Tafuta

2023.07.29 Wanahia vijana kutoka Brazil walipitia mjini Vatican  wakielekea Lisbon katika maadhimisho ya Siku ya vijana 2023. 2023.07.29 Wanahia vijana kutoka Brazil walipitia mjini Vatican wakielekea Lisbon katika maadhimisho ya Siku ya vijana 2023. 

WYD2023:kutoka Brazil hadi Lisbon kwa kukutana na Kristo kijana

Kuna takriban vijana ishirini wanaowakilisha harakati zilizopo katika jimbo kuu la kaskazini mwa Brazili,kwenye malango ya Amazonia,waliowasili Lisbon tarehe 30 Julai 2023 wakisindikizwa na askofu msaidizi Ribeiro.Walitoa ushuhuda wa huduma ya vijana inayokua,yenye nguvu zaidi,iliyo wazi walipotembelea studio za Radio Vatican.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mahujaji jijini Roma wakiwa njiani kuelekea Siku ya Vijana WYD huko Lisbon walitembelea hata Studio za Radio Vatican. Chaguo la vikundi vingi vya vijana kutoka ulimwenguni,pia linashirikishwa na wasichana na wavulana 19 wa Brazil kutoka jimbo kuu la Belem, katika jimbo la kaskazini la Parà, lango la Amazon. Wakiwa wameandamana na askofu wao msaidizi, Msalesiani Askofu  Antonio de Assis Ribeiro, mjumbe wa huduma ya vijana na kijamii na anayewakilisha harakati na vyama vyote vya Kikatoliki vya Belem, walitembelea jijini Roma kuanzia tarehe 23 hadi 30 Julai 2023. Walijiandaa kwa zaidi ya mwaka mmoja na mikutano ya kila mwezi, ambayo iliunda timu halisi, Kama alivyoeleza Graciete Cardoso, mfanyakazi wa kujitolea katika sekta ya vijana ya jimbo kuu, ambaye alisoma katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Salesian jijini Roma.

Watashuhudia ujumbe watakaoupata wakirudi baada ya WYD

Ni kweli kwamba wameshiriki katika mikutano ya sekta, hata ya kitaifa, na vijana kutoka kote Brazil  lakini WYD ni ya kipekee, kwa sababu watakutana na vijana kutoka duniani kote, na Papa Francisko ambaye ni hatua yao ya kumbukumbu na ambaye atawapatia ujumbe mmoja muhimu, ambao wanatazamia kwa hamu, kwa sababu yeye ndiye Baba wa Kanisa. “Kubadilishana huku na vijana wengi kutaboresha maisha yetu”, walisisitza na pia wanatazamia kupokea utajiri huo. Kwa sababu wanafikiri kwamba hawatakuwa sawa na  walivyo baada ya Siku hii ya Vijana Duniani.  

Kikundi cha vijana wa Brazil wakiwa Uwanja wa Ndege Fiumicino kuelekea Lisbon
Kikundi cha vijana wa Brazil wakiwa Uwanja wa Ndege Fiumicino kuelekea Lisbon

Wana imani kwamba watarudi nchini Brazil wakiwa na uhakika kwamba kujitolea na juhudi zinastahili,  kama alivyo sisitiza Eduarda Sanches, naibu mratibu wa sekta ya vijana wa Jimbo  kuu la Belem na kwamba mapadre wao waliwambia  wakati wote wa maandalizi, na ni Kweli. “Nadhani vijana wa siku hizi, sio tu nchini Brazili bali ulimwenguni kote, lazima wajifunze kuthamini kazi na jasho lao”. Eduarda anatumaini kuwa kutakuwa na mahujaji wengi zaidi vijana kutoka Belem ili kupata uzoefu wa WYD ijayo, “shukrani kwa ujumbe ambao tutasambaza tukirudi”.

Vijana wa Brazil walipitia jijini Roma kabla ya kwenda Lisbon na pia studi za Radio Vatican
31 July 2023, 15:38