Tafuta

Mtakatifu Clara wa Assisi. Mtakatifu Clara wa Assisi. 

11 Agosti:Siku kuu ya Mtakatifu Clara wa Assisi,mche wa Bwana!

Kila tarehe 11 Agosti Mama Kanisa anakumbuka Mtakatifu Clara wa Assisi.Kijana mdogo aliyekimbia kumfuata Yesu Kristo kwa njia ya umaskini kabisa,alifuatiwa na dada zake Agnes,Beatrice na hatimaye Mama Mama yake Ortolana katika Monasteri ya Mtakatifu Damiano.Ni dada yake pekee Penenda kati ya wanne aliyeolewa

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Mtakatifu Clara kijana aliyemuiga Mtakatifu Francis katika kukumbatia umaskini kabisa, ishara ya Yesu aliye hai kwa kila mmoja aliye mdogo. Clara alItambuliKa kama “mmea mdogo wa Bwana” kupitia  wimbo: “Chiara, mtamu, mmea mdogo wa Bwana, Chiara, hua wa upendo. Pamoja na Francis na Dada Umaskini unaikana dunia na ubatili wake.”Kwa njia hiyo kila tarehe 11 Agosti, Mama Kanisa anamkumbuka Mtakatifu Clara wa Asssi. Clara alizaliwa huko Assisi, Italia mnamo 1193, katika familia mashuhuri ya Favarone ya Offreducci. Alikuwa bado mtoto wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipozuka katika jiji hilo kati ya wakuu na wabepari na Clara  alilazimika kukimbia, pamoja na familia yake, huko Perugia kilomita chache kutoka Assisi, ambapo alibaki hadi ujana wake. Huko Assisi, akiwa na hamu ya kuwa wa Kristo pekee yake na kuvutiwa na mfano wa Mtakatifu Francis wa Assisi, usiku wa kuamkia Dominika ya Matawi mnamo mwaka 1212 alitoroka nyumbani kwa baba yake kupitia mlango wa nyuma na akaenda huko  Porziuncola, mahali ambapo alikumbatia mfumo wa maisha ya kiinjili katika nyayo za Bwana Yesu Kristo, lakini pia alifuatiwa na mama yake mzazi na dada zake Beatrice, na Agnes ambao walikuwa watawa pia katika monastri hiyo.

Kanisa la Mtakatifu Clara huko Assisi mahali wanapoishi Waclara na kaburi lake
Kanisa la Mtakatifu Clara huko Assisi mahali wanapoishi Waclara na kaburi lake

Mtakatifu Francis wa Assisi ndiye aliyemkata nywele zake na kumfanya avae mavazi ya Wafransiskani, maskini kabisa na kisha kumpeleka kwenye monasteri ya Wabenediktini ya Mtakatifu Paolo, huko Bastia Umbra, kwa sababu wakati huo, Francis hakuwa na sehemu ya kumweka kijana msichana aliyejiunga na ufukara huo. Akiwa huko baba yake mara moja alijaribu kumshawishi kuacha utawa lakini bila mafanikio ya kurudi nyumbani. Baadaye Mtakatifu Francis alimpeleka huko Mtakatifu Damiano, ambako ndipo aliunda shirika la kike la kimasikini likaitwa Watawa wa ndani Maskini wa Waklara na Clara akawa  ndiye Mkuu wa Kwanza wa Shirika hilo(Abadessa) kwa kuteuliwa na Francis mwenyewe na kuwa na  kanuni ya kwanza. Lakini baadaye, Clara aliandika Kanuni ya uhakika  huku akiomba na kupata ruhusa kutoka  kwa Papa Gregory IX kuhusu mapendeleo ya umaskini  kabisa ambayo ilikuwa ni ngumu sana. Maisha ya Clara kwa hiyo yaliteketezwa kama mshumaa ndogo unaowaka katika uwanja mdogo wa monasteri ya Mtakatifu Damiano, huku akifuata  kwa  furaha  Injili ya Kristo maskini na msulubiwa.

Kanisa la Mtakatifu Clara na eneo lake huko Assisi.
Kanisa la Mtakatifu Clara na eneo lake huko Assisi.

Ni katika kuishi maisha rahisi, ya bidii na ya kidugu, na kwa njia ya umaskini, alijifungulia kabisa katika  fumbo la Mungu. Zawadi ya udugu yalikuwa ni  matunda ya njia hiyo ambayo pamoja naye ulizaliwa mfumo mpya wa maisha ya Dada Maskini ambao  hadi leo hii tunawaita Waclara wa Ndani.  Akiwa na  umri wa miaka thelathini, Clara  alianza kuugua  ugonjwa ambao ulimudu kwa mrefu  karibu miaka arobaini na ambao ulimfanya kuwa dhaifu. Pamoja na hayo, lakini aliendelea kuwa mama mwenye kujali, kiongozi mwenye busara na kielelezo cha maisha ya kweli ya Kiinjili kwa dada zake watawa.

Historia ya Mtakatifu Clara sehemu I

Ilikuwa mnano tarehe 11 Agosti 1253, huko Mtakatifu Damiano Assisi, Clara aliitwa na Mwenyezi Mungu kuelekea mbinguni, huku akisherehekea zawadi ya uhai na ambapo mwandishi wake anaandika maneno haya ya mwisho: “Nenda salama, kwa amani, roho yangu iliyobarikiwa, kwa sababu una msindikizaji mzuri katika safari yako! Hakika aliyekuumba, amekufanya kuwa mtakatifu na, akikutazama kama mama wa mtoto wake mdogo, alikupenda kwa upendo mpole. Na wewe, Bwana, uhimidiwe kwa sababu uliniumba”. Hata hivyo pamoja Kanuni ya Shirika hilo , Mtakatifu Clara aliacha pia Baraka na Barua nne zilizoelekezwa kwa Mtakatifu Agnes wa Prague. Tukirudi nyuma kuhusu kuishi umaskini wa dhati, Kardinali Ugolino, aliyekuwa Askofu wa Ostia na msimamizi wa watoto wadogo, alimpatia sheria mpya ambayo ilikuwa ikipunguza ukali wa kuishi umaskini, lakini Clara  hakuwa amekubali punguzo hilo hivyo Kardinali Ugolino, ambaye pia alikuja kuwa Papa Gregory IX (1227-41) alimpatia tena  ruhusa ya upendeleo wa kuishi umaskini  kama ilivyokuwa imekwisha thibitishwa na Papa Innocent IV na Hati kuu ya  1253, iliyowasilishwa kwa Clara siku chache kabla ya kifo chake.

Ugumu daima

Katika moja ya maandishi ya barua (hapa katika tafsiri ya kisasa) kwa Agnes wa Praga binti wa mfalme wa Bohemia, kuhusu ugumu wa kuishi maisha ya kimasikini ambapo  kulitokea shida kali ya monasteri iliyochochewa na wazo bora la Wafransiskani la umaskini. Katika Barua ya Clara ya ushaur aliyotuma ya upendo na ya wazi aliandika kuwa: “Lakini hata  hivyo hatuna mwili wa shaba, wala wetu si uimara wa punje. Nakuomba ujidhibiti kwa busara katika ukali uliokithiri na usiowezekana ambao najua umejiingiza.” Katika hilo hakika Agnese alipaswa kuona jinsi gani Clara alivyojua jinsi ya kutoa hata huduma za unyenyekevu na zisizopendeza kwa dada zake wagonjwa, lakini bila kupoteza tabasamu lake na bila kuruhusu lipotee.

Clara ni Msimamizi wa Televisheni

Mnamo tarehe 17 Februari 1958, Papa Pio XII alimtangaza kuwa msimamizi wa televisheni na mawasiliano ya simu. Kulingana na mila utamaduni, ilikuwa siku ya Noeli wakati wa misa iliyohudumiwa na Mtakatifu Francis, lakini Clara hakuwepo, katika tukio hilo,  kwa sababu kama tulivyosema alikuwa amelazwa kitandani kwa sababu ya udhaifu wake. Kwa kutaka kushiriki katika sherehe hata hivyo, kumbukumbu zinasema kwamba maono ya misa hiyo yalimtokea na wakati komunio, malaika alijiwasilisha mbele yake ambaye alimpatia  uwezekano wa kushiriki mkate uliobarikiwa.

Clara na Muujiza wa Ekaristi

Mtakatifu Clara hadi leo hii  alijitofautisha kwa kujitolea kwake kwa ajili ya Ekaristi. Na mara nyingi anaoneshwa akiwa ameshikiria monstrance. Hii ni kwa sababu katika historia ya enzi za kati nchini Italia  ambapo mara mbili huko Assisi ilitishiwa na  jeshi la Mtawala Frederick II ambaye aliyekuwa anahesabiwa kuwa katili kati ya askari wake, pia Wasaracens. Mtakatifu Clara akiwa, mgonjwa wakati huo, walipavamia Monasteri yao, alipeleka kwenye kuta za jiji akiwa ameshikilia (monstance iliyokuwa na Sakramenti Takatifu mkononi mwake. Waandishi wa wasifu wake wanasema kwamba jeshi, wakati huo, lilikimbia. Kwa hiyo tangu wakati huo, tukio hilo hukumbukwa na kuadhimishwa huko Assisi katika siku kuu kubwa ya  Waklara Maskini, kila ifikapo tarehe 22 Juni ya kila mwaka.

Clara na dada zake Penenda, Agnes na Beatrice

Hapo mwanzo niliwambia kuwa Mama yake Mtakatifu Clara na dada zake walijiunga na shirika la Waclara. Kwa maana hiyo walikuwa ni  binti wa tatu kati ya watoto wanne wa Bwana Favarone Offreduccio Scifi, ambapo katika monasteri alitangulian Clara, Penenda pekee yake kati yao aliyeolewa, akifuatiwa na Beatrice wa Assisi, ambaye  baadaye  alijiunga na dada huko Mtakatifu  Damiano na mama yake. Kwa njia hiyo dada yake Clara kwa  jina lake halisi, aliitwa Caterina ambalo  lilibadilishwa na Clara mwenyewe wakati wa kufunga Nadhiri za Kitawa kama ilivyotumika kipindi kile cha enzi hizo. Kwa hiyo Caterina, anayejulikana kama Agnese wa Assisi, alizaliwa mnamo 1197. Katika mkutdha huo tunaweza kusema  Mama yake Ortolana (aliyeheshimiwa kama mtumishi wa Mungu na Kanisa Katoliki) alikuwa wa familia tukufu ya Mito na binamu yake Rufino alikuwa mmoja wa Wenzake wa tatu wa kwanza wa Mtakatifu Francis wa Assisi. Utoto wa Agnese ulipitia kati ya jumba la baba yake jijini na lile la Sasso Rosso kwenye Mlima wa  Subasio. Tarehe 18 Machi 1212, dada yake mkubwa Clara, akichochewa na mahubiri na mfano wa Mtakatifu Francis, aliondoka naye nyumbani kwa baba yake ili kufuata mafundisho yake. Siku kumi na sita baadaye, kulingana na historia nyingine zinabainisha kuwa alikimbilia katika nyumba ya watawa ya Mtakatifu Angelo huko Panzo, ambapo watawa wa Benediktini walikuwa wametoa kimbilio kwa Mtakatifu Clara na aliamua kushiriki maisha ya dada yake ya umaskini na toba.

Historia ya Mtakatifu Clara sehemu II

Akiwa amekasirishwa na uamuzi huu, kulingana na kile kinachosimuliwa kwa undani katika Simulizi ya Mambo ya Nyakati za Wakuu  Ishirini na Wanne,(wa shirika la Ndugu wadogo OFM) baba yake  alimtuma kaka yake Monaldo pamoja na jamaa fulani na watu wenye silaha kwenda kwenye monasteri ya Mtakatifu Angelo ili kumlazimisha Agnese arudi, au kumshawishi lakini haikutosha kurudi Nyumbani. Historia  inasimulia jinsi ambavyo mjomba wake Monaldo, kando yake kwa hasira, alichomoa upanga wake ili kumpiga msichana huyo bila kufanikiwa katika dhamira yake. Kiukweli, mkono wake ulianguka, bila nguvu, kando ya upande; wengine baadaye wakamkokota Agnese, wakamshika kwa kumvuta nywele zake, kutoka nje ya nyumba ya watawa na kumpiga mateke mara kwa mara. Clara alifika mara moja kumuokoa lakini ghafla mwili wa Agnese ukawa mzito kiasi kwamba hata askari walijaribu kumbeba bila mafanikio. Mwishowe walimwacha, akiwa nusu mfu, katika shamba karibu na nyumba ya watawa. Kulingana na historia hiyo, jamaa zake Agnese walilazimika kujiondoa na kumruhusu kukaa na dada yake Clara, akizidiwa na nguvu ya kiroho ambayo nguvu za mwili hazingeweza kufanya chochote. Agnese alifariki mnamo tarehe 16 Novemba 1253, ambapo alikuwa tayari ni Mkuu wa Monasteri ya  Monticelli,  mahali ambapo alianzisha   hata monasteri nyingi za wanawake maskini katikati mwa Italia. Na mnamo 1752 Papa Benedikto XIV aliruhusu kutambuliwa  kama Mtakatifu.

Beatrice ni dada yake Clara

Kwa upande wa dada yake mwingine wa Mtakatifu Clara, Beatrice,  tunapaswa kurudi nyuma tena katika hisotoria. Ujenzi wa Kanisa na nyumba ndogo ya Waklara Maskini katika Eneo la Rieti ulianza mnamo mwaka 1237 katika eneo liitwalo ‘Voto dei Santi;’ ambapo inasadikika  kwamba mwanzilishi alikuwa Mwanamke Isabella Savelli, (aliyekuwa mwanamke mashuhuri wa wakati huo). Jumuiya ya kwanza ya Maskini Waclara ilianzishwa Rieti mnamo tarehe 3 Septemba 1236 baada ya kupata  idhini ya Upapa na pia alifungua monasteri ya Mtakatifu Agnese. Shukrani kwa mwenyeheri Angelo Tancredi, mmoja wa Ndugu Wadogo kumi na wawili wa kwanza wafuasi wa  Mtakatifu Francis wa Assisi, ambaye kiukweli alijitahidi kuanzisha monasteri halisi kutoka katika jengo ndogo la awali. Baada ya kupata jengo moja la Mtakatifu Lucia, huko Rieti kutoka kwa Askofu Tommaso, shukrani kwa sadaka na wafadhili  zilizokusanywa, Ndugu Mdogo Tancredi (OFM) alianza kazi za upanuzi wa Jengo hilo. Mnamo mwaka 1253, mara tu ujenzi ulipokamilika, Ndugu Mdogo Tancredi alikimbia hadi Assisi ili kutangaza habari njema hiyo kwa Mtakatifu Clara ambaye alipata  wakati wa kufurahi kabla ya kifo chake.  Na ili kueneza hali ya kiroho ya Wafransiskani, Mtakatifu Clara alimtuma mdogo wake Beatrice huko Rieti ambaye alikaa katika monasteri kwa muda wa miezi minane na ambaye, pamoja na Ndugu mdogo Angelo Tancredi(OFM), walifuata jumuiya ambayo tangu wakati huo ilizingatiwa kuwa kama mwaanzilishi wake mkuu. Ikumbukwe kwa hiyo Nyumba ya watawa Waclara ilikuwa nje ya kuta za Rieti, lakini kwa kufuata masharti ya Baraza la Trento, mnamo 1575 ilihamishiwa ndani ya jiji la Rieti. Na watawa hao Waclara walidumu kwa maisha ya ndani hadi walipobadilisha kuwa na maisha ya huduma za nje na kusali na wakaitwa Shirika la Masisita Waklara wa Mitume mnamo 1929 huko Rieti kutokana na hitaji la huduma kwa maskini lililojitokeza enzi hiyo.

Mama yake Clara Ortolana

Baada ya kusimulia historia za dada hao wanne wa Assisi kuanzia na Clara, Penenda, Agnes na Beatrice,  basi hebu tuone  Mama yao Ortolana.  Huyu kiukweli hakuwa mwanamke wa hivi hivi tu, bali alitoka katika familia ya kiungwana, na alikuwa ameolewa na Favarone, mshiriki wa moja ya familia muhimu zaidi huko Assisi, Italia. Alikuwa amesafiri sana kwa safari ndefu, ambazo zilimpeleka kuanzia Roma, hadi Mtakatifu Yakobo  wa Compostela huko Hispania, Mtakatifu  Mikaeli huko  Gargano na pia kwenye Nchi Takatifu. Hizi zilikuwa hija za kiutamaduni za karne ya 12 na 13 ambazo zilikuwa safari ndefu zilizojaa matukio yasiyotarajiwa, na ambayo mwanamke angeweza tu kujitolea ikiwa angetegemea kampuni na msaada wa wanawake wengine kama(wanafamilia, marafiki, wanawake ambao waliishi katika mtaa mmoja kwa kusaidiana). Alipokuwa akiondoka kwenda kuhiji, majirani zake vijana walimfuata, pengine wakiwa na kazi ya kumtunza na kumsaidia mwenyewe. Hata hivyo katika wasifu wa Clara sura ya baba yake inaonekana kidogo, pia kwa sababu mara nyingi hakuwepo nyumbani, huku ile ya mama yake Ortolana ikioneshwa na kuwekwa umuhimu wake wote kama mama. Kiukweli alikabidhiwa usimamizi wote wa nyumba, ambayo atakuwa kitovu cha familia na mwalimu wa moja kwa moja wa binti zake watatu: Clara, Caterina (ambaye baadaye atapokea jina la Agnese kutoka Francis) na Beatrice, kukumbuka dada mwingine Penenda  pekee aliyeolewa.

Utabiri uliotimilizika

Mazingira mazuri ya familia yanaashiria na kumaanisha kwa sura ya  Ortolana kwa upande mmoja fikra ya kike na ya mama, ambayo ilijidhihirisha katika utunzaji wa vitendo wa kazi za nyumbani, ngumu katika nyumba iliyo wazi kwa ukuu wa Assisi, na kwa upande mwingine umakini mkubwa kwa malezi ya kibinadamu na kidini ya familia. Majukumu haya yalioanishwa vyema na kila mmoja, hivi kwamba Ortolana alikuwa na wakati uliobaki wa kuhiji sehemu za mbali na kujitolea kwa masikini mjini. Ni yeye ambaye alionesha jina la kumpatia Clara, akichagua moja ya majina yasiyo ya  kawaida kabisa katika familia yake. Labda alitaka kuthibitisha  kwa jina, utabiri ambao aliupata kabla ya kujifunga mtto huyo, wakati, alipokuwa akimwomba Bwana, sauti ilikuwa imemtangazia kwamba “angezaa nuru kuu, ambayo itadhihirisha sana katika ulimwengu”. Kwa hiyo kwa kupata nuru ya unabii huu , alitaka mtoto mchanga, aliyezaliwa upya kwenye kisima cha ubatizo, aitwe Clara, akitumaini kwamba kwa njia fulani baadaye uwazi ulioahidiwa wa nuru ungetimizwa, kulingana na mpango wa upendo wa  mapenzi ya Mungu. 

Heri yeye jaye kwa jina la Bwana

Daima alikuwa ni Mama yake Ortolana ambaye alitazama kwa huruma juu ya maisha mapya yaliyofanywa na binti yake. Alikuwa yeye, hatimaye, ambaye alimfuata baada ya miaka kadhaa. Kwa hiyo ilikuwa tena ni Dominika ya Matawi, Ortolana pia aliungana na binti zake watatu, Clara, Agnese, Beatrice huko Mtakatifu  Damiano, na kukaa nao na kujitolea kutunza bustani ya watawa. Hata hivyo jina lake ‘Ortolana’, kwa kiitaliano linamaanisha ukweli  kama Bustani, lilivyopendekezwa na Clara. Baada ya kuandika wosia wake (ambao Monaldo ataupata na kutekeleza bila kupinga, kwa sababu yeye hakua katili  tena wa miaka michache iliyokuwa imepita) na barua ya kuaga kwa jamaa zake, ambao walisalia, Ortolana  aliacha maisha yake kawaidia yakiwa yamejaa huko Assisi yenye heshima milele ma kusifiwa na kuheshimiwa. Clara alimkaribisha kwa naneno  kuwa:  “Heri yeye ajaye kwa jina la Bwana.”

Historia ya Mtakatifu Clara, mama yake na dada zake:Agnes,Beatrice na Penenda
11 August 2023, 11:39