Tafuta

2022.11.10 Askofu Mkuu Martinelli- Balozi wa Kitume Abu Dhabi 2022.11.10 Askofu Mkuu Martinelli- Balozi wa Kitume Abu Dhabi 

Martinelli:Mwaka wa Jubilei wa mashahidi wa Arabia kushuhudia uaminifu kwa Kristo

Mwakilishi wa kitume wa Arabia ya Kusini aliongoza ibada Misa Takatifu ya ufunguzi wa Mlango Mtakatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu huko Abu Dhabi,wakati wa Jubilei maalum ya miaka 1500 tangu kuuawa shahidi Mtakatifu Areta na wenzake.Kushuhudia inamaanisha kuwasiliana na imani ya Kikristo kupitia maisha ya mtu.

Vatican News

Historia ya Wakristo katika Ghuba ni historia yaKanisa la wahamiaji", watu waliofika kutoka nchi tofauti zenye lugha na mila tofauti ambao hata hivyo wakawa sehemu ya historia ya Kanisa katika eneo hili. Askofu Mkuu Paolo Martinelli, Balozi wa  kitume wa Kusini mwa Arabia,  aliwaeleza waamini  kwa ujumbe wa barua kwa nia ya video wakati wa ufunguzi, huo tarehe 9 Novemba  2023 huko Abu Dhabi, wa Mlango Mtakatifu, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, kwa  ajili ya Jubilei maalumu  iliyotangazwa katika Vikariati vya Kitume vya Kaskazini na Kusini mwa Arabia, ya miaka 1500 baada ya kifo cha kishahidi cha Mtakatifu Areta na wenzake, waliouawa pamoja na waamini wengine elfu 4 wakati wa mateso dhidi ya Ukristo mnamo mwaka  523 huko Najran, huko Arabia ya kabla ya Uislamu.

Mlango mtakatifu 

Kiongozi huyo aliongoza maadhimisho hayo baada ya kufungua Mlango Mtakatifu. Na Askofu Mkuu Aldo Berardi, Balozi wa  kitume wa Kaskazini mwa Arabia, alitoa mahubiri yake. Waliohudhuria, miongoni mwa wengine, walikuwa ni Kadinali Miguel Ángel Ayuso Guixot, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya kidini na a, ambaye amekuwa huko Abu Dhabi kwa Mkutano wa Viongozi wa Imani Ulimwenguni kwa kuzingatia  kilele cha COP28, na balozi wa kitume katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Askofu Mkuu  Christophe Zakhia El- Kasis. Jubilei hiyo ilizinduliwa mnamo tarehe 4 Novemba katika Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Arabia huko Awali, Bahrain, kwa sherehe iliyoongozwa na Askofu Mkuu  Aldo Berardi, Balozi wa kitume wa Kaskazini mwa Arabia.

Askofu Mkuu Berardi: tunamshuhudia Kristo kwa mtindo wetu wa maisha

Askofu Mkuu Berardi alikumbuka kwamba jumuiya ya sasa ya Kikristo ya eneo hilo ina umri wa miaka 1,500. "Wengi wenu mnajua mjue kuwa Mtakatifu Thomas alipitia hapa kwenda India; na kwamba wamisionari wengi pia walipitia hapa walipokuwa wakienda Uajemi, Uchina  na India ... Kwa hiyo tumepata kiungo cha yaliyopita: tunajua kwamba kaka na dada katika Kristo wameishi hapa. Kwa hiyo, sisi siyo peke yetu, sisi si watu wapya, sisi si Kanisa jipya bali  sisi ni mwendelezo wa Kanisa hilo." Balozi wa  kitume aliendelea kusema kuwa “Na hata kama leo hii , hatuwezi kushika njia na kumtangaza Yesu”, ushuhuda unakuwa suala la maisha ya kila siku, ambapo kila tendo, linamshuhudia Kristo katika kazi yetu, katika familia yetu katika uaminifu wetu, katika mshikamano wa maisha yetu, katika mahusiano yetu na wengine. Kwa ufupi, na mtindo wetu wa maisha."

Ushuhuda wa mashahidi wa Arabia ni uaminifu kwa Kristo

Katika ujumbe wake, Askofu Mkuu Martinelli alianza kutoka kwa ushuhuda wa mashahidi hawa wa Arabia kuonesha hali ya uaminifu kwa Kristo, akichagua kufa badala ya kukana imani yao ya Kikristo. Mwaka wa Jubilei, alisema Balozi wa  kitume, ni fursa ya kuimarisha maana ya ushuhuda wa Kikristo, ambao waamini wanaitwa kuubeba kila siku katika maisha yao. Kuadhimisha wafia imani kunamaanisha kuwaheshimu wale waliojifananisha kabisa na Kristo na upendo wake hadi kufikia hatua ya kufanya zawadi kuu ya maisha yao” na pia inamaanisha kufanya upya kujitolea kwa ushuhuda wa Kikristo ulimwenguni na katika jamii. Balozi wa Kitume  Martinelli aliwaalika waamini kuwaombea mashahidi watakatifu na kuongeza zaidi maana ya ushuhuda wa Kikristo katika eneo la Ghuba, pia akifafanua kwamba kutoa ushahidi kunamaanisha kuwasiliana imani ya Kikristo na kukutana na Yesu kupitia maisha na maneno ya mtu.

Mwaka wa Jubilei unaruhusu kupokea zawadi ya msamaha

Kwa Wakristo, ushuhuda ni dhamira ya kimsingi ya kuwepo kwa mtu: kuwasilisha upendo wa Kristo kwa kila mtu. Ushuhuda wa Kikristo basi una maeneo ambayo yameunganishwa na sakramenti. Ubatizo hufanya mashahidi wa Injili kwa ulimwengu wote; Uthibitisho hukumbuka kwamba ni Roho ambaye hutuongoza kwa maneno sahihi na vitendo vinavyofaa kwa ajili ya ushuhuda; Ekaristi husherehekea upendo wa Kristo ambaye analingana naye hadi kufikia hatua ya kuwafanya waamini mkate uliomega kwa ajili ya wengine, kama wafia imani walivyofanya; Upatanisho hufanya “mashahidi wa huruma ya Mungu. Mwaka wa Jubilei huruhusu mtu kupokea zawadi ya msamaha wa jumla na inaruhusu mtu kuwa na uzoefu mkubwa zaidi wa rehema. Ndoa “inakaribisha ushuhuda wa Kikristo katika familia na kwa jamaa na marafiki; kaka na dada zake, upako wa wagonjwa “unatuwezesha kupata magonjwa na kifo kama matukio yanayoshuhudia kumtumaini kikamilifu Kristo.

Kujenga ududu wa kibinadamu

Martinelli basi alionesha katika uzoefu wa vyama, harakati za kikanisa na vikundi vya maombi vinavyohuisha Kanisa, ushahidi kwamba karama zinazoenezwa na Roho Mtakatifu daima zina mwelekeo wa ushuhuda kwa Injili. Kwa hiyo Mwaka wa Jubilei lazima uwe fursa ya kujiuliza jinsi gani karama mbalimbali za kiroho zinatufanya tuwe na uwezo wa ushuhuda wa kweli na mazungumzo. Askofu alihitimisha kwa kukumbusha "maisha ya kuwekwa wakfu kati ya karama za karama, na ushuhuda huo unaruhusu safari ya pamoja na waamini wa dini na imani nyinginezo, ambao  alisema wote tumeitwa nao kujenga ulimwengu wa kidugu zaidi na wa kibinadamu.

10 November 2023, 17:28