Tafuta

2023.07.26 Kivumbi na jasho huko Lisbon. Mkutano wa vijana mara nyingi huwafanya wakue katika kuchukua maamuzi mazito ya kufuata. 2023.07.26 Kivumbi na jasho huko Lisbon. Mkutano wa vijana mara nyingi huwafanya wakue katika kuchukua maamuzi mazito ya kufuata. 

Mexico,WYD:Ask.Villareal,Mikutano kama WYD hufanya vijana kukaribia Kristo!

Askofu Msadizi Villareal anaamini kwamba kunaweza kuwa na karibu vijana 30,000 watakaokuwa huko Ureno kutoka Mexico.Kati ya majimbo tisini ya Mexico,vijana 200 na 500 kwa kila Jimbo wamejiandikisha kama ilivyoripoti Ofisi ya kichungaji ya vijana majimbo na kama vikundi vya watu binafsi pia.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Siku ya Vijana Duniani inawakilisha uzoefu mkubwa wa kukutana ambayo inasaidia vijana wengi kuhuisha imani yao, alisema  hayo Askofu Héctor Pérez, msaidizi wa Jimbo kuu la Mji wa Mexico. Katika mahojiano na Shirika la habari za kimisionari Fides, Askofu huyo anayehusika na Huduma ya miito ya vijana,  alimulika hata hivyo umuhimu wa kuwashirikisha vijana katika kuishi matukio haya yanayowaleta karibu na Kristo na kuwasaidia kutambua safari yao ya ufundi.

Kuhusiana na idadi kamili ya washiriki ni bado hawawezi  kufanya makadirio rasmi yakuwa ni vijana wangapi watashiriki katika siku ya vijana (WYD) ambayo itafanyika kuanzia tarehe 1 hadi 6 Agosti 2023  kwa  maoni yake Askofu Villareal lakini anaamini kwamba kunaweza kuwa na karibu  vijana 30,000. Kati ya majimbo tisini ya  Mexico,  vijana kati ya 200 na 500 kwa kila Jimbo  wamejiandikisha kama ilivyoripoti Ofisi ya kichungaji ya vijana majimbo  na kama vikundi vya watu binafsi pia. Kuhusu jimbo kuu la Mji wa Mexico Askofu msaidizi alithibitisha kuandikishwa kwa vijana 89 kutoka Kitengo cha Ufundi cha Vijana pamoja na wengine wengi ambao wamejiandikisha kibinafsi, au kwa vikundi vya vijana, harakati na mashirika. Kikundi kitaondoka pamoja na majimbo ya Azcapotzalco, Iztapalapa na vijana waliojiunga mmoja mmoja kutoka majimbo ya Ecatepec, San Luis Potosí, Chihuahua, Texcoco na Xochimilco.

Kwa mijubu wa Askofu alisema “kwa mfano katika mkoa wa  Mji wa Mexico, vijana 190 wanaondoka Jumatatu  Julai 24”. Askofu huyo alisema  pia kwa kuzingatia WYD, kuanzia Desemba mwaka 2022 hadi Dominika  tarehe 9 Julai 2023 wakati Misa ya kuwatuma  ilipokuwa ikiadhimishwa, vijana walikusanyika katika mikutano 8 ya malezi, na  uhuishaji na maombi. “Kama askofu nilishiriki katika awamu mbalimbali za usindikizaji na uundaji wa kikundi kilichoandaliwa na Kitengo cha Kichungaji cha  Vijana kwa Jimbo Kuu la Mexico City. Na katika muktadha huo mhusika wa Ofisi ya kichungaji, Padre Alvaro Lozano Plattonof, ndiye anaondoka nao.

Wengi wa washiriki watarejea tarehe 12 Agosti 2023. Ratiba hiyo inajumuisha kupita madhabahu ya  Fatima kwa ajili ya baraka na kisha kuwasili katika Jimbo la  Algarve ambapo watakaribishwa na kisha kuendelea hadi Lisbon mnamo tarehe 1 Agosti, na kumalizia kutoka huko tarehe 9 Agosti hadi 11  watakuwa jijini Roma kwa kutoa shukrani. Kama sehemu ya uundaji na mwendelezo wa WYD, Askofu Villareal alisema kwamba: “wakati wa kurejea kutoka WYD hii, Kitengo cha kichungaji cha  Vijana kimepanga mikutano miwili ambayo vijana wataweza kuelezea tafakari zao za ufundi na kimisionari kutokana na tukio hilo”.

26 July 2023, 16:27