Tafuta

Watawa wamefanya mengi katika malezi bora ya watoto. Watawa wamefanya mengi katika malezi bora ya watoto. 

Warsha ya mpango wa malezi ya kikatoliki,Fr.Makunde:Masista wawe marubani na madereva!

Tunafahamu kwamba Masista tayari wanafahamu mchakato huu na wamefanya mengi katika malezi ya watoto na marekebisho ya malezi na tunashukuru kwa hilo.Alisema hayo Padre Makunde,Katibu Mkuu wa AMECEA katika warsha ya Wasimamizi wa Mpango wa Malezi ya Kikatoliki ya Watoto kutoka nchi nne ndani ya AMECEA,huko Kampala,Uganda.

Sr. Jecinter Antoinette Okoth, FSSA - AMECEA & Angella Rwezaula, - Vatican.

Wakati makundi mbalimbali yakiwemo ya Kanisa, serikali na asasi za kiraia zikitafakari kwa  upya juu ya malezi ya watoto mbali na malezi ya kitaasisi,  lakini kwa kujikita zaidi ya  malezi ya familia na jamii, Katibu Mkuu Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika Mashariki (AMECEA) aliwashauri watawa wa kike kuwa  mstari wa mbele kwa ajili ya utambuzi wa ndoto hiyo katika kanda. Hawa walikuwa ni Wasimamizi wa Mpango wa Malezi ya Kikatoliki ya Watoto (CCC) kutoka nchi nne ndani ya kanda ya AMECEA waliokusanyika mjini Kampala, Uganda, kuanzia  tarehe 4 Julai 2023 ili kutafakari kwa kina juu ya mpango  uliozinduliwa hivi karibuni wa tafiti za kimsingi zilizopewa jina: ‘picha ya kikanda. Kwa maana hiyo katika ufunguzi wa warsha hiyo, Padre Anthony Makunde alikiri  na kusisitiza hatua hiyo ambayo tayari imeanzishwa na Masista wa Kikatoliki na kuwapongeza katika kuongoza mchakato wa mageuzi katika nchi zao. Padre Makunde alisema: “Tunafahamu kwamba Masista tayari wanafahamu mchakato huu na wamefanya mengi katika malezi ya watoto na marekebisho ya malezi na tunashukuru kwa hilo. Katika kesi hii, ilisifiwa na maaskofu katika uzinduzi wa picha katika Hoteli ya Boma jijini Nairobi kwamba Masista wawe marubani na madereva huku maaskofu, watawa wa kiume na makasisi wakiiga mfano wao.”

Jitihada za kukuza mpango wa malezi kikatoliki

Wakati Masista wakiongoza mchakato huo, Katibu Mkuu alisisitiza, “Tunapaswa kusaidiana na kufanya hili kuwa la kikanda na pia kufikia wengine ... na kuja na mpango kazi ili utume huu  uweze kukamilika kwa mafanikio.” Akisisitiza juu ya lengo la warsha la siku tatu kuanzia tarehe 4-6, Julai 2023, iliyowaleta pamoja wawakilishi kutoka nchini Uganda, Kenya, Zambia na Malawi, Padre Makunde ambaye amekuwaKatibu Mkuu wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Afrika Mashariki (AMECEA)tangu mwaka 2018 alisema kuwa: “Tupo hapa kuendelea kujenga kutokana na msingi mzuri uliowekwa na wadau kadhaa hasa watawa katika mpango huu wa kulea watoto. Sasa inakua polepole na tunatazamia nchi zilizosalia ndani ya kanda za AMECEA na ACWECA ambacho ni Chama cha Watawa Afrika Mashariki na Kati kuwamo.” Padre Makunde aidha alisisitiza kuwa "nchi zilizosalia sio tu za kujiunga na mchakato wa mageuzi ya malezi kwa ajili yake, bali zinapaswa kuelewa kwamba wanao wajibu wa kusoma alama za nyakati,na kulea watoto katika familia ni miongoni mwa  ishara hizo." Na wakati huo huo, “Tuna wajibu si kwa sababu ni mpango, bali ni dhamira ya kuwa na au bila mpango,” alisema kuhani huyo wa Tanzania na kuongeza kuwa washiriki wakati wa warsha hiyo watapitia upya utafiti wa awali ambao tayari umefanywa katika nchi hizo nne ili kuelewa hali ilivyo katika mkono.

Ripoti ya picha halisi ya kanda la AMECEA

Akiwa mshikiri wa washiriki wa Warsha hiyo kupitia ripoti ya picha halisi za kanda, Mratibu wa Mawasiliano wa AMECEA, Padre Andrew Kaufa, alisisitiza kwamba takwimu kutoka katika tafiti za kimsingi ni muhimu kwa Kanisa kufanya maamuzi yenye msingi wa ushuhuda, kushughulikia matatizo yanayojitokeza na kwa mpango wa Malezi kikatoliki ya Watoto (Catholic Care of Children, CCC)kutathmini kwa uwazi utendaji. “Wakati picha halisi ya kikanda inatoa kama ripoti juu ya hatua iliyofikiwa hadi sasa katika kuhama kutoka katika malezi ya kitaasisi kwa watoto na kujikita kama kituo chetu cha kuzingatia mazingira ya familia, picha hiyo pia inaonesha umuhimu wa Malezi Kikatoliki ya  Watoto, kuthamini takwimu na kuwa na mazungumzo na picha halisi; kuchukua ushuhuda  kama chombo cha sisi kutafiti mioyo na akili za wadau wetu ambao ni pamoja na mawakala wa kichungaji, wanaume watawa, watunga sera, wasomi, Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo na washirika wa ufadhili; na kwa Malezi Kikatoliki ya Watoto(CCC) binafsi kutambua na kutafsiri mapengo ndani ya nchi yao kuwa vituo vinavyowezakutekeleza kutokana na mtazamo wao wa ndani,” alisema Padre  Kaufa.

Maazimio ya kuwajengea uwezo wa wafanyakazi wao

Baada ya kutoa maoni yao kuhusu picha halisi ya kanda  kwa kunasa viwezeshaji, Mbinu bora, mapungufu, masimamizi wa mpango wa Malezi Kikatoliki ya Watoto kwa pande nne, washiriki hao wa Warsha waliazimia kuja na mikakati itakayohakikisha kuwa wadau wote wanashirikishwa katika mchakato huo, ili kuwajengea uwezo wafanyakazi wao na kuhakikisha kuwa familia zinaimarishwa kwa kuzingatia malezi ya watoto.

AMECEA: Warsha kuhusu Malezi ya Watoto Kikatoliki huko Kampala Uganda.
11 July 2023, 13:19