Tafuta

Kardinali Marengo na Balozi wa Vatican nchini Mongolia. Kardinali Marengo na Balozi wa Vatican nchini Mongolia. 

Kard.Marengo,Balozi wa Ulaanbaatar:kuna wakatoliki 1,500 huko Mongolia

Kadinali Giorgio Marengo, mmisionari wa Consolata na Balozi wa Vatican huko Ulaanbaatar anaelezea katika ripoti ya video kuwa nchi hiyo ni yenye utamaduni wa muda mrefu wa shamanic na Buddha na pia kwa kiasi fulani kiroho cha Kiislamu mara moja ilijiimarisha yenyewe kwa utajiri huu mkubwa ambao ukawaita wamisionari Wakatoliki pia.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

“Nilikutana na viongozi wa Mongolia na wakanihakikishia kwamba Katiba mpya inahakikisha huwepo wa wingi wa kidini na kwamba dini zote na madhehebu yote yatakaribishwa. Jambo la kufurahisha ni kwamba hadi sasa kati ya Wamongolia zaidi ya milioni mbili hakuna Mkristo hata mmoja. Namaanisha moja ya idadi. Kwa hiyo, mwezi Aprili 1992, mmisionari mkubwa wa Ubelgiji na mtaalamu wa dhambi Jerome Heyndrickx, aliyekuwa mkuu wa Provinsi ya Shirika la Wamisionari wa  Scheuts, alisimulia mambo fulani yenye kupendeza ya safari yake aliyofanya mnamo Oktoba 1991, alipokwenda Ulaanbaatar kuanzisha utume wa kwanza Katoliki nchini Mongolia, baada ya viongozi wa nchi hiyo kuomba kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia na Vatican.

Ni wakatoliki 1500 nchini Mongolia 

Hata leo, hii takriban Wakatoliki 1,500 wa Kimongolia wanawakilisha jumuiya ndogo katika idadi ya watu ambao wengi wao wanadai  ni Ubudha wa Lamaist. Kulingana na sensa ya kitaifa ya mnamo mwaka  2020, asilimia  52% ya taifa ni Wabuddha, 41% wanadai kutokuwa  na dini na asilimia  3.2% ni Waislamu. Na kazi yote ya kimisionari ambayo imestawi nchini Mongolia katika miongo ya hivi karibuni imekuwa na uwazi wa kukutana na waamini wa imani nyingine kama kipengele muhimu cha kimuundo, kama inavyothibitishwa na ripoti ya tano ya video iliyotolewa na shirika la habari za Kimisionari  Fides na Teresa Tseng Kuang yi katika mtazamo wa Ziara ya Kitume ya Baba Mtakatifu Franciskokwenda Mongolia kuanzia tarehe 31 Agosti hadi tarehe 4 Septemba 2023.

Kardinali Marengo Msimamizi wa Kitume huko Ulaanbaatar nchini Mongolia anafanua kuhusu dini

Katika video hiyo, Kardinali Giorgio Marengo, Mmisionari wa Consolata na Msimamizi wa Kitume wa Vatican huko Ulaanbaatar, anabainisha kuwa Mongolia ni “kama nchi yenye mapokeo marefu ya hali ya kiroho ya kishamani na Kibudha, na pia kwa kiasi fulani ya Kiislamu"ilijiimarisha mara moja kwa sababu ya utajiri huu mkubwa"ambao mara moja uliwavutia wamisionari Wakatoliki pia. Wingi wa kidini ambao wamisionari wanaume na wanawake wamejifunza kujua, kusoma na kuthamini, katika mazungumzo ambayo yamekua kwa wakati, na pia imechukua mtindo wa  mazoea ya kuongezeka kwa mikutano ya mara kwa mara na wawakilishi wa imani zingine. Kwa miaka miwili, mikutano ya kuishi pamoja na mazungumzo baina ya dini mbalimbali imekuwa ikifanyika kila baada ya miezi miwili. Na wakati wa mikutano - mandhari ya maslahi ya kawaida na pia matatizo yanachunguzwa, uwezekano wa ufumbuzi wa pamoja, na mipango ya pamoja inakuzwa, hasa katika uwanja wa hisani ambao ni upendo wa kujitolea.” Alisisitza Kardinali Marengo katika ripoti kwa njia ya video.

Hata marafiki wawakilishi wa tamaduni na mila nyingi wana heshima kwa Baba Mtakatifu

Uzoefu wa urafiki na ushirikiano kati ya waamini wa jumuiya tofauti za kidini, mbali na ufupisho wowote, una athari za kivitendo zinazojionesha kuishi pamoja kitaifa. Uzoefu huu unaonesha kwamba kila utamaduni wa kweli na wa  kidini ya kweli huchangia kwa njia yake katika ukuaji wa jamii. Na  tamaduni  mbalimbali za kidini si tishio katika utofauti wao, lakini zikifanikiwa kuwiana vyema wao kwa wao ni rasilimali kwa kila jamii, kwa Serikali. Kama utajiri ambao tunaweka katika mazungumzo, na kuzunguka kati yetu,” alisisitiza Mkuu wa kitume huko  Ulaanbaatar Kwa njia hiyo Mikutano ambayo Papa Francisko atakuwa nayo na viongozi wa kidini katika safari yake ijayo nchini Mongolia itaweza kuwafariji na kuwathibitisha wamisionari wa Kimongolia na jumuiya za Kikatoliki katika safari yao ya udugu na ukaribu na wamini wa imani nyingine. Kardinali Marengo katika ripoti kwa njia ya video  alithibitisha kwamba: “Tunajua kuwa hata marafiki na wawakilishi wa tamaduni na mila zingine za kidini wana heshima kubwa na kuvutiwa na Baba Mtakatifu.”

Kardinali Marengo anaelezea kuhusu dini nchini Mongolia
23 August 2023, 16:34