Tafuta

 Ziara ya Papa mnamo Aprili 2023 huko Hungaria Ziara ya Papa mnamo Aprili 2023 huko Hungaria  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Novemba 17 ni kumbukizi ya Mtakatifu Elizabeti wa Hungaria na mama wa maskini

Kila tarehe Novemba 17 ya kila mwaka,Mama Kanisa anamkumbuka Mtakatifu Elizabeti wa Hungaria,Mama,mjane na Mtawa wa Shirika la Tatu la Kifransiskani ambaye alipitia majaribu mengi lakini akijali maskini.Aliolewa na mfalme akiwa na miaka 14 tu na kuzaa watoto watatu.Alifariki akiwa na miaka 25 tu.

Na Angella Rwezaula, Vatican.

Kila tarehe 17 Novemba ya kila mwaka ni Siku ya Kumbukumbu ya Mtakatifu Elizabeth wa Hungaria, ambaye akiwa kijana wa miaka 14 tu, aliolewa na Louis IV, Mfalme wa Thuringia, mwenye umri wa miaka 20 na akamzalia watoto wa kiume Ermanno na wasichana wawili Sofia na Gertrude, wa mwisho alizaliwa siku ishirini tu mara baada ya kifo cha mumewe, huko Otranto alipokuwa akingojea kuanza safari na Frederick II, kwenda kwenye vita vya msalaba kuelekea Nchi Takatifu. Elizabeti akiwa amebakia mjane baada ya kuvumilia dhiki kubwa kwa ujasiri na kujitolea kwa muda mrefu kutafakari juu ya hali halisi ya mbinguni, alistaafu akachagua kama nyumba ya kawaida huko Marburg ambako alikuwa na hospitali ya wagonjwa na pia nyingiine ya wakoma, zilizojengwa kwa gharama zake mwenyewe, huku akitaka kupunguza umaskini wa kijamii. Akiwa amejiandikisha katika daraja la Tatu la Wafransiskani,(OFS)alijitolea mwenyewe kwa dhati kwa maskini zaidi, huku akiwatembelea wagonjwa mara mbili kwa siku, akawa mwombaji na kila mara akifanya kazi za unyenyekevu zaidi.

Chaguo la umasiki kuibua hasira

Chaguo lake hili  la umaskini kwa Elizabeti  liliamsha hasira za shemeji zake ambao walifikia hatua ya kumnyima watoto wake na kwa maana hiyo hata utajiri wa mumewe. Elizabethi akiwa amevutiwa na Mtakatifu Fransisko wa Assisi, aliyefariki kunako mwaka 1226, Elizabeth  hakukata tamaa kwa hiyo aliongozwa na hali ya kiroho ya Shirika la Tatu la Wafransicana, kama mke na mama alijitolea kwa ajili ya maskini, akakumbatia "umaskini wa dada" kama unavyoimbwa na Mtakatifu Francis, mpenzi wa umaskini. Ndiyo maana tunaoweza kuona kwamba Mtakatifu Elizabeth, jina lake kutoka kwa Kiebrania linamaanisha Mungu ni kiapo changu, ambaye kwa hakika alikuwa na sifa ya muuguzi, na  upendo katika jamii. Hadi sasa anajulikana akiwa na mikate mkononi huku akiwagawia maskini. Elizabeti Aliendelea kujitolea kwa nguvu zake zote hadi kunako tarehe 17 Novemba 1231 alipofariki akiwa na miaka 25 tu. Askofu wa Marburg, ambako Elizabeth  mwenyewe alitekeleza utume wake, aliandika kuhusu jambo hili kwamba: “Mbali na kazi hizi zenye bidii kwa niaba ya maskini, ninasema mbele za Mungu kwamba ni mara chache sana nimeona mwanamke mwenye kutafakari zaidi kama yeye; akirudi mahali pa faragha ambapo alikwenda kusali, na alionekana mara kadhaa uso wake uking'aa kwa namna ya ajabu, huku miale miwili ya jua ikimtoka machoni pake."

Alitangazwa kuwa Mtakatifu tarehe 1 Juni 1235 

Elizabeth alitangazwa mtakatifu tarehe Mosi Juni 1235 na Papa Gregori IX.  Kwa njia hiyo Elizabeth  aligeuka kuwa ni msukumo na kielelezo kwa wanawake wa Ujerumani na kwa wale waliotaka kujitolea kwa ajili ya maskini na kutafakari ambapo  kati ya hao, waliojulikana zaidi ni watawa wa Shirika la tatu la Wafransicakani Welizabetini walioanzishwa  na Mwenyeheri Elisabeti Vendramini kunako (1790-1860).

Katika katekesi yake Papa Mstaafu benedikito XVI alimwelezea Elizabeth

Papa Mstaafu Benedikto XVI wakati wa Katekesi yake mnamo tarehe 20 Oktoba 2010 alielezea kuwa Elizabeth wa Hungaria: alitenda kwa bidii kazi za huruma, aliwapatia chakula na vinywaji wale waliogonga mlango wake, alitoa nguo, alilipa deni, alitunza wagonjwa na kuzika wafu. Akishuka kutoka kwenye ngome yake, mara nyingi alienda na wajakazi wake kwenye nyumba za maskini, akiwapelekea mikate, nyama, unga na vyakula vingine. Alipeleka chakula hicho kibinafsi na kukagua kwa uangalifu nguo na matandiko ya maskini. Tabia hii iliripotiwa kwa mumewe, ambaye sio tu hakuwa na hasira, lakini alijibu kwa washtaki kuwa: "Alimradi  asiniuzie ngome, ninafurahi!" Muujiza wa mkate uliogeuzwa kuwa waridi ulifanyika katika muktadha huu: Elizabeti alipokuwaakitembea barabarani akiwa na vazi lake lililojaa mikate kwa ajili ya maskini, alikutana na mumewe ambaye alimuuliza kwamba alikuwa amebeba nini. Na kwa hiyo alifungua aproni yake na,badala ya mikate, maua ya kupendeza yalitokea. Ishara hii ya upendo inapatikana mara nyingi katika taswira ya Mtakatifu Elizabeti." Alisema Papa Mstaafu (rej. Benedetto XVI, Santa Elisabetta d’Ungheria, Udienza generale del 20 ottobre 2010).

Shirika la kitawa linalofuata tasaufi ya Mtakatifu Elizabeti wa Hungaria

Shirika la Tatu la Wafransikani  ambao wanajulikana kama watawa wa elimu ya juu wa Wafransiskani wa Elizabetini wa Padua,  ni Taasisi iliyoanzishwa na Mtakatifu  Elisabeti Vendramini mnamo mwaka wa 1828. Shirika hili limeenea katika mataifa ya  Italia Misri, Kenya, Argentina na Ecuador na nyumba Mama iko Padua. Nchini Italia. Katika nyayo za Mtakatifu Fransis wa Assisi na Elizabeth wa Hungaria,  Watawa hawa wanaishi Injili takatifu ya Bwana wetu Yesu Kristo katika utii, umaskini, usafi wa kimwili uliowekwa wakfu na jumuiya kamilifu". Hali yetu ya kiroho imechochewa na hali ya kiroho ya Wafransican ya kuwa na mtazamo wa mtawa  Elizabeti yanaelekezwa na Yesu katika unyenyekevu wa kufanyika kwake mwili na katika upendo wa mateso yake.  Uzoefu wa huruma ya Baba, ambayo kwa hakika ulionysha maisha na utume wa Elisabeti  Vendramini, pia inaashiria maisha na utume wao, binti zake, walioitwa kuwa na moyo kama wa Mungu pamoja na wale wanaoteseka, wanaotengwa, wanatafutwa. au wanakosa  marejeo ya elimu; kwa wale wanaotaka kuunda dhamiri na utamaduni wenye mwelekeo wa Kikristo.  Kwa kuimarishwa na zawadi ambayo imewajia kuanzia kwa Mtakatifu Elizabei, wwao anajitambua kama jumuiya za imani: wanashiriki maisha ya  wakati, furaha na shida, 'mkate' na msamaha kila siku, ili kusaidiana kuishi ufahamu kwamba. Mungu ni wema wetu mkuu na kwamba maana ya utume wao katika utofauti wa huduma, uko katika kuhisi kwamba wao ni washiriki wake ili kila mtu aweze kukutana naye kama Baba.

Mahubiri ya Mtakatifu Yohane Paulo II wakati wa kumtangaza Mwenyeheri

Katika mahubiri ya Mtakatifu Yohane Paulo wa II, wakati wa kumtangaza mwenyeheri Elizabetu Vedramini kunako tarehe 4 Novemba 1990 , alithibitisha kuwa, “ Hata sura ya Mwenyeheri Elisabeti Vendramini ni sehemu ya nguvu ya kiroho ambayo ina lengo kuu la "muungano" wa kina na Yesu na upendo kwa maskini, ambao ni wahusika wakuu wa kurasa nyingi za Injili. Maneno ya Bwana: “Nauhurumia umati huu, kwa sababu wamekuwa wakinifuata kwa siku tatu na hawana chakula”(Mk 8, 2 )yalitia alama sana moyo wa Elizabeti aliyebarikiwa tangu ujana wake wa mapema, alipofanya hivyo kwa bidii. alihisi msukumo wa kujiweka wakfu kabisa kwa Kristo na kwa huduma ya maskini. Aliacha starehe za maisha ya familia na kijamii bila kusita kujitolea kwa wasichana waliotelekezwa na wahitaji katika vitongoji vilivyotengwa zaidi. Katika kazi hii, Elizabeti alipata msukumo na nguvu kutoka Juu na kutoka kwa roho yake kali ya maombi. Akiongozwa na dini , akiwa na usikivu wa kutafakari uliosafishwa, aliyetangazwa mwenyeheri alijipoteza katika kutafakari Fumbo la Utatu Mtakatifu, na kushika nguvu ya umwilisho wa Neno, ili kufika, kwa hiyo, katika sifa na sifa ya Kristo maskini na msulubiwa, ambaye alimtambua na kumtumikia, kwa hiyo katika maskini  wa kupendwa sana. Kutoka mbinguni leo hii  Elizabeti anawahimiza wale wote wanaotaka kusaidia ipasavyo ndugu zao katika nafsi na mwiliili kupata nguvu kutokana na imani katika Mungu na kutokana na kumwiga Kristo. Katika hili alithibitisha kuwa chipukizi chenye matunda ya hali ya kiroho ya Wafransiskani. Aliiga zaidi ya maisha duni ya Mtakatifu Francis, imani ya hakika na rahisi na upendo wa Kristo aliyesulubiwa. Mwenyeheri Vendramini pia anatufundisha kwamba pale ambapo imani ina nguvu na uhakika zaidi, hapo msukumo wa upendo kwa wengine utakuwa na nguvu zaidi. Mahali ambapo hisia ya Kristo inatambuliwa zaidi, hapo hisia ya mahitaji ya ndugu itakuwa sahihi zaidi na yenye matokeo. (Rej:https://www.vatican.va/content/john-paul-ii/it/homilies/1990/documents/hf_jp-ii_hom_19901104_quattro-beatificaz.html(.

 

17 November 2023, 10:25