Tafuta

Misa ya Ufunguzi wa Siku ya Vijana iliyofanyika Jini tarehe 1 Agosti 2023 na kuongozwa na Kardinali Manuel Clemente Mkuu wa Kanisa Katoliki Ureno. Misa ya Ufunguzi wa Siku ya Vijana iliyofanyika Jini tarehe 1 Agosti 2023 na kuongozwa na Kardinali Manuel Clemente Mkuu wa Kanisa Katoliki Ureno.  (ANSA)

WYD Lisbon2023:Kard.Clemente,kwa vijana Ulimwengu mpya huanza na mambo mapya!

Katika misa ya ufunguzi wa Siku ya vijana Duniani huko Lisbon tarehe Mosi Agosti 2023,imeongozwa na Patriaki Manuel Clemente Mkuu wa Kanisa Katoliki Ureno ambaye katika mahubiri yake amewambia kwamba Lisbon inawakaribisha kwa moyo wote na kushauri wakabiliane na maisha kama mchakato wa safari kila siku kwa hatua mpya.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kwa wengi imekuwa safari ngumu kutokana na umbali, miunganisho na gharama. Mlipaswa kutafuta rasilimali, kuandaa shughuli mbalimbali na kutegemea ishara za mshikamano ambazo, shukrani kwa Mungu, hazikukosekana. Kuanzia mbali au karibu, mlijiweka njiani. Ni muhimu sana kuingia barabarani. Na hivyo ndivyo tunapaswa kukabiliana na maisha yenyewe kama njia ya kufuata na kuifanya kila siku kuwa hatua mpya. Amesema hayo Kardinali Manuel Clemente, Patriaki wa Lisbon wakati wa mahubiri yake kwenye misa Takatifu ya ufunguzi wa Siku ya Vijana duniani 2023 katika Hifadhi ya Eduardo VII Jijini Lisbon Ureno, jioni tarehe 1 Agosti 2023, ikiwa ni sehemu rasmi ya kuingia kwa uhai wote siku hizi maalum za vijana hadi Dominika tarehe 6 Agosti 2023.

Misa ya ufunguzi wa Siku ya vijana Duniani 1-6-2023
Misa ya ufunguzi wa Siku ya vijana Duniani 1-6-2023

Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuondoka Jumatano asubuhi tarehe 2 Agosti kuelekea huko Lisbon kukutana na vijana hawa wanaomsubiri kwa hamu kubwa. Na kauli mbiu inayoongoza maadhimisho haya ni Maria akaamka na kuondoka kwa haraka (Lk 1,29). Ni katika muktadha wa mara baada ya kutangaziwa na Malaika kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Lengo kuu ni kuwataka vijana wajifananishe na sura hii ya Mama Maria akiwa kijana. 

Patriaki Clemente wa Lisbon aliongoza Misa Takatifu ya Ufunguzi wa Siku ya Vijana 1 Agosti 2023
Patriaki Clemente wa Lisbon aliongoza Misa Takatifu ya Ufunguzi wa Siku ya Vijana 1 Agosti 2023

Kadinali Clemente aliendelea katika mahubiri hayo kuwa: “Uadilifu hutufanya tuketi mbele ya njia za mawasiliano ambazo hututumia kwa urahisi tunapofikiria kuwa tunazitumia. Ukweli halisi, kwa upande mwingine, hutusukuma kudhamiria kukutana na wengine na ulimwengu kama ulivyo, kuutafakari na kuuboresha. Ni katika mwendo ule ule uliomtegemeza Maria,  na katika Roho yule yule anaye tutegemeza sisi pia. Wacha tuingie barabarani! Na ndiyo mwaliko wa Kardinali Clemente kwa vijana kwamba “Maria aliambata  pamoja naye Yesu, yule yule ambaye alikuwa mjamzito.

Umati wa Makuhani wanaosindikiza vijana wakati wa Misa Takatifu
Umati wa Makuhani wanaosindikiza vijana wakati wa Misa Takatifu

Na Yesu ni Mungu pamoja nasi, ili kuwa Mungu pamoja na wote. Kwa hivyo ndiyo haraka ya kwenda kwa Elizabeth, hata kwa kupanda milima. Kardinali Clemente ameeleza kuwa wao wanaijua 'haraka' hii, kwa sababu wengine pia wameharakisha kukutana ili kumpeleka Yesu na yote anayowapatia kwa maana ya upeo na wingi wa maisha. Kwa upande wa Kardinali alisema "hata sio lazima kila wakati kuelewa maneno, kama inavyotokea sasa, kati ya lugha nyingi zilizo hapa, bali ni macho ambayo yanazungumza na unajisikia salama na imani, katika mazingira ya Kikristo ambayo mnaunda pamoja na kwa ishara rahisi ambazo mnawasiliana nazo.  Kwa hiyo kiukweli kuna haraka hewani ambayo inazunguka kati yenu na katika maeneo mtakayotembelea siku hizi. Hewa ambayo ndani yake Roho wa kimungu hutembea, kwa utayari ambao Mungu pekee anao na anaowasiliana nao,” Alisisitiza Patriaki wa Lisbon.

Vijana wakiwa wanaudhria misa Takatifu
Vijana wakiwa wanaudhria misa Takatifu

Patriaki alisema: “Nilipomwambia Papa Francisko kwamba hii ndiyo kauli mbiu ya Siku yetu ya “Maria alikwenda kwa haraka ...,  mara moja aliongeza kusema kuwa: "Ni vizuri kwenda kwa haraka, lakini bila wasiwasi". Kwa dhati, tunahisi wasiwasi juu ya kile ambacho bado hatuna na tunatamani sana. Haraka ni tofauti, ni kushirikisha kile ambacho tayari kinatusukuma kuchukua hatua. Kwa hiyo ni suala la dharura ya utulivu ambayo haijui kusita. Mmefika hapa na wakati wa kukaa kwenu, mnawapa wengine kile mlichopokea pia.” Patriaki Clemente kwa hiyo ameongeza kusema  “Injili inatuambia juu ya furaha ya mkutano ule kati ya Maria na Elizabeti na kutambuliwa na yote yaliyotokea. Ni muhimu sana iwe hivi kwenu pia, kwa kila mtu. Kiukweli, kila moja ya mikutano yetu lazima ifunguliwe kwa salamu ya kweli, ambayo tunabadilishana maneno ya ukaribisho wa dhati na kushiriki kikamilifu.”aliwashauri Patriaki vijana.

Vijana wakishiriki Misa Takatifu
Vijana wakishiriki Misa Takatifu

“Lisbon inakukaribisha kwa moyo wote, kama sehemu nyingine ambazo tayari mmetembelea au mtatembelea katika Ureno hii ambayo pia ni Ureno yenu. Familia na taasisi zinawakaribisha”, alisisitiza ma kwa kuongeza  Patriaki Clemente amesema: “kwa wale  ambao wametoa nafasi na huduma zao kupatikana, ninatoa shukrani zangu, nikitambua katika kila mmoja wao nyumba ya Elizabeti, ambaye alimkaribisha Maria na Yesu aliyempelekea!  “Kuna hitaji kubwa la namna hii,  hata katika ulimwengu tunamoishi, wakati hatujui wengine,na hatuzingatii watu tunaokutana nao. Ulimwengu mpya huanza na mambo mapya ya kila mkutano na uaminifu wa salamu tunazobadilishana, alihitimisha Patriaki wa Lisbon.

Misa ya Ufunguzi wa Siku ya vijana Duniani huko Lisbon
Misa ya Ufunguzi wa Siku ya vijana Duniani huko Lisbon

Masomo yalisomwa kwa lugha tofauti na Maombi ya misa yaliombwa kwa lugha mbali mbali za mahali vijana wanakotokea na hata utoaji wa matoleo ya sadaka yalisindikizwa na baadhi ya vijana na familia. Nyimbo nzuri sana, kwa lugha zote zaidi  na zaidi Kireno na Kilatino. Mwisho wa Misa, Patriaki kwa kuzungumza lugha ya Kiingereza, kifaransa, Kireno, Kitaaliano na kuhispania, aliwaeleza jinsi ambavyo Jumatano Baba Mtakatifu atafika kati yao na  wanamsubiri na kumuombea. Amewashukuru wote na kuwapa baraka takatifu.

Maaskofu wakiwa katika misa ya ufunguzi wa siku ya vijana 1-6 Agosti 2023
Maaskofu wakiwa katika misa ya ufunguzi wa siku ya vijana 1-6 Agosti 2023
01 August 2023, 21:52