Tafuta

21 Novemba 2023 manovisi 10 wa Shirika la Mabinti wa Bikira Maria Mama wa Msaada wa Daima,walifunga nadhiri za Kwanza katika Parokia ya Kagondo Jimbo la Bukoba Tanzania.  21 Novemba 2023 manovisi 10 wa Shirika la Mabinti wa Bikira Maria Mama wa Msaada wa Daima,walifunga nadhiri za Kwanza katika Parokia ya Kagondo Jimbo la Bukoba Tanzania.  

Bukoba-Tanzania,Manovisi 10 wafunga nadhiri za Kwanza

Watawa watambue na kuitumikia miito yao mitakatifu kwa nguvu zao zote na kutii nadhiri walizoweka.Kwa waamni Wakristo waitikie miito pale tu wanapoitwa kuitumikia.Alisema hayo Novemba 21 na Askofu Kilaini,Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki la Bukoba,Tanzania wakati wa Misa ya kufunga nadhiri kwa manovisi 10 wa Shirika la Mabinti wa Bikira Maria Mama wa Msaada wa Daima.

Patrick Tibanga, - Radio Mbiu na Angella Rwezaula, - Vatican.

Mama Kanisa kila mwaka ifikapo tarehe 21 Novemba anaadhimisha Siku kuu ya Bikira Maria kutolewa Hekaluni, sambamba na Maadhimisho ya Siku ya Watawa wa Ndani. Siku hiyo iitwayo ya Pro Orantibus kwa kilatino yaani wanaosali, huwa pia ni  fursa ya kutembelea jumuiya za watawa wa ndani, kukutana na kufahamiana na watawa na kuwaruhusu wasaidiwe kugundua upya kile ambacho ni muhimu katika maisha na hasa kuanzia na Injili ya Bwana. Kwa maana nyingine ni kwamba Waamini katika siku hiyo wanakumbushwa kwamba, Kanisa ni nyumba ya Sala na Ibada, mahali ambapo Fumbo Takatifu la Mungu linaadhimishwa ili kumsifu Mungu kwa sababu mwanadamu anapata wokovu.

Askofu Kilaini wakati wa misa kwa ajili ya nadhiri za kwanza kwa manovi 10
Askofu Kilaini wakati wa misa kwa ajili ya nadhiri za kwanza kwa manovi 10

Ni katika muktadha wa sherehe hizo ambapo Msimamizi wa Kitume Jimbo Katoliki la Bukoba, Nchini Tanzania, Askofu Method Kilaini, aliongoza ibada ya misa Takatifu kwa ajili ya Watawa wa Shirika la Mabinti wa Bikira Maria Mama wa Msaada wa Daima, wakiwa na manovisi 10 ili kufunga nadhiri zao za kwanza katika Parokia ya Bikira Maria,  Mama wa Msaada wa Daima huko  Kagondo Jimbo Katoliki la Bukoba.  Askofu Kilaini kwa kuongozwa na  Masomo yaliyosmowa na hasa Somo la Kwanza kutoka katika Kitabu cha Samueli 1Sam 3,1-10.19-20, katika  kifungu kinachelezea wito wake, kilikuwa ni kitovu cha mahubiri yake kwamba Samueli  hakujua wito wake japokuwa alikuwa analala katika hekalu la Bwana,  hadi anlipoitwa bila kujua ni nani  anaye mwista na kwa maongozi ya  Heri alilimwelewesha wito huo, baada ya kuanchwa usingizini mara tatu.

Mara baada ya kufunga nadhiri za kwanza katika Parokia ya Kagondo Bukoba
Mara baada ya kufunga nadhiri za kwanza katika Parokia ya Kagondo Bukoba

Askofu Kilaini alikazia kwa watawa hao  ili waelewe vema maana ya utawa kwa sababu hawakuitwa kwa ajili ya  utajiri, bali ni utumishi wa kuwa tayari kumfuata Bwana na kujitoa bila kujibakiza licha ya changamoto na magumu yatakayojitokeza katika safari ya wito wao.  Askofu aidha alisistiza kwamba kujiunga katika  utawa siyo kazi rahisi na tambarare, watawa kwa hiyo wanatakiwa kuvaa silaha ya imani na ukakamavu kwa ajili ya kukabiliana na magumu katika utumishi huo na kutii sheria zote za wito na kuuishi vyema katika ya Shirika lao. “Ukiwa katika Utawa milima na mabonde pamoja na changamoto mbali mbali vyote hivyo havitakuwa shida kama umejitoa kwake Mungu, kwani  naye atakupatia maelekezo na lazima uyafuate,” alisema Askofu Kilaini. “Umeingia katika Shirika lako na leo utaahidi utii kwa wakubwa na maelekezo ya Shirika ambayo ndio dira ya kufikia lengo,  kwani hutowezi kufikia malengo kwa kujipangia malengo yako binafsi, na Mungu anataka uweze kutimiza wajibu kutokana na maelekezo na malengo ya shirika ili ufikie lengo lako.” Alisema Askofu Kilaini.

Wazazi msiwazuie watoto kujiunga na utawa katika mashirika mbali mbali

Katika mahubiri hayo, aidha aliwageukia  wazazi na walezi kwamba wawaruhusu watoto wao kujiunga na mashirika mbali mbali ya kitawa na si kuwazuia kwani kwa kufanya hivyo ni kuzuia kuitii sauti ambayo Mungu  anamwita mtu huyo na vilevile kuwashauri wakristo kuwa tayari kumfuata Kristo katika magumu na furaha zote na kwamba  wito sio kutafuta ukubwa bali ni utumishi hivyo mwanadamu anatakiwa kujitoa kuwatumikia wengine na kujinyenyekeza na kuomba neema ya Mungu kwa kusali ili kudumu katika wito ambao wameitwa  wakijua kuwa bado wao ni dhaifu. “Kwanza ni kumpenda na kujitoa kwa Mungu kwa nguvu zako zote, unakua sista kwa sababu unampenda Mungu na upo tayari unataka kumtumikia, na mengine yote yatakwenda vizuri na mengine yatakuwa ya ziada, nanyi wazazi muwaruhusu na kuwasaidia watoto wenu kuitikia wito wanaoitiwa katika kanisa, msiwazuie”. Kwa huhitimisha Askofu Kilaini alisema, utawa ni utumishi unaohitaji kujitoa na kukubali kunywea kikombe cha Bwana na kuwa tayari kumfuata Kristo katika nyakati zote na kuwa mtumishi wa wote na kujitoa bila kujibakiza na kuacha ubinafsi na kuwafikiria wengine kwa kujitoa na kuwa tayari kumpa Mungu walivyonavyo.

Tumshukuru Mungu kwa zawadi ya Wito
Tumshukuru Mungu kwa zawadi ya Wito

Katika Misa hiyo iliyoudhuriwa na Maaskofu, Mapadre, Waamini walei na Wazazi, jamaa na marafiki katika Kanisa hilo, waliwaona kwa hiyo Manovisi 10 wakiweka nadhiri za kwanza Kwa Mungu katika Shirika la Mabinti wa Bikira Maria Mama wa Msaada wa Daima  na wote hawa  ni kutoka katika   Jimbo Katoliki la Bukoba Tanzania. Watawa hao ni: Sr Maria Caritas Twinomujuni, mzaliwa wa Parokia ya Katoke. Sr Maria Agripina Kokusiima, mzaliwa wa Parokia ya Bugandika, Sr Maria Saraphina Kokutangaza,  mzaliwa wa Parokia ya Kasherero, Sr Maria Alfredina Namayanja mzaliwa wa Parokia ya Kassambya, Sr Maria Peninsula Kahumbya, mzaliwa wa Parokia ya Bumbire, Sr Maria Leonarda Alinda, mzaliwa wa Parokia ya Maruku, Sr Maria Diana Asiimwe, mzaliwa wa Parokia ya Kaazi, Sr Maria Sophia Malonda, mzaliwa wa Parokia ya Bumai, Sr Maria Vedastina Kaliba mzaliwa wa Parokia ya Kimwani, na hatimaye  Sr Maria Violeth Aganyira, mzaliwa wa Parokia ya Nshamba.

Je unajua nini juu ya Siku kuu ya Bikira Maria kutolewa Hekaluni?

Siku kuu ya Bikira Maria kutolewa Hekaluni, Siku kuu yenye  asili ya kale na ibada, ambayo imeunganishwa na utamaduni wa uchamungu. Sherehe ya kiliturujia, ambayo ilianza karne ya 6 huko Mashariki na karne ya 14 huko Magharibi, inaakisi mchango kamili wa kwanza ambao Maria alijitolea kabisa na kuwa kielelezo cha kila roho ya kujiweka wakfu kwa Bwana. (rej. Misale ya Kirumi). Katika maandishi ambayo hayakujumuishwa miongoni mwa vitabu vya Biblia Takatifu, kama yale ya Yakobo,yatuambia kuhusu kuzaliwa kwa Maria Mtakatifu kwa Yoakimu na Anna huko Yerusalemu, katika nyumba isiyo mbali na hekalu, ambaye alipelekwa Hekaluni akiwa na umri wa miaka mitatu.

Bikira Maria alipokea  habari njema ya furaha kutoka kwa Malaika
Bikira Maria alipokea habari njema ya furaha kutoka kwa Malaika

Kwa hiyo Siku kuu ya tarehe 21 Novemba ya kila mwaka ya kuwakilisha Hekaluni kwa   wa Bikira Maria ina umuhimu mkubwa, pia kwa sababu inajumuisha ishara thabiti ya uekumeni na mazungumzo na ndugu zetu kutoka Mashariki.  Zaidi ya ukweli wa kihistoria wa habari nyingi, fikira nzuri za kitaalimungu ziliibuka: Maria ni binti wa Sayuni, anayehusishwa na hekalu. Mara kadhaa tunaona picha Bikira Maria katika maisha ya nyumbani, akiwa na ahadi ya kutimiza iliyotolewa kwa Malaika kuwa mtumishi wa Bwana.  Kiukweli, katika mapokeo ya Kiyahudi, Adamu na Eva, walipokuwa katika hali ya kutokuwa na hatia, walilishwa na Malaika. Kwa hiyo ukweli wa kuwasilishwa kwa Maria Hekaluni   lazima uwe wa kiasi zaidi na wakati huo huo wa utukufu zaidi.  Na ni ukweli kwamba  ilikuwa pia kupitia huduma hiyo kwa Bwana katika hekalu kwamba Maria alitayarisha mwili wake, lakini juu ya roho yake yote, kumkaribisha Mwana wa Mungu, akitekeleza ndani yake neno la Kristo: "Heri walisikiao neno la Mwenyezi Mungu na kuweka katika matendo.

2019 Papa aliwatembelea watawa wa ndani wa  Vallegloria, huko Spello
2019 Papa aliwatembelea watawa wa ndani wa Vallegloria, huko Spello

Waandishi wengine watakatifu wamechukua hiyo kama sababu ya kuwasilisha  kwa Mama Bikira Maria  kama kielelezo cha maisha ya wakfu. Kwa hivyo uwasilishaji  wa Maria katika hekalu unaonekana kwetu kama wakfu wa kweli kwa Bwana. Maria anatolewa kwa Mungu na Mungu anamrudisha kwetu sisi kama mama wa waamini wote. "Yeyote anayefanya mapenzi ya Mungu ndiye kaka yangu, dada yangu na mama yangu(Mk 3,35). Yeye, Mama, hekalu la Mungu, alikaribisha Neno aliyefanyika mwili, na tunamwilishwa Neno maishani mwetu.

Bikira Maria na
Bikira Maria na

Na kwa njia hiyo katika fursa ya siku kuu hiyo, Mama  Kanisa pia huadhimisha Siku ya Maisha ya  Watawa wa Ndani duniani ambao ni Watafakuri  kwa wengine wanasema Siku ya "Pro Orantibus", ambayo ni maneno ya Kilatini yenye maana ya "kwa wale wanaosali." Tukio muhimu la kikanisa kwa Wakatoliki wote ulimwenguni kuadhimisha maisha yaliyofichika ya wanaume na wanawake waliowekwa wakfu katika Monasteri, Konventi yaani na nyumba za watawa. Ni maadhimisho ya siku hiyo  kwa sababu maisha ya kutafakari ni zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwetu sote, katika  ulimwengu wote ambao  unanufaika kiroho kutokana na sala na sadaka ya roho zilizojitolewa na za uaminifu, hata ikiwa zote zimefichwa machoni pa wanadamu na kuonekana kwa Mungu tu. Katika siku hii, waamini wanahimizwa kusaidia jumuiya za utawa wa ndani na tafakari katika jimbo lao kwa njia ya sala, faraja na msaada ikiwezekana.

Nadhiri za Kwanza kwa Manovisi 10 huko Bukoba Tanzania
27 November 2023, 15:28