Tafuta

Hali ya Maisha nchini Niger bado ni ngumu. Hali ya Maisha nchini Niger bado ni ngumu.  (AFP or licensors)

Niger:Jumuiya ndogo karibu na maskini licha ya kutawaliwa na serikali ya kijeshi

Jumuiya Ndogo Ndogo za kikristo nchini Niger ziko karibu na maskini bila kelele licha ya kutawaliwa na serikali ya kijeshi yapita miezi mitatu sasa.Hali ni ngumu ya maisha kwa sababu hakuna hata njia ya kutoka.Bidhaa msingi hazipatikani na watumishi wa umma hawana mishahara.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Mmisionari katika Jumuiya ndogo ya Kikristo  ya Dosso, kilomita 150 kutoka mji mkuu Niamey, Padre Rafael Casamayor, akizungumza na Shirika la Kipapa la Habari za Kimisionari Fides kuhusiana na hali nchini Niger alisema kuwa baada ya miezi mitatu ya serikali ya kijeshi  nchini humo hakuna njia hata ya kutoka. Tunaendelea kukumbana na hali ngumu nchini kote. Hali inaonekana kuwa mbaya zaidi kwa sababu hadi sasa hakuna suluhisho ambalo limejaribiwa au kupendekezwa, ama katika ngazi ya kiuchumi au kisiasa. Tangu mapinduzi ya mwezi Julai,  nchi imebaki kupooza, hata watumishi wa umma hawapati mishahara, bei za bidhaa za msingi zikiwemo dawa zinaendelea kupanda au kukosa kabisa – aliongeza Padre huyo wa Jumuiya ya Utume wa Kimisionari wa Afrika, mmisionari katika jumuiya ndogo tangu 2021.

Ongezeko la kufunga ndoa ndani ya Kanisa

Padre Rafael amezungumzia jinsi ambavyo matatizo ya jumla yameathiri pia mwanzo wa mwaka huu 2023/2024 wa kichungaji na katika ugumu huo, ameeleza kwamba  hata hivyo ameona umoja na mshikamano mkubwa zaidi katika jumuiya ya Kikristo anamofanyia kazi. "Katika kipindi cha miezi mitatu au minne iliyopita kumekuwa na wanandoa watano vijana waliofunga ndoa ndani ya Kanisa, idadi ya wakatekumeni imeongezeka zaidi kidogo na kuna hali inayoonekana kuwa ya kidugu na tulivu." Akiendelea na maelezo yake Padre Rafael alisema kuwa "Katika majuma ya mwisho ya Oktoba, pamoja na jumuiya zetu kuu tulisambaza chakula katika vitongoji tofauti vya jiji, katika maeneo ya mbali zaidi, kwa familia maskini zaidi ambapo wanashangaa jinsi inawezekana kuishi hivi katika vibanda vya watu wanane tu au mita kumi iliyosongamana yote pamoja. ‘Na mvua inaponyesha, wanakwenda wapi?’ na mwanasemina kutoka Benin ambaye alishiriki katika mpango huu pamoja nasi aliniuliza swali hilo. Hii ni kwa sababu aliongeza kwamba Hajawahi kuona umaskini kama huu na  kwamba: 'Ni mara ya kwanza kushiriki katika ugawaji wa chakula kwa maskini zaidi na kutafakari hali ya hatari sana ya hawa ndugu moyo wangu umevunjika'.

Ishara ya Mshikamano kwa waio na uwezo

Padre Rafael Casamayour alisema, "Kilichofanya ishara hii ya mshikamano kwa ndugu wasio na uwezo iwezekane ni roho ya udugu iliyoanzishwa kati ya watu kutoka tamaduni, nafasi, ardhi na ulimwengu tofauti", alisisitiza Padre. "Jumuiya ndogo ndogo za vitongoji mbalimbali hukusanya marejeo kutoka kwa watu wengi,  familia zenye uhitaji na usiku, kwa njia ya busara zaidi, wanaendelea kusambaza magunia ya mchele na pesa kwa ajili ya mboga. Diwani wa kijiji alitupongeza kwa mpango huo, lakini juu ya yote kwa njia iliyohifadhiwa na ya unyenyekevu ambayo tunasaidia maskini zaidi, bila kelele." Padre Rafael alihitimisha ushuhuda wake kwa kuongeza maelezo juu ya mipango zaidi wanayofanya. "Baada ya kusanyiko letu la hivi karibuni jimboni huko Niamey tunapanga kozi kwa vikundi mbalimbali vya vijana ikiwa ni pamoja na: utamaduni wa songhay-djerma, caritas -usaidizi kwa wagonjwa, shule ya sala, utambuzi, michezo, kikundi cha wamisionari... Na pia katekesi kwa watoto na watu wazima. Kazi yetu na watoto vipofu na vijana pia inaendelea kwa kiasi kikubwa."

03 November 2023, 14:50