Tafuta

2023.10.30  Tendo la kuwekwa wakfu kwa Moyo safi wa Maria Nchi Takatifu 2023.10.30 Tendo la kuwekwa wakfu kwa Moyo safi wa Maria Nchi Takatifu   (@ Patriarcato latino di Gerusalemme)

Kard.Pizzaballa,Nchi Takatifu kuwekwa wakfu kwa Moyo Safi wa Maria

Kwa maombezi yako,huruma ya Mungu inaweza kuenea duniani kote na mdundo mtamu wa amani utaashiria siku zetu tena.Hapo zamani za kale ulitembea katika mitaa ya nchi yetu;tuongoze sasa kwenye njia za amani.Ni kifungu cha sala aliyosali Patriaki wa Yerusalemu,Kardinali Pizzaballa Oktoba 29,2023 kuombea amani.

Na Angella Rwezaula, -Vatican.

Katika hali halisi inayoendelea ya ghasi, vurugu na silaha kupamba moto kati Ya Israel na Gaza na kusababisha si vivyo tu, bali majeruhi, na maafa mengi, ya miundo mbiunu, kama vile hospitali, shule, nyumba na mengine mengi, tarehe 29 Oktoba 2023, Patriaki wa Kilatini, Kardinali Pierbatista Pizzaballa alisali sala ya kuweka wakfu kwa Moyo safi wa Bikira Maria kwa ajili ya Nchi Takatifu na watu wake.

SALA

Ee Maria, Mama wa Mungu na Mama yetu, Malkia wa Palestina na Nchi Takatifu, wakati huu wa majaribu tunakugeukia wewe kwa sababu unatupenda na unatujua: hakuna mahangaiko ya mioyo yetu ambayo yamefichwa kwako. Mama wa rehema, ni mara ngapi tumepata utunzaji wako wa kufikiria na uwepo wa amani! Huachi kutuongoza kwa Yesu, Mfalme wa Amani. Hata hivyo ubinadamu umeondoka kwenye njia hiyo ya amani. Umesahau mambo tuliyojifunza kutokana na mikasa ya hivi karibuni, kutokana na sadaka za mamilioni ya wale waliouawa katika vita. Kwa dhambi zetu tumevunja moyo wa Baba yetu wa Mbinguni, ambaye anatamani tuwe kaka  na dada. Sasa kwa aibu tunalia: Utusamehe, Bwana!

Mama Mtakatifu, katikati ya mapambano na udhaifu wetu, katikati ya fumbo la uovu ambao ni uovu na vita, unatukumbusha kwamba Mungu kamwe hawaachi watu wake, bali anaendelea kututazama kwa upendo. Alikupa sisi na kuufanya Moyo wako Safi kuwa kimbilio la Kanisa na kwa wanadamu wote. Sasa tunabisha kwenye mlango wa moyo wako. Sisi ni watoto wako wapendwa. Tuna hakika kwamba, katika nyakati za taabu zaidi za historia yetu, hutabaki kiziwi kwa ombi letu na utatusaidia.

Hivi ndivyo ulivyofanya huko Kana ya Galilaya, ulipomwomba Yesu katika kutaka  kuhifadhi furaha ya karamu ya arusi, ulimwambia: “Hawana divai” (Yh 2:3). Sasa, ee Mama, rudia maneno haya, kwa sababu katika siku zetu tumeishiwa divai ya matumaini, furaha imetoweka, udugu umeshindwa. Tumesahau ubinadamu wetu na kutapanya zawadi ya amani. Ni kiasi gani tunahitaji msaada wako wa mama! Malkia wa Rozari, utufanye tuhisi hitaji la sala na toba. Waongoze viongozi wa ulimwengu na wale wanaoamua hatima ya mataifa, ili waamue kulingana na haki na ukweli, na kufanya kazi kwa faida ya wote.

Malkia na Mama yetu, waonyeshe wenyeji wa nchi yako njia ya udugu. Katikati ya ngurumo za silaha, geuza mawazo yetu kuwa amani na panga zetu kuwa majembe. Mguso wako wa mama utulize wale wanaoteseka na kukimbia kutoka kwa roketi na mabomu. Kumbatio lako la mama liwafariji wale waliojeruhiwa au kulazimishwa kuondoka majumbani mwao, waliopoteza wanafamilia wao, wafungwa na waliopotea na wafungwa. Mama Mtakatifu wa Mungu, ulipokuwa chini ya msalaba, Yesu, akiona mwanafunzi kando yako, alisema: "Tazama mwana wako" (Yh 19.26). Kwa njia hii amemkabidhi kila mmoja wetu kwako. Kwa mwanafunzi, na kwa kila mmoja wetu, alisema: "Tazama Mama yako"(Yh 19:27). Mama Maria, sasa tunapenda kukukaribisha katika maisha yetu na historia yetu.

Katika saa hii, watu wa Nchi Takatifu wanapokugeukia, moyo wako unadunda kwa huruma kwao na kwa watu wote walioangamizwa na vita, njaa, ukosefu wa haki na umaskini. Kwa hivyo, Mama wa Mungu na Mama yetu, kwa Moyo wako Safi tunakabidhi kwa dhati na kujiweka wakfu sisi wenyewe, Kanisa letu, wanadamu wote, watu wa Mashariki ya Kati na zaidi ya yote, watu wa Nchi Takatifu, ambayo ni yako, umeipamba kwa kuzaliwa kwako, kwa fadhila zako na kwa uchungu wako, na kutoka hapo ukampa Mkombozi kwa ulimwengu. Acha vita viishe na amani isambae katika miji na vijiji vyetu. Kwa maombezi yako,huruma ya Mungu inaweza kuenea duniani kote na mdundo mtamu wa amani utaashiria siku zetu tena. Hapo zamani za kale ulitembea katika mitaa ya nchi yetu; tuongoze sasa kwenye njia za amani. Amina.

Sala kwa ajili ya Nchi Takatifu
05 November 2023, 11:42