Tafuta

Askofu Mkuu Martinelli huko Abu Dhabi. Askofu Mkuu Martinelli huko Abu Dhabi. 

Papa huko Dubai,Martinelli:ishara ya kujitolea kwa Kanisa katika

Siku chache kabla ya kufunguliwa kwa Mkutano mpya wa Nchi Wanachama wa COP28 na kuwasili kwa Papa Francisko katika mji mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu,Vatican News imefanya mahojiano na Msimamizi wa kitume wa Kusini mwa Arabia:“Papa ameamua kushiriki pamoja na Wakuu wa Mataifa duniani kuelezea wasiwasi wote kwa ulimwengu ulio katika shida kubwa.

Na Federico Piana na Angella Rwezaula – Vatican.

Zimebaki siku chache kabisa ambazo katika wakati huu Baba Mtakatifu anajiandaa ufanya ziara fupi. Kwa njia hiyo, "Tutamsindikiza Papa kwa sala ili mkutano huu na wakuu wa nchi juu ya mada muhimu ya mabadiliko ya tabianchi uweze kufikia malengo yote yaliyowekwa." Alisema hayo Askofu Mkuu Paolo Martinelli, Balozi wa  kitume wa Kusini mwa Arabia, akionesha furaha katika  ziara hiyo  ijayo ya Papa Francisko kwenda huko Dubai, kwenye mwaliko wa kuzungumza kwenye COP28 ambayo itafunguliwa rasmi tarehe 30 Novemba na utahitimishwa mnamo tarehe 12 Desemba 2023.

Mara ya kwanza kwa Papa

Papa Francisko - ambaye atawasili katika jiji la Umoja wa Falme za Kiarabu jioni ya tarehe 1 Desemba 2023, na atakayerudi mjini Vatican alasiri ya tarehe 3 Desemba ndiye atakuwa Papa wa kwanza kuwahi kushiriki katika aina ya Mkutano mpya wa Vyama ulioitishwa na Umoja wa Mataifa ambapo wakuu wa dunia wanapaswa kuchukua hatua muhimu juu ya upunguzaji wa gesi chafuzi na maendeleo ya nishati mbadala. "Inaonekana kuvutia sana kwangu kwamba Papa ameamua kushiriki katika tukio hili kwa wakati wa kushangaza ya hali ya Tabianchi  ya sayari yetu na umakini na wasiwasi wote wa Kanisa", alisema Askofu Mkuu Martinelli.

Eneo la Mkutano wa COP28

Mahali ambapo COP28 itafanyikia, kwa hakika kuna  maana nyingi, kambapo Papa pia alikuwa amekumbusha hilo katika wito wake mpya wa Waraka wa  kitume  wa Laudate Deum kuhusu mgogoro wa Tabia nchi. Na kwa hiyo mkutano utafanyika katika moja ya maeneo ya Waajemi. Ghuba ambayo anahisi uharaka wa mabadiliko ya kiikolojia inazidi kukua. Haja ya mabadiliko katika mtindo wa maisha ambayo pia hujirudia katika maisha ya Kanisa.

Kanisa liko mstari wa mbele

Kwa miaka mingi, miito ya  Papa Francisko kuhusu ulinzi na utunzaji wa Common Home yaani Nyumba yetu ya Pamoja zimefafanuliwa kwa kina katika Vicariate yote, ambayo ina mamlaka juu ya Wakatoliki wanaoishi sio tu katika Umoja wa Falme za Kiarabu bali pia  hata huko Oman na Yemen, na zaidi ya milioni moja wamebatizwa. "Sisi tunatumia waraka wa Laudato Si' ndani ya mafunzo ya  katekesi tunayofanya hasa na vijana ambao ni nyeti sana kwa masuala haya, kwa ikolojia fungamani kweli". Kimsingi, tangazo la Injili pia linakuja kupungua kama jukumu la kazi ya Uumbaji"alieleza Askofu Mkuu Martinelli kwa undani.

Ziara inayoungwa mkono na sala

Hata kama haitakuwa ziara  ambayo Papa atakutana na Kanisa la mahali hapo, kama ilivyokuwa katika ziara ya 2019 katika mji mkuu, Abu Dhabi, Askofu Mkuu Martinelli ameonesha nia ya kusema kwama waamini wote wa Vicariate wamependezwa na hilo tangu mwanzo  wa tukio la ajabu. "Mimi pia niliandika barua iliyoelekezwa kwa waamini ambapo nilisisitiza umuhimu wa ushiriki wa Papa Francisko katika COP28, nikimwomba kila mtu kusindikiza uwepo wa Papa kwa sala zetu za kibinafsi".  

 

28 November 2023, 14:23