wanajikuta katika ngazi ya kifamilia na kazi. Kaka na dada wa Shirika la Kifransisko la kisekulari wanatafuta mtu aliye hai na mtenda kazi wa Kristo ndani ya ndugu zao wengine, katika Kanisa, katika Neno la Mungu na katika liturujia. Wanamtangaza Kristo kwa njia ya maisha na neno; wanashuhudia mambo yajayo katika maisha ya kila siku kuanzia na  kupenda umaskini na waliobaguliwa, katika utii, na katika usafi wa moyo. Wafransiskani Wasekulari (OFS)wamejizatiti katika kujenga ulimwengu wa haki zaidi, wa Kiinjili na kidugu kwa kuwakaribisha watu wote kama zawadi kutoka kwa  Mwenyezi Mungu, kwa furaha ya kuwa katika usawa na wanyonge zaidi na dhaifu huku wakiendeleza haki. Aidha OFS Wanaishi roho ya Mtakatifu Francis wa Assisi  katika kazi zao na katika familia zao, katika safari ya ukomavu wa kibinadamu na wa Kikristo pamoja na watoto wao. Wao wana amani, wanamtumaini mwanadamu na kumletea ujumbe wa furaha na matumaini.

Muujiza wa Mbayuwayu

Kwa kuzaliwa kwa Wasekulari Wafransiskani ambapo leo hii kwa hakika ni Shirika la Wafransiskani la Kisekulari, OFS lililitaabika sana na halikukosa au karibu kutaka kupoteza kati ya vyanzo na nyaraka nyingi za kihistoria, zilizoandikwa katika zama tofauti na mara nyingi  zilitaka kupingana. Na si hivyo, watu wengu kutokurlewa maana ya Ufransiskani Sekulari. Zaidi hasa ni pale  ambapo, swali linakuja la mahali ambapo mwanzo wake  uliliundwa ambao kwa kiasi fulani ilikuwa ikibishaniwa na mara  nyingi iliunganishwa na usomaji usio sahihi au hata maandishi yaliyoandikwa kwa mkono kwa karne nyingi,  yakibadilishwa kwa hiari asili ya mahali. Lakini kiukweli, kulingana na tafsiri moja, ambayo inahusisha kuzaliwa kwa Shirika la  Tatu la Wafransiskani linahusishwa na muujiza wa "ukimya wa mbayuwayu", ambao inawezekana kufikiwa kutoka katika maandishi ya mwandishi wa wasifu wa kwanza wa Kifransiskani wa, ndugu Mdogo  Tommaso wa Celano, kwamba kwa upande wa Mtakatifu Francisko wa kuunda shirika hili ulitolewa mnamo mwaka 1212 huko Alviano, kijiji cha kupendeza kati ya Orte na Orvieto, si mbali na Todi nchini Italia.  Na ufafanuzi sawa uliweza kufanywa katika Maandiko makuu (Legenda Maior) ya Mtakatifu Bonaventure.

Wafransiskani wa kwanza  wa OFS

Wafransiskani wa kwanza walei kwa kawaida wanaaminika kuwa wenyeheri Lucchese na Buonadonna wa Poggibonsi, walioishi wakati wa Mtakatifu Francis. Hasa kwa kurejea uongofu wa mfanyabiashara Lucchese na nguo ya  toba ambayo, pamoja na mke wake, alipokea kutoka kwa Mtakatifu Francis, wengine wanatambua kuzaliwa kwa Shirika la Tatu la Wafransisko huko Poggibonsi, mji wa Tuscana, kati ya  mwaka 1209 na 1211 na kwa hali yoyote sio zaidi ya 1214. Leo hii wasomi wengi zaidi wanathibitisha kusimikwa rasimi kwa Shirika la Tatu la Wafransiskani (OFS) na Papa Nicholas IV, aliyekuwa Papa wa kwanza katika historia Ndugu Mdogo (OFM); aliyenzisha  wa udugu wa walei, wakiutambua na kuuwasilisha kwa utaratibu wa mapadri wadogo, na na hati ya mnamo 1289. Kusudi la  Papa Nicholas IV lilikuwa kuweka harakati hizi za walei waliozaliwa katika Ukristo, lakini ambazo zilikua sambamba na Kanisa na sio ndani ya Kanisa. Kanisa, chini ya udhibiti. Kama vile mapapa waliotangulia, wana wa wa Mageuzi ya  Kanisa katika karne ya 11-13, waliwekwa chini ya udhibiti na kuingiza harakati za wahubiri (Wadominikani) na Ndugu Wadogo Wafransiskani(OMF), wakitofautisha badala yake na harakati  nyingine  ambazo hazikutambua utawala wa Kanisa la Roma katika mambo ya imani.

Watakatifu na Wenyeheri  Wafransiskani

Baada ya Mwenyeheri Lucchese na Mwenyeheri Buonadonna, kuna Mtakatifu Elizabeth wa Hungaria, Mtakatifu Rose wa Viterbo, Mtakatifu Ferdinand III wa Castile, Mtakatifu Louis IX, Mfalme wa Ufaransa, Mwenyeheri Yolanda wa Poland, Mwenyeheri Salomea wa Krakow, Malkia wa Hungaria.  Mtakatifu Margaret wa Cortona, Mtakatifu Ivo wa Kermartin, Mtakatifu Amato Ronconi, Mtakatifu Angela wa Foligno, Mwenyeheri Ludovica Albertoni, Mwenyeheri Raymond Llull, Mtakatifu Elzeario da Sabrano, Mwenyeheri Maria Barba, Mtakatifu Rocco, Mtakatifu Elizabeth wa Ureno, Mtakatifu Corrado Confalonieri, Mwenyeheri Michelina wa  Pesaro, Mtakatifu Bridget wa Uswiss, Mwenyeheri Francesco Faà di Bruno, Mwenyeheri Eurosia Fabris Barban, Mwenyeheri Paola Gambara Costa, Mtakatifu Thomas More, Mtakatifu Angela Merici, Mtakatifu Charles Borromeo,

Orodha ya Wakatifu wafransikani inaendelea, Mtakatifu Giovanna Francesca wa Chantal, Mtakatifu Peter Betancur, Mtakatifu Maria Frances wa Majeraha Matano, Mtakatifu Giuseppe Benedikto Cottolengo, Mtakatifu Vincenza Gerosa, Mtakatifu Vincenzo Pallotti, Mwenyeheri Contardo Ferrini, Mwenyeheri Giuseppe Tovini, Mwenyeheri Giovanni Pelingotto, Mwenyeheri Sazias Ferigiovanni Matiti Feli De, Mwenyeheri Pier Pettinaio, Mwenyeheri Catherine Malkia wa Bosnia, Mwenyeheri Margaret Bays, Mtakatifu Yohane Maria Vianney, Mwenyeheri Papa Pio IX, Mtakatifu Joseph Cafasso, Mtakatifu Yohane  Bosco, Mtakatifu Louis Guanella, Mtakatifu Leonard Murialdo, Mtakatifu Louis Orione, Mwenyeheri Andrea Carlo Ferrari, Mwenyeheri Francesco Jägerstätter, Mwenyeheri Edvige Carboni, Mtakatifu Yohane XXIII, Mwenyeheri Luigi Beltrame Quattrocchi na Maria Corsini, Mwenyeheri Giovanni Saziari, Mwenyeheri Giuseppe Toniolo, Mtakatifu Malaika Mkuu Tadini, Mwenyeheri Elisabeth  Sanna, Mwenyeheri Armida Barelli na wengine wengi.

Watumishi wa Mungu Wafransiskani

Giacomo Gaglione, Teresa Gardi, Paolo Pio Perazzo, Lucia Bocchino, Maria Clotilde wa Bourbon, Malkia wa Sardegna, Giuseppe Morgera, Egidio Bullesi, Robert Schuman, Leone Dehon, Ludovico Necchi, Francesca Caterina wa Savoy, Maria Apollonia Concetta Bertoli, Genoveffa de Troia, Papa Pio XII, Carlo Tancredi Falletti na Juliette Colbert, marquises wa Barolo, Giorgio La Pira, Ludovico Coccapani, Don Tonino Bello (Askofu ) na wengine wengi tu.

Wengine

Ndugu msomaji wa makaka hii, Watu wengine wengi mashuhuri walijiunga na Shirika la  Tatu la Wafransiskani Wasekulari ambamo kati yao pia kuna  Antonello wa Messina anayejulikana zaidi, Dante Alighieri, Christopher Columbus, Vasco da Gama, Michelangelo, Raphael, Giotto (ambaye aliwaita watoto wake majina ya Mtakatifu), Francesco Petrarca, Ulf Gudmarsson mume wa Mtakatifu Brigida, Silvio Pellico, Franz Liszt, Cola di Rienzo, Giuliano Antoniotto Adorno mume wa Mtakatifu Catherine wa Genova, Battista Sforza, Lucrezia Borgia, Amerigo Vespucci, Giovanni Pierluigi wa Palestrina, Miguel de Cervantes, Lope de Agi Galvani, Lu Volta, Ettore Thesorieri, André-Marie Ampère, Gabriel García Moreno, Georgiana Fullerton, Henry Edward Manning, Charles Gounod, Louis Pasteur, Coventry Patmore, Papa Leo XIII, Papa Benedikto XV, Papa Pio  Savoia, Herbert Vaughan, Mario Fani, Elizabeth Herbert, Tomás Mac Curtain, Terence MacSwiney, John Michael Talbot, Giovanni Papini, Giosuè Borsi, Giuseppe Dossetti, Frido von Senger und Etterlin, na Remo Vigorelli. I

Idadi ni kubwa ya Wafransiskani na wewe jiunge!

Idadi ya Wafransiskani ni kubwa kuimaliza lakini angalau unapata mwanga wa kujua jinsi ambavyo ni watu wengi ambao kwa karne zote wamejiunga na Ufransinsiskani. Na labda unaposoma kama haukuwa na Shirika lolote lile, au harakati na chaka cha kitume  inawezekana kuwa na hamu ya kwenda katika kituo chochote cha Wamisionari Wafranciskani, wawe Ndugu Wadogo(OFM), Ndugu Wadogo OFM Capuccini, Ndugu Wadogo OFM Wakomventuali ili wakuelezee mchakato wa kujiunga na Shirika la Wafransiskani Wasekolari (OFS).

 

17 November 2023, 12:41