WYD,Lisbon 2023:Vijana wa majimbo 10 kati ya 15 nchini Ivory Coast wako tayari kwa WYD
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Padre Régis Akpess ni mkuu wa kijimbo wa Mashirika ya Kimissionari ya Kipapa (PMS) huko Yopougon, mojawapo ya majimbo kumi ya Ivory Coast yatakayoshiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani huko Lisbon kuanzia tarehe 1 -6 Agosti ambayo yanaongozwa na Kauli mbiu “Maria aliondoka akaenda kwa haraka” (Lk 1:39). Na ambaye akihojiana na Shirika la Habari za Kisionaria Fides kuhusiana na tukio hili muhimu alisema: “Wakati Askofu wangu, Jean Salomon Lezoutié, aliponiomba niandamane na vijana hadi Lisbon katika Siku ya Vijana Ulimwenguni, nilikubali kwa shukrani na furaha kubwa!
Mmisionari wa Ivory Coast, ambaye ni wa jimbo la Yopougon aliongeza kusema kuwa “Sisi ni kundi la mapadre, watawa, vijana wa kike na kiume kutoka majimbo 10 kati ya 15 ambayo ni ya Kanisa la Ivory Coast. Tulifika Portimao, Ureno, Alhamisi tarehe 20 Julai 2023 na kisha tukaelekea Lisbon ambako tutakaa wiki moja tukisubiri Misa na Papa Francisko”, alieleza Padre Regis. Kwa kuongezea, “Katika mwaka huu vijana walishiriki katika mikutano mbalimbali ya maandalizi iliyoandaliwa na Sekretarieti ya Kitaifa ya Mashirika ya Kimissionari ya Kipapa. Washiriki wote walijiandikisha kwa shauku kwa ajili ya Siku ya vjana (WYD) hii ambayo wanaiona kuwa tukio la ajabu la maombi na mikutano”. Na zaidi alisema “Jimbo la Yopougon lina kanisa lilip ha ambal linajumuisha takriban 45 harakati, makundi na vyama vya sala”. Kwa hiyo majimbo 10 yanayowakilisha katika Siku ya vijana (WYD) huko Lisbon ni yale ya: Abidjan, Yopougon, Bassam, Mtakatifu Pedro, Abengourou, Agboville, Katiola, Korogho, Daloa, na Bouaké.”