Tafuta

Waraka wa mwisho uliotiwa saini na viongozi wa Madhehebu ya Kikatoliki na Madhehebu mengine ya Imani ya Kikristo, Dini za Kiislamu na Wenyeji, ulionesha mgogoro mkubwa wa madeni, unaoathiri matumizi ya sekta ya kijamii Waraka wa mwisho uliotiwa saini na viongozi wa Madhehebu ya Kikatoliki na Madhehebu mengine ya Imani ya Kikristo, Dini za Kiislamu na Wenyeji, ulionesha mgogoro mkubwa wa madeni, unaoathiri matumizi ya sekta ya kijamii  

Viongozi wa kidini Afrika wajadili mikakati ya kukabiliana na majanga ya kisasa

Wakatoliki na wataalam wa dini mbalimbali walikusanyika mjini Nairobi,Kenya,ili kuweka mapendekezo na ushirikiano madhubuti kwa lengo la kufikia maendeleo endelevu na kuunga mkono ahueni ya Afrika.Ni katika mkutano wa siku mbili 7-8 Agosti ulioandaliwa na Caritas,Wajesuit na JubileeUSA.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Taarifa ya mwisho ya kuhitimisha mkutano wa siku mbili uliondaliwa na Caritas, Wajesuit na JubileeUSA, katika Hoteli ya Elysian jijini Nairobi inabainisha kuwa walikutana ili kushiriki katika majadiliano kuhusu namna bora ya kuvuka Afrika kupitia majanga ya kisasa yanayokumba bara zima. Katika tukio hilo ilibainisha, miongoni mwake athari za janga la Uviko-19, uhaba wa chakula na lishe, mabadiliko ya tabianchi, upotevu wa viumbe hai, uhaba wa maji, mifumo dhaifu ya afya, migogoro, ugaidi na madeni.” Mkutano huo, uliofanyika tarehe 7-8 Agosti 2023, ambao ulijumuisha mawasilisho, mijadala ya jopo, na vikao vya maingiliano vilivyoshirikisha viongozi wa kidini kutoka bara zima, pamoja na wataalamu wa Kanisa na wasio wa Kanisa, kama ilivyotathminiwa na hati ya awali iliyotolewa na taasisi ambazo iliandaa hafla hiyo.

Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ilitaja jinsi ambavyo, katika mazingira yenye changamoto barani Afrika, Kanisa Katoliki lilichukua jukumu muhimu kutokana na dhamira yake ya muda mrefu ya kukuza haki ya kijamii na utu wa binadamu. Katika Mtandao wake mkubwa wa taasisi za elimu, vituo vya huduma za afya, na programu za huduma za kijamii, taarifa hiyo ilithibitisha, kuwa hugusa mamilioni ya maisha, kutoa suluhisho malum kabisa  katika  muktadha kwa masuala mbalimbali ya bara. Waraka wa mwisho uliotiwa saini na viongozi wa Madhehebu ya Kikatoliki na Madhehebu mengine ya Imani ya Kikristo, Dini za Kiislamu na Wenyeji, ulionesha mgogoro mkubwa wa madeni, unaoathiri matumizi ya sekta ya kijamii ili kufikia maendeleo endelevu ya kimataifa na malengo ya tabianchi. Viongozi wa imani walifuatilia muhtasari wa mgogoro wa kiuchumi wa leo wa Afrika kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1990, wakati jumuiya zetu za kidini zilikuwa miongoni mwa wale waliokusanyika katika harakati za Jubilee kutetea kuvunja minyororo ya madeni katika nchi zinazoendelea.

Waraka huo ulitambua na kubainisha kuwa: “Tulisherehekea kwamba viongozi wa dunia waliwasilisha dola bilioni 130 za msamaha wa madeni, ambayo ilisaidia kuendeleza matumizi ya kupunguza umaskini katika nchi zinazopokea misaadaHata hivyo, bila kushughulikia kukosekana kwa usawa katika mfumo wa fedha wa kimataifa na changamoto za utawala wa ndani katika nchi zinazopokea misaada, mzigo unaolewesha wa madeni yasiyo endelevu unaendelea. Hasa, leo nchi za Kiafrika zinadaiwa kwa pamoja zaidi ya $1.1 trilioni katika deni la nje, na 25 kati yao ziko katika mgogoro mkubwa wa madeni”. Kupanda kwa viwango vya riba katika uchumi mkubwa na kupungua kwa ukuaji kunaongeza malipo ya madeni, wakati hali ya gharama ya maisha inamomonyoa mishahara na mapato. Uwekezaji mkubwa unahitajika ili kuokoa sayari inayodumisha maisha barani Afrika na kwingineko, wakati wa dirisha ambalo linafungwa kwa kasi, viongozi hao walibainisha. Kadhalika “Taarifa hiyo iliunganisha mapambano ambayo nchi maskini zilikumbana nazo kujaribu kujibu athari za kiafya, kiuchumi na kijamii za janga la Uviko-19 na uwekezaji mdogo katika afya, elimu, chakula, na ulinzi wa kijamii.

Kwanza, kabisa mchakato wa kupunguza madeni unaohakikisha wakopaji wanaweza kuomba na kufikia kwa haraka upunguzaji wa malipo ya deni hadi, angalau, kiwango kinachohitajika kulinda maendeleo muhimu na uwekezaji wa hali ya hewa. Kwa njia hiyo Viongozi wa madhehebu mbali mbali  pia walitoa wito kwa nchi kuweka sheria, kanuni, na mazoea ambayo yanatekeleza uwajibikaji wa kukopesha na kukopa ili kuzuia mzunguko mpya wa madeni. Sera nyingine zinazotarajiwa ni pamoja na “upatikanaji wa mikopo yenye masharti nafuu na kutokomeza wizi wa fedha za umma na ufisadi wa aina zote katika usimamizi wa fedha. Taarifa hiyo ilifafanua mkutano huo kuwa sio tu mkusanyiko lakini ushuhuda thabiti wa nguvu ya mshikamano ya umoja wa dini mbalimbali, hekima iliyounganishwa, na kujitolea kwa pamoja kwa haki. “Kwa kuaangaziwa  na Maandiko Matakatifu na imani zetu za kimaadili, tunashughulikia kwa uthabiti masuala muhimu ya madeni, utawala, na tofauti za kijamii na kiuchumi zinazokumba bara la Afrika.”

Viongozi wa kidini Afrika wajadili masuala yanayotazama bara lao na changamoto zake
09 August 2023, 14:49