Tafuta

Maombi kwa ajili ya Nchi Takatifu Maombi kwa ajili ya Nchi Takatifu   (ANSA)

Comece,Askofu Crociata,Ombeni kwa ajili ya amani Yerusalemu

Kwa niaba ya Maaskofu wa COMECE,Rais wake anaelezea ukaribu wake wa maombi na mshikamano na wahanga na familia huko Israeli na Palestina.Anaomba Jumuiya ya Kimataifa na Ulaya kuingilia kati kufuatilia juhudi za kufikia amani ya kudumu katika eneo la Mashariki ya Kati,kwa kuzingatia sheria za kimataifa na haki sawa kwa wote.

Na Angella Rwezaula, Vatican.

Katika  Taarifa ya Rais wa  Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Nchi za  Umoja wa Ulaya (COMECE) Askofu  Mariano Crociata kuhusu hali ya sasa katika Nchi Takatifu imeanza na kifungu cha Neno la Mungu kisemacho: "Ombeni kwa ajili ya amani ya Yerusalemu!" (Zaburi 122). Na kwa  kwamba, "Nimejawa na majonzi makubwa na wasiwasi kutokana na ripoti zinazoendelea kutoka Nchi Takatifu, kufuatia mashambulizi makubwa kutoka Gaza yakilenga raia wasio na hatia katika Israeli na kuongezeka kwa wimbi la vurugu, na kusababisha mamia ya vifo na majeruhi. Kwa niaba ya Maaskofu wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Barani Ulaya  COMECE, ninapenda kueleza ukaribu na mshikamano wangu kwa wahanga wote na familia zao. "

Kushiriki wasi wasi wa Papa Francisko

"Nikishiriki wasiwasi wa Papa Francisko kuhusu hali hii mbaya, ninapenda kutoa wito kwa pande zote zinazohusika kusitisha mashambulizi, kuwaachilia mateka waliotekwa nyara na kusitisha wimbi la ghasia, kwani “ugaidi na vita havileti maazimio yoyote, bali tu kifo na mateso ya watu wengi wasio na hatia”. Vile vile ninatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Ulaya, kufanya kila jitihada katika kuchangia kupunguza hali hiyo, huku wakihakikisha haki za kimsingi za watu wote katika eneo hili na kuheshimu Hali ya kihistoria na kisheria ya nchi zote. Maneneo yote ya Madhabahu Matakatifu. "

Tuombe amani kupitia Bikira Malkia wa Amani

Kwa upande wa Rais huyo ana matumaini yake  kwamba "kuendelea kwa umwagaji damu kunaweza kuwakumbusha wanachama wa jumuiya ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Ulaya, juu ya udharura wa kufuatilia kwa nguvu zaidi juhudi za kufikia amani ya kudumu na endelevu katika eneo la Mashariki ya Kati, kwa kuzingatia sheria za kimataifa, haki. na haki sawa kwa wote. Tukimgeukia Bikira Maria, Malkia wa Amani, tuombe kwamba amani iwe katika Israeli na Palestina." Amehitimisha ujumbe wake Askofu Mariano Crociata Rais wa COMECE.

Rais wa COMECE, Askofu Crociata atoa ombi kwa ajili ya Israeli na Palestina
11 October 2023, 16:15