Vijana wa Roma wasali kwa ajili ya Israeli na Palestina
Na Angella Rwezaula, Vatican.
Wakiwa wamepangwa katika duara kubwa katika uwanja wa Jumba la Laterano, Roma vijana karibu 600, walioshikana mikono, na kusali pamoja sala ya Baba Yetu ili kusihi zawadi ya amani ulimwenguni. Ni katika kesha la usiku wa tarehe 13 Oktoba 2023, na kutoa shukrani kwa shughuli za kiangazi ambazo katika miezi ya hivi karibuni zimehusisha maelfu ya vijana wengi wa Jimbo la Roma. "Furaha tunayopata inafunikwa na wakati wa huzuni sana katika ulimwengu unaopitia. Lakini furaha huleta amani na kwa furaha tushikane mikono na kumwomba Bwana atufanyie sote vyombo vya amani” alisema hayo Askofu msaidizi Dario Gervasi wa Roma.
Tukio hilo liliandaliwa na ofisi ya jimbo kwa ajili ya huduma ya kichungaji ya vijana kwa ushirikiano wa Kituo cha Kuzungumza cha Roma, Skauti wa Agesci na Fse, Chama cha Matendo ya Vijana Katoliki (CA) na Anspi. Hata huvyo kabla ya hayo sherehe ya kwanza ya shukrani ilianza kwa adhimisho la Ekaristi Takatifu katika Kanisa kuu la Mtakatifu Yohane huko Laterano iliyoongozwa na Kardinali Angelo De Donatis, Makamu wa Papa. Miongoni mwa waliokuwa naye ni mkuu mpya wa Seminari kuu ya Kipapa ya Roma Monsinyo Michele Di Tolve, na maaskofu wasaidizi watatu waliofuatana na vijana wa Roma kwenye Siku ya Vijana Duniani WYD huko Lisbon: makamu Baldo Reina, Paolo Ricciardi na Dario Gervasi. Katika afla ya pamoja uwanja ulijaa vijana, wengi wao walishiriki katika Siku ya Vijana Duniani huko Lisbon, wengine katika kambi za majira ya joto au vikundi vya Parokia.
Uzoefu wa kushirikishana na udugu ambao umefika “saa ya kushukuru na kumtolea Bwana matunda ya huduma ya mtu”, alisema Kardinali huyo akiwafafanua vijana kuwa ni “watu wa mapambazuko” kwa sababu kila wakati mtu huzingatia mapenzi ya Bwana na "mnafanya ishara ya huduma, ya huruma, ya kukaribisha" ninyi ni "mashahidi wa mapambazuko yenye kuendelea duniani. Ukuu wao ni huduma, nguvu yao ni urafiki na Bwana na kila mmoja ". Akiwatazama wadau hao vijana ambao angependa kuwakumbatia "mmoja mmoja" ili kuwashukuru kwa "zawadi iliyotolewa kwa Kanisa na jiji la Roma", Kardinali De Donatis alisema alikuwa na hakika kwamba "ugumu na furaha ya huduma, kuhiji na kushiriki” waliwaruhusu kuelewa siri mbili za furaha. "Kuwa marafiki wa Mungu na kuwa wakarimu. Kuamini na kupenda hutoa umoja na usitawanyike, usigawanyike ndani. Nguzo hizi mbili zimetoa amani."
Picha ya Mwenyeheri Carlo Acutis, ambaye Kanisa huadhimisha kila tarehe 12 Oktoba, iliwekwa karibu na Altare. Matumaini ya Kardinali De Donatis ni kukutana kila mwaka, siku ya kumbukumbu ya kiliturujia ya wenyeheri, alyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 15 tu mnamo mwaka 2006, ili “kumrudishia Bwana yale tuliyopokea kutoka kwa upendo wake”. Mwaliko wa Kardinali ulikuwa ni kuwa na uwezo, kama Carlo, daima kusema ndiyo kwa upendo wa Bwana "nyumbani, shuleni, kati ya marafiki, katika Chuo Kikuu, katika parokia. Ndiyo yenye furaha, thabiti, hakika, yenye kutegemeka, yenye ujasiri na ya uhakika."
Na kwa upande wa Padre Alfredo Tedesco, mkurugenzi wa ofisi ya Jimbo kwa huduma ya vijana, alikumbuka kwamba katika siku hizi liturujia mara nyingi hupendekeza picha ya shamba la mizabibu. "Tunapitia kipindi cha mavuno, mavuno mazuri ya msimu huu wa joto" alisema, huku akizingatia uzoefu wa WYD ambapo Jimbo la Roma lilipata kushiriki na majimbo mengine kumi na moja ya Mkoa wa Lazio. Ni zaidi ya vijana 1,300 waliofika Lisbon baada ya safari ndefu ya meli. "Uzoefu mkubwa wa imani, mabadiliko ya maisha kwa wengi," alisema. Pia kutoka kwa Don Alfredo mwaliko wa kuombea amani. "Tuweke katika Ekaristi hii nchi ya Yesu na vita vinavyoshika ulimwengu" alisema.
Wakati wa tafrija katika ua wa Vicariate alionyesha matukio yajayo ya huduma ya vijana huko Roma kuanzia WYD ya jimbo ambayo itaadhimishwa Dominika tarehe 26 Novemba, Siku Kuu ya Kristo Mfalme. Vijana wa Romai watashiriki Ibada ya Misa Takatifu itakayoongozwa na Papa Francisko katika Kanisa la Mtakatifu Petro ambayo itafuatiwa na wakati wa sherehe katika kituo hicho cha kihistoria. Hija imepangwa kuanzia tarehe 2 hadi 7 Januari 2024, ambayo lakini hajajulikana itakuwa wapi,kwa sababu "ilipaswa kuwa katika Nchi Takatifu- alielezea Padre Alfredo-. Walakini, watafanya mahali pengine, wakiomba amani kila wakati."