Tafuta

Maaskofu wa Burundi wakati wa ziara yao ya  kitume  mjini Vatican mnamo Machi 2023. Maaskofu wa Burundi wakati wa ziara yao ya kitume mjini Vatican mnamo Machi 2023.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Burundi yakosa rasilimali za kiuchumi ili kukaribisha vijana katika malezi ya kipadre

Nchini Burundi kuna miito mingi ya kikuhani,licha ya kukosekana majengo ya kukidhi haja ya malezi yao katika seminari kuu.Ni katika muktadha wa kufunga Jubilei ya miaka 125 ya Uinjilishaji itakayoadhimishwa tarehe 15 Agosti 2023.Jubilei ilizinduliwa rasmi kunako tarehe 1 Oktoba 2022.

Na Angella Rwezaula, - Vatican

Kuna ukosefu wa rasilimali za kiuchumi za kuweza kuwakaribisha watahiniwa vijana wengi katika maisha ya kikuhani nchini Burundi. Tarehe 15 Agosti, Kanisa Katoliki nchini  Burundi linajiandaa kuadhimisha matukio ya mwisho ya Jubilei ya miaka 125 ya Uinjilishaji, yaliyozinduliwa kunako tarehe 1 Oktoba 2022. Licha ya kuongezeka kwa harakati mpya za kidini na uwepo wa madhehebu mengine ya Kikristo, lakini pia ni umaskini mkubwa ambao idadi ya watu wanaishi nao, tangu miaka ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo havijawahi kuleta upatanisho wa uhakika. Pamoja na hayo yote katika miaka ya hivi karibuni Kanisa Katoliki nchini Burundi limeweza kuona ongezeko la idadi  ya waamini. Kwa hakika, kulingana na makadirio ya Kanisa mahalia, nchi hiyo imepata ongezeko la miito ya maisha ya kuwekwa wakfu na ukuhani.

Hali ngumu ya kiuchumi inatazama hata Kanisa nchini Burundi

Kutokana na hali ngumu za kiuchumi katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, seminari kuu zilizopo katika majimbo nane ya Kikatoliki haziwezi kukidhi maombi yote ya vijana watahiniwa  wanaoomba  kujiunga na kukubaliwa kila mwaka. Kwa hivyo uamuzi wa hivi karibuni umetolewa wa kuweza kuchukua idadi ya waseminari 13 tu kwa kila seminari.  Kwa upande wa nchi ya Burundi, theluthi mbili ya wakazi ni Wakatoliki huku asilimia 90 wakiwa Wakristo wa madhehebu mengine. Vile vile dini nyingine za kimila pamoja na aharakati mpya za kidini zinazidi kuibuka kila kuchao.

Kanisa katoliki Burundi

Kanisa Katoliki nchini Burundi, lina jimbo kuu katoliki la Bunjumbura yakiafuatia Majimbo yake ya Bubanza, Bururi na Rurana. Jimbo Kuu la Gitega, ambamo ndani mwake kuna Jimbo la Muyinga, Jimbo la Ngozi na jimbo la Ruyigi. Na kuna uhusiano mzuri wa Kanisa la Burundi na Vatican kwa sababu  Ubalozi wa Vatican nchini Burundi ulianzishwa mnamo tarehe 11 Februari 1963 na Hati fupi ya Christianae veritatis ya Papa Yohane XXIII.

Historia fupi ya Kanisa Katoliki nchini Burundi

Kwa kifupi  histori ya Kanisa  katoliki nchini Burundi liliona kuwasili kwa wamisionari wa kwanza wa Kikatoliki, walioitwa Wamisionari wa Afrika (White Fathers mnamo, mwaka 1879. Na mnamo mwaka 1895,  Burundi iliunganishwa na Vikariate ya Kitume ya Unyanyembe,   tunazungumzia (nchini Tanzania); na wakati huo huo mnamo mwaka 1912 iliunganishwa na Rwanda na kuunda vicariate ya Kivu. Kunako mwaka 1922 ilianzishwa vikarieti huru ya kitume inayojitegemea huko Burundi, ambayo ilikuwa na maisha yenye mafanikio makubwa. Na hii ni kutokana na kwamba upadirisho wa mapadre wa kwanza wazawa ulikuwa ni mwaka 1925.

1990, Mtakatifu Yohane Paulo II  aliitembelea Burundi

Mnamo mwaka wa 1959 uongozi wa mamlaka ya  maaskofu ulizaliwa na eno hilo kuwa Jimbo na mwaka uliofuata  yaani 1960, Burundi ikawa Kanda ya  kikanisa unayojitegemea kwa kuchaguliwa kuwa Jimbo Kuu la Gitega. Hata hivyo, vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka ya mwisho vilisababisha wahanga wengi, akiwemo hata Askofu mkuu wa Gitega, Joachim Ruhuna na Balozi wa Vatican  nchini Burundi, Askofu Mkuu Michael Aidan Courtney. Haitasahulika kamwe ziara ya Kitume ya Mtakatifu Yohane Paulo II wakati wa kutembelea Afrika mnamo ambapo alitembelea nchini Burundi mnamo 1990,

Uzinduzi wa Jubilei ya Miaka 125 ya Uinjilishaji nchini Burundi

Katika kuelekea kwenye tukio muhimu la Jubilei ya Miaka 125 ya Uinjilishaji nchini Burundi, Ibada ya Misa Takatifu iliadhimishwa katika Madhabahu ya Maria wa Mlima Sion Gikungu, katika mji mkuu wa Bujumbura na wakati huo huo wakifunga Jubilei za Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari (PMS) iliyofanyika mnamo tarehe 1 Oktoba 2022. Ibada ya Ekaristi Takatifu iliongozwa na Askofu Joachin Ntahondereye, wa Jimbo la Muyinga na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Burundi, pamoja na Baraza zima la Maaskofu, mbele ya Balozi wa Vatican nchini Burundi, Askofu Mkuu Dieudonné Datonou na Waziri wa Burundi Gervais Ndirakobuca, mapadre, watawa kike na kiume, waamini na wenge mapenzi mema.

Heshima kwa wamisionari wa kwanza wa Burundi

Katika mahubiri yake, Askofu Ntahondereye alikuwa ametaka mna kuenzi kazi kubwa ya Kardinali Charles Lavigerie, ambaye Kanisa la Burundi lina deni la wamisionari wake wa kwanza, na shukrani kwao  katika nchi hiyo ambayo imekuwa ikiinjilishwa tangu  mnamo mwaka 1897.  Kwa njia hiyo Askofu alibainisha kwamba Kardinali Lavigeria alitoa changamoto kwa waamini wa Kanisa Katoliki  ili kutilia maanani utume huo  wa thamani na zawadi ya kujua injili ya Kristo kupitia wamisionari. Katika mahojiano yaliyotolewa kwa vyombo vya habari nchini humo  wakati wa uzinduzi wa Jubilei hiyo , rais wa Baraza la Maaskofu wa Burundi alifichua viashiria vinavyoonesha ukomavu wa Kanisa katika nchi hiyo. Misa hiyo ilihitimishwa kwa kuwatuma vijana 120 wa ujumbe wa Injili katika majimbo manane yanayounda Kanisa Katoliki la Burundi.

Maskofu Katoliki nchini Burundi
Maskofu Katoliki nchini Burundi

Ndugu msomaji kumbuka kuwa: Charles Martial Allemand Lavigerie, M. Afr. alikuwa Kadinali wa Kikatoliki wa Ufaransa, na Askofu Mkuu wa Carthage na Algiers  barani Afrika. Na ndiye aliyeanzisha Shirika la Wamisionari wa Afrika(White Fathers).  Alipandirishwa  nchini Ufaransa, na kuanzisha hata  tume nyingi za kimisionari nchini Ufaransa.

Maaskofu Katoliki Burundi
Maaskofu Katoliki Burundi
28 July 2023, 17:56